SI KWELI Grafiki hii inayoonesha kuwa 'CHADEMA imemuua dereva wa Heche' ni halisi?

SI KWELI Grafiki hii inayoonesha kuwa 'CHADEMA imemuua dereva wa Heche' ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na graphic inayosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikidai kuwa kuwa na maneno yafuatayo "Kwa nini CHADEMA imemuua dereva wa Heche?"

Katika kufuatilia ju ya kile ambacho kimechapishwa imebanika kuwa graphic hiyo inapotosha umma kwa kutoa hitimisho lisiloungwa mkono na ushahidi kuhusu kifo cha aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Suezi Dani Maradufu, ambaye alifariki akiwa katika nyumba ya kulala wageni mkoani Kigoma.

Aidha, ufuatiliaji umeonyesha kuwa graphic hiyo imetengenezwa kwa kutumia nembo na muundo unaofanana na wa Jambo TV. Hata hivyo, chombo hicho kwa sasa kimefungiwa kufanya shughuli za utangazaji na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hivyo taarifa hiyo kubanika kuwa ni potofu

Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Tanzania kupitia mitandao yake ya kijamiii mechapisha taarifa kwa umma .Kwa mujibu wa taarifa hiyo, askari polisi walifika katika nyumba ya kulala wageni wakiambatana na Mrimi Zabron Mwita pamoja na wafanyakazi wa nyumba hiyo, baada ya kupokea taarifa kuwa mwenzao hakuwa akipatikana kupitia simu.

Polisi walieleza kuwa walikuta mlango wa chumba umefungwa na kulazimika kuuvunja mbele ya waliotoa taarifa. Baada ya mlango kufunguliwa, walimkuta Suezi Dani Maradufu akiwa amelala chini kifudifudi.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa katika uchunguzi wa awali ndani ya chumba hicho, zilipatikana dawa za binadamu za aina mbalimbali. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini chanzo halisi cha kifo kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yoyote inayohusisha chama cha CHADEMA au mtu yeyote na kifo hicho, wala halijathibitisha madai kwamba dereva huyo aliuawa.
Jambo leo.jpg
 
Hao ni CCM tu inajulikana mbona..na hizo ndiyo huwa Project za akina Mtela Mwampamba etc.
 
Back
Top Bottom