Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Daah! umenena, nini nafahamu kuwa furahi ya mtu haitokani na kuwa na pesa nyingi tu bali mjumuiko wa mambo mengi na hela ikiwemo. Nimekutana na kijana ambae huko majuu ambae analala kwenye gari yake maisha, nilipomuuliza kwanini kwanini huna chumba chako aliniambia ninafanya kazi shift 3 kwa siku hivyo muda wa kulala sina, hata hiyo nyumba naona nitapoteza pesa zangu bure wakati silali humo. Akanambia ana madeni mengi yanayohitaji ku service (kulipa) hivyo lazima afanye kazi zaidi ya 1 ili apate ziada. kaka kijana huyu hajawahi kula chakula cha nyumbani kwake zaidi ya kule fast foods mitaani, makato mengi na anashindwa kutuma pesa nyumbani maana wafyeka hela nyingi sana. kaka kuna mitaa/maduka/malls ukiingia mwenye ngozi nyeusi wanadhani huna pesa ya kuingia hapo bali unataka kuiba, ubaguzi bado haujakwisha tunalazimisha tu.

Nguvu, muda, juhudi, maarifa na akili mnazozitumia kumudu kuishi huko hata zingewekezwa japo nusu tu kwenye jangwa zingetoa matunda. Vijana wetu huku ni wavivu sana ni wavivu sana na ni wavivu sana ndio maana wanapata tamaa ya green card wakidhani huko US pesa ziko kwenye viroba tu ni za kuzoa na kutumia.

Kama asili na chanzo kikuu cha ushoga huko ni maisha magumu, watu wanaunganisha nguvu ili kumudu maisha bila kulazimika kuwa na watoto wa kutunza, yaani kuona mwanamke ni kuongeza ugumu kwenye ugumu. bahati mbaya mimi nimeishi huko sana tena vijijini kabisa ambako maisha ni kama haya hapa ya tandika na kwamtogole, kuchafu na idadi kubwa ya ombaomba wazungu mitaani ambao wanapatiwa nguo kule salvation army na kwingineko kwenye malls kama vile Walmart zenye madirisha ya watu maskini (wazungu) kupatiwa misaada.

kaka usiwadanganye watu ukawapa hope na kuja kuishia kuolewa na wanaume wenzao, wanaofanikiwa ni watu kidogo sana kati ya hao wahamianji. Wengi wao wanaishia kwenye vyombo vya usalama kufungwa na hata kuuliwa.
Nafikiri hapa kinachoongelewa ni uwezekano wa mafanikio. Mafanikio iwe Bongo au nje hayaji kwa matamshi tu. Watu wengi waendao USA, Canada, na UK kama wana nyenzo (elimu inayouzika wanafanikiwsa. Kama mtu una kazi TZ yenye kipato kizuri, sishauri uende Majuu. Lakini kama wewe ni kati ya vijana wakiyohitimu chuo, high schoo, na sekondari, ukienda USA na una nia ya kuendelea kipesa wewe nenda tu. Ukipata green card, siyo lazima uhamie. Unaweza ukajibana ukatafuta mtaji ili uje kujiendeleza TZ. Kuna kijana alishinda hiyo green card. Yeye alipofika huku hakutaka hata kusikia habari ya shule (nafikiri liiogopa). Yeye alipata kazi kiwanda, analipwa $19 kwa saa. Baada ya mika mitatu tayari alikuwa na tekta mbili. Sasa hivi anajenga appartments. TZ alipewa mkopo na benki na anauservice kwa pesa anayolipwa huku. Angekuwa TZ asingekuwa alipo.

Ni kweli siyo kila anayekuja huku hufanikiwa. Ikiwa wananchi wenyewe wa huku hawafanikiwi, itakuwa wa kuja. Ila ukweli ni kuwa uwezekano wa kupta mtaji ni mkubwa kuliko TZ. Ila napo ukienda ukajiingiza kufurahia mbususu za kizunbgu, mafanikio utayasikia tu. Ushauri wangu kama una nafasi nzuri TZ, usihangaike, lakini kama unabangaiza, jaribu bahati yako and you will not regret.
 
Unachosema wewe ni sawa na house girl ambae anafanyakazi kwa boss wake kuanzia alfajiri na kulala saa 5 usiku baada ya kumalizia kumfungulia na kumlisha mbwa kutoka bandani kwa ujira wa TZS 60,000 kwa mwezi. Lakini msichana huyu alipokuwa kwao alikuwa anaamka saa 2 asubuhi, kuzurura, kuangalia TV na kwenda kulala saa 2 usiku.

