Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Nafikiri hapa kinachoongelewa ni uwezekano wa mafanikio. Mafanikio iwe Bongo au nje hayaji kwa matamshi tu. Watu wengi waendao USA, Canada, na UK kama wana nyenzo (elimu inayouzika wanafanikiwsa. Kama mtu una kazi TZ yenye kipato kizuri, sishauri uende Majuu. Lakini kama wewe ni kati ya vijana wakiyohitimu chuo, high schoo, na sekondari, ukienda USA na una nia ya kuendelea kipesa wewe nenda tu. Ukipata green card, siyo lazima uhamie. Unaweza ukajibana ukatafuta mtaji ili uje kujiendeleza TZ. Kuna kijana alishinda hiyo green card. Yeye alipofika huku hakutaka hata kusikia habari ya shule (nafikiri liiogopa). Yeye alipata kazi kiwanda, analipwa $19 kwa saa. Baada ya mika mitatu tayari alikuwa na tekta mbili. Sasa hivi anajenga appartments. TZ alipewa mkopo na benki na anauservice kwa pesa anayolipwa huku. Angekuwa TZ asingekuwa alipo.

Ni kweli siyo kila anayekuja huku hufanikiwa. Ikiwa wananchi wenyewe wa huku hawafanikiwi, itakuwa wa kuja. Ila ukweli ni kuwa uwezekano wa kupta mtaji ni mkubwa kuliko TZ. Ila napo ukienda ukajiingiza kufurahia mbususu za kizunbgu, mafanikio utayasikia tu. Ushauri wangu kama una nafasi nzuri TZ, usihangaike, lakini kama unabangaiza, jaribu bahati yako and you will not regret.
 
Stories za vijiweni hizo
Ila ukweli utabaki palepale USA ndio dream country kwenye kutafuta maisha kwa kila mtu hapa duniani hivi wachina wajapan waarabu sijui takataka gani zote zinatamani kwenda huko wewe wa maji chumvi huku unajitutumua eti hakuna cha maana huko..utakuwa na shida sehemu sio bure uwivu na husda vimekujaaa.
 
Kenya mnayoishobokea over 30M wanataka kwenda nje, wabongo mnataka mbaki ndani tu
 
Ushoga ni fursa pia, ndio hapo ninaipendea Marekani. China kila kitu ni chakula na Marekani kila kitu ni fursa,
 
Mtumie ps4 kavuluta afungue play station hana hata kazi huku yupo kwenye kijiwe cha kahawa pale lumumba anajibishana uzalendo.
 
Mtumie ps4 kavuluta afungue play station hana hata kazi huku yupo kwenye kijiwe cha kahawa pale lumumba anajibishana uzalendo.
Wewe goal yako kuu ni kupambana kwa hali na Mali hata kwa kuu tako lako moja ili kupata financial freedom. Sisi wenzio tunapqmbania kupata total freedom yetu, jamii na taifa lote kwa do or die tukiwa humuhumu. Hata hako kaahueni wanakokapata weusi pale Marekani ilikuwa ni kazi ngumu ya akina Martin Luther king na wenzake, kalipatika kwa jasho na ujasili sio kwa kuwaza kiboyaboya kama wanavyowaza watafuta greencard ili kukimbia matatizo kwao, huo ni uboya uliokithili kiwango. Huwezi kukimbia tatizo labda uwe umebemendwa akili. Mungu hakuwa mjinga kutuweka sisi Tanzania.

Do not uproot the pumpkin at your home state (Chinua Chebe)
 
Mkuu tofauti na Green card njia gani nyingine salama na ya uhakika naweza kutumia kufika hiyo nchi ya ahadi?

Green card nimeapply, nasubiri tokeo japo hiyo siwezi kuitegemea sababu ni bahati nasibu
 
Ushoga ni fursa pia, ndio hapo ninaipendea Marekani. China kila kitu ni chakula na Marekani kila kitu ni fursa,
Ama kweli! Unazidi kujiweka wazi! Kuipenda kwako Marekani ni fursa ya Ushoga! Kweli una mambo umenipe Nukuu nyingine ya wiki!
 
