Gray Mgonja, mwenye kuonja vinavyoonjwa!


Around the same time RO naye alikuwa mlimani.....
Kalaghabao!!!!
 
you can't be serious Icadon.... this is too much.. but what are the chances though kwamba it is all coincidental kuwa Chuo kilikuwa kimoja na kwa vile karibu wote hawa wanakaribiana kiumri basi chances ni kuwa waliwahi kuwa mahali pamoja wakati fulani?
 

It will be like our generation in the next few years time, let us just pray that we may not inherit the same disease of forgetting the past. Nayaona mabadiliko huko mbele tunapokwenda, na wengi humu watakuwepo sehemu ya hayo mabadiliko. Swali gumu ni kuwa, kwa kuwa tunajuana, je tutalindana kama kizazi hiki kinavyofanya au tutaendelea kusimamia misingi tunayoihubiri sasa. Nilikuwa nasoma maandiko ya Museveni hivi karibuni akiwa kijana, nimepata hisia kwamba kadiri umri unavyokwenda pengine na mawazo nayo yanaanza kurudi kinyumenyume

JJ
 
Ni kweli, hii timu ya mafisadi ilishajiandaa tangu awali. Nadhaniw apo ambao walikuwa na siri yao kwa muda wote huo na wengine wamekutwa kwa bahati katika system, wakaunganishwa kuendelea kula nchi
 
Ndio Sababu Wanjiita Wanamtandao,
Mind You Kuna Watu Wengi Sana Pembeni Ambao Hawapo Kwenye Siasa.
Wako Pembeni Wanaendesha Bisahra Zao Kubwa Wanazoendelea Kufungua, Hawa Ni Mabilionea Na Wala Tusogope Kuwa Tukitaka Na Tukipania Hela Yetu Yote Itarudi.
Mahekalu, Mahoteli, Ma Skyscapers, Viwanda, Mabenki. Hela Bado Iko Kwenye Mzungupo, Pamoja Na Kuliwa Sana.
 
source;http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5890
mwandishi Muhibu Said, Dodoma
 
Hawa jamaa nafikiri hawasikii kitu. Kiburi kimewajaa. Wakati watu wanapiga kelele kuhusu ufisadi na jamaa amehusishwa na huo ufisadi bado anaruka na kufanya madudu mengine. Nafikiri JK ni wa kulaumiwa pia. Kwa nini anachagua watu walwale waliohusishwa au kusaidia ufisadi kwenye tume za kuchunguza ufisadi???
 
Na ndiye aliyekuwa instrumental katika kuweka delays kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni

Ufisadi si kuiba pesa tuu bali kuikosesha pesa mapato nayo inaconstitutre to IFISADI
 
Na ndiye aliyekuwa instrumental katika kuweka delays kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni

Ufisadi si kuiba pesa tuu bali kuikosesha pesa mapato nayo inaconstitutre to IFISADI

Huwezi jua labda alikuwa ameshaagiza Kivuko cha Kizushi kingine ili aendeelee kujilia Fwezaaa, Mimi naamini Mwisho wa Ufisadi upo karibu mno na watakuja watu wachache tuuu kufumua kila kitu sasa wazee wenye pressure mkae mkao wakula
 
Mgonja: Niacheni na ufisadi wangu

na Edward Kinabo
Tanzania Daima~Sauti ya watu

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeadhimisha mwaka mmoja, tangu kitangaze orodha ya majina ya vigogo 11 wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Gray Mgonja, mmoja wa watu waliotajwa katika orodha hiyo, amewataka waandishi wa habari wamwache na ufisadi wake.

Mgonja alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, alipotakiwa kueleza hatima ya azima yake ya kutaka kufungua kesi dhidi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na wenzake.

Akijibu swali hilo kwa jaziba, Mgonja alisema hana cha kueleza juu ya sababu iliyomfanya ashindwe kufungua kesi hiyo hadi leo na kuwataka waandishi wa habari kumwacha na ufisadi wake.

“Bwana hilo ni langu, niache na ufisadi wangu, sina lolote la kukueleza,’’ alisema.

Alipobanwa zaidi ataje ni kitu gani kimemchelewesha kufungua kesi na lini anatarajia kuifungua baada ya mwaka mzima kupita, Mgonja alikataa katakata kuzungumzia suala hilo.

“Tafadhali niache na ufisadi wangu, maana sitaki kabisa kuzungumzia hilo, wewe nenda, niache na ufisadi wangu, lakini uadilifu wangu ndio ulionifanya niwe kazini kwa miaka 33 sasa,” alisema Mgonja.