Nguvu, juhudi na muda anaotumia kufanyakazi kwa boss kama angetumia nusu tu ya nguvu,juhudi na muda kufanyakazi akiwa nyumbani kwao hata kwa kuchoma vitumbua na maandazi na kuyauza angepata pesa nyingi zaidi hukohuko kwao kuliko hizi 60,000 za boss.

Fursa ziko hapahapa nyumbani Tz ni kuacha uvivu. Nilimkuta kijana mmoja Marekani anaona aibu kurudi Tz kwakuwa wenzake aliowaacha TZ walikuwa na maendeleo makubwa sana kuliko yeye. Wenzake wameoa, wana mashamba ya miti Iringa, wamejenga kule Goba, shamba kubwa la kuku, wana magari na ardhi kubwakubwa tu. Visa yake na passport vimekwisha lakini anashindwa kurudi kurudi kwa kuogopa kuwa atadakwa kwa makosa hayo pia.

Hebu waambieni ukweli vijana wenu.
Stories za vijiweni hizo
Ila ukweli utabaki palepale USA ndio dream country kwenye kutafuta maisha kwa kila mtu hapa duniani hivi wachina wajapan waarabu sijui takataka gani zote zinatamani kwenda huko wewe wa maji chumvi huku unajitutumua eti hakuna cha maana huko..utakuwa na shida sehemu sio bure uwivu na husda vimekujaaa.
 
Kenya mnayoishobokea over 30M wanataka kwenda nje, wabongo mnataka mbaki ndani tu
IMG-20221111-WA0037.jpg
 
Kwani mwenye Greencard hana uwezo wa kukaa Marekani na kuja Tanzania na kuondoka? Je unajua with American Passport naweza kufanya hivyo? Kwangu mimi kila mahali ni best mradi mambo yangu yanaenda! With my American Passport imeongeza wigo wangu mkubwa wa kwenda, kukaa napotaka! Hata kuja kujenga kijijini kwako!

Nimekuambia mara elfu, sikushawika na mtu kuja Marekani! Na simshawiti yoyote kama anaona mipango yake inafanikiwa Tanzania kuja US.

Nawaonyesha options tu kwa wale ambao wanaona milango yao imefungwa Tanzania! Sijui kwa nini hunielewi!
Ushoga ni fursa pia, ndio hapo ninaipendea Marekani. China kila kitu ni chakula na Marekani kila kitu ni fursa,
 
Hii ndio hoja yangu! Lakini kwa nduguyo Kavuluta yeye ni tofauti, nashangaa anavyokuwa illogical, irrational etc Kuja nje ni kukosa uzalendo! Wakati hao tunaowaita Wazelendo ambao wapo hapo hapo nchini, ndio leo mnawatuhumu kwa ufisadi! Hakuna mwenye Green card

Tuwewapa nafasi, tumekuja kutafuta ugenini, imekua kosa! Tunajaribu kuwaambia vijana ambao wamekosa fursa imekuwa tabu! Fursa zimenyimwa na hao hao mlio nao ndani! Kwa kifupi kabisa siwaelewi!

Ndugu yako Kaluvuta ameniita nimekimbia shida nk! Angelijua maisha yangu angeniita mtoto wa fisadi! Nimeogopa kutoa CV yangu angesema najimwambafy! Passport ya kwanza i ilijaa 2005! Sijui nimebadili Passport mara ngapi!

Baba yangu mzazi Mungu amuweke mahali pema peponi alianza kunipandisha ndege nikiwa na miaka kumi na mitatu, na kunipa broader perspective ya kuangalia maisha nje ya Tanzania! Mdogo wangu wa kike anaishi Nerthaland, wa kiume kasomeshwa Canada, Wakike mdogo kaishi Germany, watoto sita wote tumezunguka ulimwenguni. Hivyo najua nachofanya! Sina chochote cha uhaini! Nataka na wengine wajaribu! Imekua Nauza nchi!

Tunajaribu kuwasaidia Watanzania tu! Hatuna nia ovu hata kidogo! Lakini inaonekana hatueleweki!

Asante Mkuu!
Mtumie ps4 kavuluta afungue play station hana hata kazi huku yupo kwenye kijiwe cha kahawa pale lumumba anajibishana uzalendo.
 
Mtumie ps4 kavuluta afungue play station hana hata kazi huku yupo kwenye kijiwe cha kahawa pale lumumba anajibishana uzalendo.
Wewe goal yako kuu ni kupambana kwa hali na Mali hata kwa kuu tako lako moja ili kupata financial freedom. Sisi wenzio tunapqmbania kupata total freedom yetu, jamii na taifa lote kwa do or die tukiwa humuhumu. Hata hako kaahueni wanakokapata weusi pale Marekani ilikuwa ni kazi ngumu ya akina Martin Luther king na wenzake, kalipatika kwa jasho na ujasili sio kwa kuwaza kiboyaboya kama wanavyowaza watafuta greencard ili kukimbia matatizo kwao, huo ni uboya uliokithili kiwango. Huwezi kukimbia tatizo labda uwe umebemendwa akili. Mungu hakuwa mjinga kutuweka sisi Tanzania.