Kuna watz wengi wanaishi South Africa,Botswana,Malawi ect hao nao ni watumwa?mbona mnawasakana warz wanaoishi USA tu?
Kamongo,

Inashangaza sana, nadhani kuna wakati madaktari, manesi na hata engineers walioko kwa wingi kwenda Botwasana, It was exodus ya aina yake, lakini hakukua na kelele za umanamba, utumwa!

Huwa naogopa ni wivu au chuki binafsi na Marekani? Na hata kama unaichukia Marekani, kwa nini unichukie na mimi niliyekuja kutafuta maisha Marekani.

Waarabu in general wanaonekana wana chuki na Marekani ukiangalia kwenye Media, lakini ukweli unasema tofauti! Nadhani kwa miaka mingi wao ndio wanaongoza kuleta watoto kusoma na kuwekeza!

Kuni kipindi fulani nikiwa Tanzania tulitembelewa na auditor mmoja mwenye asili ya kiarabu toka Sudan lakini ni Mmarekani, na alikuwa mtu wa dini hasa, mimi ndiye niliye kuwa mwenyeji wake Tanzania, kumuonyesha wapi akitaka kusali Ijumaa nk! (Mimi sio mwislamu) Katika ushauri alionipa, kabla hajarudi US, yaani jinsi kufanikiwa katika shirika letu na mambo ya kawaida tu ya maisha, alitoa Passport ya Kimarekani mfukoni mwake, na kuniambia " Ukijaribu kupata hii" akionyesha Passport ya Kimarekani Itakusaidia sana mambo yako!

Aliniambia uwazi, yeye akiwa Mwarabu na Muislamu hapendi baadhi ya Mambo ya Marekani, lakini kuwa Mwamerika imemsadia sana yeye na familia yake! Nilipokuja Marekani nilimtafuta Atlanta na kusema, Asante!

Waswahili walisema Baniani mbaya kiatu chake dawa!
 
Kenya ni manamba tangu ukoloni hadi Leo. Hawajawahi kupata Uhuru kamwe, ni hustlers since then. Tabu tupu
Hakuna anayeishobokea Kenya! Bila kujua mfumo wetu Tanzania unatengeneza Hustlers wengi, na wasomi kama nyinyi hamtoi kabisa solutions! Ila nikuulize since then Tanzania haijawa Tabu tupu! Hujui watanzania waliondolewa vijiji vya asili, kuanzisha vijiji vya Ujamaa, viko wapi leo! Nadhani huja experience foleni za unga wa yanga, sabuni, na kuwa dawa za mswaki mbili unaweza kusweka rumande! Unajua waliojinyonga kwa kucheleweshewa mafao yao! Hujui tabu tupu ya Kenya mnaitengeneza kwa spidi kubwa Tanzania.

Leo tunajengewa vyoo kwa msaada toka nje! Je hiyo sio tabu tupu!

Tuko page ya 15 kwenye hii mada, hujasema lolote la kufanya kuwasaidia hao hustlers mnaowatengeneza! Sana sana ni kuwapa Vibali vya umachinga!

Sisi tuliko mbali, tunapoombwa na graduate PS3/P4 afungue biasahara ya kuchezesha game! tunaona nchi inakwenda wapi! Ila wewe msomi, ulayejaza Passport kwa kuzunguka duniani huoni umezungukwa na time bomb!

Unapopokelewa Airport na V8, na dereva wa Serikali, unapopita Tazara, Buguruni, Ubungo, unashindwa hata kufikiri solution ya hao wamachinga na bidhaa wakizunguka gari lako! Unapoona Boda boda na Bajaj wakikatiza mbele yako, unasema wana kera hawa!

Bila kujua ni kodi zao ndio zimefanya Passport yako kujaa visa za nchi mbali mbali! Unabakia kusema Tanzania ina fursa, Tanzania ina fursa!

Jumapili Njema!
 

Naona wewe umetafuta solution ya Matatizo ya Tanzania, kwa kuongeza safari za Marekani! Maybe ndio ulio design vitambulisho ya Wamachinga! Na labda uko behind Tozo!

