Gramaphone ya Mwalimu Subeti (1903 - 1974)

Gramaphone ya Mwalimu Subeti (1903 - 1974)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
GRAMOPHONE YA MWALIMU SUBETI SALUM
1578514791788.png

1578514732371.png

Mwalimu Subeti Salum Subeti
(1903 - 1974)

Mwalimu Subeti alikuwa mwalimu wa shule Kitchwele akifundisha useremala na pia alikuwa mmoja katika wapiga fidla (violin) maarufu wa Egyptian katika miaka ya 1940.n

Leo mwanae Hassan ambae ni rafiki yangu alikuja nyumbani kwangu mchana na zawadi adhim sana.

Hassan amenipa zawadi gramaphone ambayo marehemu baba yake alikuwa akiitumia kusikiliza muziki wa nyakati zile katika miaka ya 1940 hadi 50 kabla gramophone na santuri zake hazijatoweka kutokana na mabadiliko makubwa yalikuja katika vyombo vya muziki.

Hii granophone alikuwa ameihifadhiwa stoo kwa miaka mingi sana.

Gramopho zilizopo zinatumiwa kama pambo kupendezesha mandhari na zaidi utazikuta katika mahoteli makubwa ya kitalii.
 
Kosa kubwa tulilofanya nyumbani kwetu ni kutupilia mbali ile gramophone ya marehemu baba yetu. Ilikaa idle kwa muda mrefu baada ya record player na baadaye cassete player kutawala anga, tukaona kuwaumuhimu wa hiyo Garamohpne hauopo tena; tulikuwa tumeakiwa na santuri kama nne; nakumbuka Malaika, Teresa na Kilimanjaro. Haikuwa na sauti kubwa kwa vile ilikuwa haitumiee umeme, inabidi usikililize ukiwa umekaa pembeni. Leo hii Gramophone hiyo inaweza kuwa hazina.
 
Kichuguu,
Ninaweza kuandika kitabu kidogo kuhusu mimi na gramophone.

Kupitia gramophone ndipo nikiwa mtoto hata sijaanza darasa la kwanza nikiimba nyimbo za Kispanishi za Septet Habaner kutoka Cuba na ndipo nikicheza dansi nikimchana mama yangu mbavu kwa vile vituko vyangu.

Mama akinambia, ''Mohamed hii nakuwekea itakuwa zawadi yako siku ya harusi yako.
 
Back
Top Bottom