Do not uproot the pumpkin at your home state (Chinua Chebe)
 
Mkuu kuja Marekani sio kusaliti nchi, achana na vipofu wasiojua kitu! Wasaliti mnao hapo hapo!

Ndio maana kila mara,Ngorongoro imeuzwa! Mara Twiga na Tausi wamepelekwa sijui Oman! Mara Richmond, Mara pesa za EPA! Mara mabehewa ya makinika! Mlolongo kibao!
Je hao wametoka Marekani! Je wana Greencard!? Mnapishana nao wakiwa ndani ya viyoyozi na V8! Mnasalitiwa mchana kweupe!
Tengeneza maisha yako jamaa yangu! Iwe bongo au popote pale!
Mkuu tofauti na Green card njia gani nyingine salama na ya uhakika naweza kutumia kufika hiyo nchi ya ahadi?

Green card nimeapply, nasubiri tokeo japo hiyo siwezi kuitegemea sababu ni bahati nasibu
 
Ushoga ni fursa pia, ndio hapo ninaipendea Marekani. China kila kitu ni chakula na Marekani kila kitu ni fursa,
Ama kweli! Unazidi kujiweka wazi! Kuipenda kwako Marekani ni fursa ya Ushoga! Kweli una mambo umenipe Nukuu nyingine ya wiki!
 
Kuna watz wengi wanaishi South Africa,Botswana,Malawi ect hao nao ni watumwa?mbona mnawasakana warz wanaoishi USA tu?
Kamongo,

Inashangaza sana, nadhani kuna wakati madaktari, manesi na hata engineers walioko kwa wingi kwenda Botwasana, It was exodus ya aina yake, lakini hakukua na kelele za umanamba, utumwa!

Huwa naogopa ni wivu au chuki binafsi na Marekani? Na hata kama unaichukia Marekani, kwa nini unichukie na mimi niliyekuja kutafuta maisha Marekani.

Waarabu in general wanaonekana wana chuki na Marekani ukiangalia kwenye Media, lakini ukweli unasema tofauti! Nadhani kwa miaka mingi wao ndio wanaongoza kuleta watoto kusoma na kuwekeza!

Kuni kipindi fulani nikiwa Tanzania tulitembelewa na auditor mmoja mwenye asili ya kiarabu toka Sudan lakini ni Mmarekani, na alikuwa mtu wa dini hasa, mimi ndiye niliye kuwa mwenyeji wake Tanzania, kumuonyesha wapi akitaka kusali Ijumaa nk! (Mimi sio mwislamu) Katika ushauri alionipa, kabla hajarudi US, yaani jinsi kufanikiwa katika shirika letu na mambo ya kawaida tu ya maisha, alitoa Passport ya Kimarekani mfukoni mwake, na kuniambia " Ukijaribu kupata hii" akionyesha Passport ya Kimarekani Itakusaidia sana mambo yako!

Aliniambia uwazi, yeye akiwa Mwarabu na Muislamu hapendi baadhi ya Mambo ya Marekani, lakini kuwa Mwamerika imemsadia sana yeye na familia yake! Nilipokuja Marekani nilimtafuta Atlanta na kusema, Asante!

Waswahili walisema Baniani mbaya kiatu chake dawa!
 
Kenya ni manamba tangu ukoloni hadi Leo. Hawajawahi kupata Uhuru kamwe, ni hustlers since then. Tabu tupu
Hakuna anayeishobokea Kenya! Bila kujua mfumo wetu Tanzania unatengeneza Hustlers wengi, na wasomi kama nyinyi hamtoi kabisa solutions! Ila nikuulize since then Tanzania haijawa Tabu tupu! Hujui watanzania waliondolewa vijiji vya asili, kuanzisha vijiji vya Ujamaa, viko wapi leo! Nadhani huja experience foleni za unga wa yanga, sabuni, na kuwa dawa za mswaki mbili unaweza kusweka rumande! Unajua waliojinyonga kwa kucheleweshewa mafao yao! Hujui tabu tupu ya Kenya mnaitengeneza kwa spidi kubwa Tanzania.

Leo tunajengewa vyoo kwa msaada toka nje! Je hiyo sio tabu tupu!