Huko ndiko kutafuta solution za matatizo ya Tanzania! Unaniambia eti natamani Elon Musk ainunue Tanzania! Mbona attempts nyingi za kuiza nchi zinafanyika hapo hapo na hao mliowakabidhi nchi! Hawana Greencard! bali wana Green shirts! Na proposals za kuuza nchi mnazipitisha huko huko Ma wizarani!

Vilio vya kusema nchi ineuzwa huwa vinatoka wapi? Hapo hapo bongo!

Your perception of reality is completely obscured!
 
Tabia za kukatishana tamaa watz wengi wanazo,hizo tabia hata watz walio nje wanazo ukitaka kijiendeleza kielimu wankukstisha tamaa.
Watz wana roho mbaya kama watusi tu
 
Tabia za kukatishana tamaa watz wengi wanazo,hizo tabia hata watz walio nje wanazo ukitaka kijiendeleza kielimu wankukstisha tamaa.
Watz wana roho mbaya kama watusi tu
Mkuu, wengine hatujaitwa kuwa wana siasa au matajiri kama Bhakheresa maskini waje tuwape chochote, lakini katika safari hii fupi ya maisha unaweza kumsaidia mwenzio kilicho katika uwezo wako, wengi tuna experience fulani, basi share na wenzio! wakifanikiwa zaidi yako inakuuma nini! Hushindani na mtu, tunapishana pishana tu ulimwenguni kisha tunaondoka!
Nimefika hapa nilipo, nikiondoa wazazi wangu kuna mikono ya wengi! Na hata wengine waliisha ondoka duniani sijui jinsi ya kuwalipa! Walinipa mawazo, moral support nk! Niliwahi kukwama Bangkok, Thailand ( Nili over spend) Nikaishwia kabisa! Na ATM Card yangu iligoma, Aliyenikwamua ni Mkenya nisiyemjua! Alinipa pesa nikaondoka haraka! Sijui hata nitampata wapi kutoa shukrani! Hakujibu contacts alizonipa.

Na kwenye hii post najaribu tu kutoa chochote au hata kuwapa watu matumaini kuwa kuna njia mbadala kama options za nyumbani zimefungwa, ni hilo tu. Sasa huo ndio unaitwa Usaliti na kukosa uzalendo!
 
Nakubaliana na wewe ila watz tuna chuki mtu roho inamuuma kisa fulani anaishi USA,
 
Naona una mawazo ya ajabu sana! Hujui hapo bongo kuna wanaoshikishwa ukuta! Na unajua kabisa maana umeelimika, huo ushoga ni tabia tu, nothing to do with poverty! Naona wewe hujui mambo mengi na kijana wa leo uliyetoka vijijini ukaja Dar! kuna baadhi ya wenye tabia hizo Tanzania walikuwa wenye nafasi kubwa serikalini na watoto wa matajiri! Siwezi kutaja majina yao, wanafahamika!

Na hata huku walio katika ugonjwa huu ( mtazamo wangu) ni watu highly educated and financially well off!

Halafu naona una ugonjwa wa kusahau! Huyu sio Chinua Achebe aliyeandika usemi huu " Do not uproot pumpkin in the old homestead" Ni Okot P Bitek - Song of Lawino

Weekend Njema
 
Mkuu tofauti na Green card njia gani nyingine salama na ya uhakika naweza kutumia kufika hiyo nchi ya ahadi?

Green card nimeapply, nasubiri tokeo japo hiyo siwezi kuitegemea sababu ni bahati nasibu
Kaka hiyo sio bahati na sibu bali ni vigezo kama vitatimia. Wakati ulee wa utumwa vigezo vilikuwa uwe kiji pandikizi la Mirada 4, yaani jitu refu kama Hashem Thabiti na lenye nguvu kama Schwarzenegger na R Kelly kwakuwa kazi zilikuwa ni mashambani, viwandani na bandarini, Lakini Sasa hivi vigezo ni elimu (masters, PhD) kwenye maeneo wenye uhaba nayo wa watumishi, lottery inabakia kwa watu wasiokuwa na elimu ya juu kwa blue collar kama za mashambani
 
Watu wa kanda ya kaskazini ndio wako after financial freedom zaidi kuliko hata usalama wao, ndugu, jamaa na hata taifa. Nonsense
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…