Green banana needed in Turkey & Afghanistan

J Mbungi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
269
Reaction score
74
Wapendwa Wanaboard wenzangu..Kuna fursa ya biashara ya Ndizi mbichi kwenda Turkey na Afghanistani..Kwa kuanzia tujadili na kufahamishane ni namna gani tunaweza kufanya hii biashara.. Nina Kampuni imeniapproach.. Wanataka kusupply Ndizi Mbichi(Green Bananas) Kutoka Tanzania Kwenda Uturuki kwa njia ya Majini(Kwa kutumia Bandari ya Dar Es Salaam na Mersin(Uturuki)..

Kwanza ningependa kujua uwezekano wa kufanya hii biashara..Je inawezekana? Tunaweza kuzi fanyia Packaging namna gani zikafika zikiwa mbichi? Je kuna meli maalum au macontainer ya baridi(Freezer/Cold Rooms ambazo zinaweza kutumika?

Kwa mtu ambaye yupo serious naomba tusaidiane information na Kama... it is real feasible?..

Kokotoa gharama za packaging and transporting up to Mersin harbour Turkey..Then tuone Kilo moja inaweza kuuzwa bei gani..

NOTE: Ikiwa deal hii inakaa sawa na upatikanaji wa Ndizi nzuri zenye UBORA upo...Na kwa Bei itakayo kubalika kwa mununuzi...Tutafanya mkataba kabisa na hii Kampuni kwa kuanzia ya mwaka mmoja..Na kila mwezi tuwe na uwezo wa ku EXPORT TANI 100..! Mwenye anafikiri tunaweza kufanya kitu ani- PM kwenye INBOX na details..
 

imekaa vizuri sana, kila la kheri wakuu
 

Ni Aidea nzuri sana, Ila belive me kwenye hiyo kiasi ni vigumu sana kuweza kumeet utaishia kukimbia, na si banana tu unakuta kuna makampuni yanahitaji mfano mafuta ya alizeti ambayo hajasafishwa na unakuta wanahitaji tani za kutosha kiasi kwamba unaweza kusanya mafuta nchi nzima bado usifikie.

Uturuki iko Ulaya na ulaya kwa maswala ya Afya wako mbele sana, kuna mlolongo wa mambo ya kufanya kabla ya ku export hasa chakula nje hasa ulaya na kazalika, procedure ni nyingi sana na it will take a time kuja kupata vibari vyote vya ku export.

Some time huwa wanahitaji kuona shamba lako na hapo ndo huwa shida ilipo, Na ili ku meet standard huwa ni bora sana uwe na shamba lako mwenyewe ambapo unaweza meet standard zao ila ukitegemea kuchukua kwa wakulima wengine inakuwa ngumu sana.

Na ili Kumeet ubora ni lazima uwe unazichukua sehemu moja tu, kwa sababu wale hupima sample kila unapo export unaweza kuta ndizi zingine zilipigwa sijui madawa gani ikaja kuleta shida.
 
Kila la heri mkuu...

Tani 100 ni mzigo wa haja, ila uki-win umeukata
 
Ahsante kwa mchango wako wenye tija..Haya masuala yote nitayajadili na huyu muhitaji NDIZI..Lakini kabla ya huko ninahitaji kupata information na mambo kama haya ya upatikanaji wa NDIZI napengine kadrio la bei ya kuuzia hizi ndizi.. Than once again..!
 

Kwa kiwango hicho ni kwamba ni lazima kukusanya kwa wakulima wengi sana, na hii inakuwaga nzuri endapo unaingia contract na wazalishaji ili wakuuzie ndizi la sivyo siku unahitaji utashangaa wanakuwa wameisha uzia watu wengine, ni kazi moja ngumu sana kupata mzigo wa kiwango hicho.
 
Tukuyu inazalisha ndizi nyingi sana za aina tofauti. Tatizo la la hao atu wa ulaya wanaaina ya ndizi wanazotaka sio kila ndizi na uzalishaji wa ndizi ya aina moja ni mgumu kwa wakulima wadogo kwani hutegemea kwa chakula ndizi hizohizo. Jaribu kuuliza upate taarifa kamili juu ya hili. Kuna mzungu alienda tukuyu kutaka kulima ndizi za kusafirisha lakini alikosa eneo la kulima. Pia wewe ndio uulize bei ya ndizi huko soko la ulaya ipoje kisha ulinganishe ya huku. Mkungu ulioshiba wa kibiashara unauzwa kati ya sh. 5000 na 8000.
 
Inabidi uwe na maagent mikoa yote inayolima ndizi

Uwe na storage facilities za kufa mtu

Na pia unatakiwa uwe na uniformity sio mara leo unakusanya mshale, kesho mkuki, kesho kutwa upinde.

Hii deal nzuri sana, kusanya team ya ukweli.
 
Mkuu Ndizi si lazima ziwe za aina moja(Ila zile ndefundefu na zilizoshiba ndio ninazotaka....Kama kuna uwezekano wa kupigapicha au kumuamba ndugu/rafiki aliye karibu na ndizi apige picha anitumie..Nadhani tunaweza kufanya biashara hii..Kwasababu ndizi zinazohitajika kwa mwezi ni nyingi..Tunaweza kuingia mkataba na wakulima kabisa(100.TANI mia Moja)..Alafu Kwa makadirio ya Kilo..Mkungu mmoja unaweza kupima kati ya kilo ngapi??!
 
umeharibu ulivyosema watu waku pm.
unajua hapa kuna watu wana idea nyingi ambapo mtu akiandika wazo lake hapa watu wanalichallenge alafu mwisho wa siku utapata jibu.
_all ze best mkuu
 
Kiongozi ukienda Mkoa wa Kagera unaweza kufanikiwa kupata ndizi kiasi hicho unachosema. Mkoa huo ulikuwa na Mradi wa Ndizi za kisasa kwa ufadhili wa Ubelgiji. Wakulima wengi wamebadilisha ulimaji wa ndizi na sasa hivi wana migomba na ndizi bora. Maeneo ambayo yameboresha zao hilo ni Ngara, Biharamulo,Karagwe. Wasiliana na Maafisa Kilimo wa wilaya hizo au Mkoa watakujuza zaidi!
 

Mi mgeni sina 5 posts, so siwezi ku'pm.. Ni'pm wewe namba yako... Nna dili na kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…