Hata hivyo kauli hiyo ya Mgonja ni tofauti na kauli aliyoitoa mara baada ya jina lake kuwa miongoni mwa watu waliotajwa kuhusika na ufisadi nchini.

Septemba 26 mwaka jana, 2007, Mgonja alifanya mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa hatajiuzulu wadhifa wake na kwamba anakusudia kumshitaki Dk. Slaa na wenzake kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi yake.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha, Mgonja alisema shutuma za Dk. Slaa na wenzake si za kweli, bali ni uzushi na upotoshaji uliolenga kuchafua jina lake.

“Kwa kuzingatia uzito wa tuhuma zilizotolewa kwa nia mbaya ya kunipaka matope na hasa nikizingatia uadilifu wangu wa miaka 33 bila kuwa na shutuma au kashfa ya aina yoyote, ili haki itendeke nimeamua kutumia mkondo wa sheria kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya Dk. Slaa, gazeti la Mwana Halisi na Kiwanda cha Printech kilichochapisha matoleo hayo,” alisema.

“Nitafungua kesi mapema iwezekanavyo na si lazima mjue kampuni itakayosimamia kesi yangu na wala siwezi kutaja kiasi cha fidia nitakachodai, nitasema mahakamani fidia nitakayodai,” alisema Mgonja.

Hadi sasa wote walioahidi kufungua kesi hawajafanya hivyo.

Wengine waliotajwa katika kashfa hiyo na kuahidi kufungua kesi ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Patric Rutabanzibwa.

Wengine waliotajwa katika kashfa hiyo lakini hawakusema kama wangekwenda mahakamani ni Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Yumo pia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Basil Mramba, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), marehemu Daudi Ballali.
 
Huyu naona kaamua kukiri mwenyewe tuhuma dhidi yake. Kilichobakia sasa hukumu!
 
Huyu naona kaamua kukiri mwenyewe tuhuma dhidi yake. Kilichobakia sasa hukumu!

Ni kweli kabisa (Niacheni na ufisadi wangu). Nadhani wahusika watachukua hatua zinazopaswa na karibuni tutapata taarifa za kufikishwa kwake mahali panapohusika
 
Huyu naona kaamua kukiri mwenyewe tuhuma dhidi yake. Kilichobakia sasa hukumu!

...............Tatizo la mafisadi wa Tz nadhani wanajua kuwa hata kama watakiri hadharani hakuna kitakachoendelea that's why mtu anakuwa na confidence kutamka hivyo....Mfumo wa sheria nadhani nao uko corrupt pia huyu alitakiwakubebwa juu kwa juu mpaka mahakamani akaleze vizuri huko huko....
 
ni kweli kabisa (niacheni na ufisadi wangu). Nadhani wahusika watachukua hatua zinazopaswa na karibuni tutapata taarifa za kufikishwa kwake mahali panapohusika

cha kufurahisha ni jinsi alivyobadili kauli na kuonyesha kabisa kwamba kale ka-kiburi ka mwanzo kameishia kwenye kimo chake sahihi na si kile alichotuonyesha mwaka jaNa
 
Ukiona hivyo ujue jamaa kishaandika barua ya ku resign
 
Ni kweli kabisa (Niacheni na ufisadi wangu). Nadhani wahusika watachukua hatua zinazopaswa na karibuni tutapata taarifa za kufikishwa kwake mahali panapohusika

I doubt if anything will be done to punish for what he has done!
 
Ukiona hivyo ujue jamaa kishaandika barua ya ku resign

Na kama ni kweli, masikitiko makubwa ni kwamba ishu itaishia hapohapo, hakutakuwa na hatua zaidi. Nasikia hata watoto wadogo siku hizi bongo wanajua wakitenda kosa ikifikia hatua ya kuadhibiwa wanasema "basi najiuzulu", yaani imekuwa kwamba "kujiuzulu" ni sawa na "kujichukulia msamaha" na wala si hata kuomba msamaha.
 

Aliwafundisha baba yao Lowassa jinsi ya kumuomba JK msamaha ili in future akurudishe madarakani na kukutetea kwa uadilifu wako na kutokuwa na tamaa ya madaraka!
 
Hivi inakuwaje hakuna anayetaka kumshitaki mwenziwe??;
1. List of Shame vs Dr. Slaa
2. Dr. Slaa vs Mtikila n.k.

Huko mahakamani haki haitendeki au wahusika wanaogopa kitu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…