Tuko page ya 15 kwenye hii mada, hujasema lolote la kufanya kuwasaidia hao hustlers mnaowatengeneza! Sana sana ni kuwapa Vibali vya umachinga!

Sisi tuliko mbali, tunapoombwa na graduate PS3/P4 afungue biasahara ya kuchezesha game! tunaona nchi inakwenda wapi! Ila wewe msomi, ulayejaza Passport kwa kuzunguka duniani huoni umezungukwa na time bomb!

Unapopokelewa Airport na V8, na dereva wa Serikali, unapopita Tazara, Buguruni, Ubungo, unashindwa hata kufikiri solution ya hao wamachinga na bidhaa wakizunguka gari lako! Unapoona Boda boda na Bajaj wakikatiza mbele yako, unasema wana kera hawa!

Bila kujua ni kodi zao ndio zimefanya Passport yako kujaa visa za nchi mbali mbali! Unabakia kusema Tanzania ina fursa, Tanzania ina fursa!

Jumapili Njema!
 
Huo ndio umanamba mamboleo, brainwashed, Sio vibaya kuishi Marekani kama mkimbizi lakini ni vizuri zaidi kuishi kwenye taifa lako mkitafuta majibu ya matatizo ya jamii yenu. Yaani wewe unatamani usikie Elon Musk ameinunua Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Naona wewe umetafuta solution ya Matatizo ya Tanzania, kwa kuongeza safari za Marekani! Maybe ndio ulio design vitambulisho ya Wamachinga! Na labda uko behind Tozo!

Huko ndiko kutafuta solution za matatizo ya Tanzania! Unaniambia eti natamani Elon Musk ainunue Tanzania! Mbona attempts nyingi za kuiza nchi zinafanyika hapo hapo na hao mliowakabidhi nchi! Hawana Greencard! bali wana Green shirts! Na proposals za kuuza nchi mnazipitisha huko huko Ma wizarani!

Vilio vya kusema nchi ineuzwa huwa vinatoka wapi? Hapo hapo bongo!

Your perception of reality is completely obscured!
 
Kamongo,

Inashangaza sana, nadhani kuna wakati madaktari, manesi na hata engineers walioko kwa wingi kwenda Botwasana, It was exodus ya aina yake, lakini hakukua na kelele za umanamba, utumwa!

Huwa naogopa ni wivu au chuki binafsi na Marekani? Na hata kama unaichukia Marekani, kwa nini unichukie na mimi niliyekuja kutafuta maisha Marekani.

Waarabu in general wanaonekana wana chuki na Marekani ukiangalia kwenye Media, lakini ukweli unasema tofauti! Nadhani kwa miaka mingi wao ndio wanaongoza kuleta watoto kusoma na kuwekeza!

Kuni kipindi fulani nikiwa Tanzania tulitembelewa na auditor mmoja mwenye asili ya kiarabu toka Sudan lakini ni Mmarekani, na alikuwa mtu wa dini hasa, mimi ndiye niliye kuwa mwenyeji wake Tanzania, kumuonyesha wapi akitaka kusali Ijumaa nk! (Mimi sio mwislamu) Katika ushauri alionipa, kabla hajarudi US, yaani jinsi kufanikiwa katika shirika letu na mambo ya kawaida tu ya maisha, alitoa Passport ya Kimarekani mfukoni mwake, na kuniambia " Ukijaribu kupata hii" akionyesha Passport ya Kimarekani Itakusaidia sana mambo yako!

Aliniambia uwazi, yeye akiwa Mwarabu na Muislamu hapendi baadhi ya Mambo ya Marekani, lakini kuwa Mwamerika imemsadia sana yeye na familia yake! Nilipokuja Marekani nilimtafuta Atlanta na kusema, Asante!

Waswahili walisema Baniani mbaya kiatu chake dawa!
Tabia za kukatishana tamaa watz wengi wanazo,hizo tabia hata watz walio nje wanazo ukitaka kijiendeleza kielimu wankukstisha tamaa.
Watz wana roho mbaya kama watusi tu
 
Tabia za kukatishana tamaa watz wengi wanazo,hizo tabia hata watz walio nje wanazo ukitaka kijiendeleza kielimu wankukstisha tamaa.
Watz wana roho mbaya kama watusi tu
Mkuu, wengine hatujaitwa kuwa wana siasa au matajiri kama Bhakheresa maskini waje tuwape chochote, lakini katika safari hii fupi ya maisha unaweza kumsaidia mwenzio kilicho katika uwezo wako, wengi tuna experience fulani, basi share na wenzio! wakifanikiwa zaidi yako inakuuma nini! Hushindani na mtu, tunapishana pishana tu ulimwenguni kisha tunaondoka!
Nimefika hapa nilipo, nikiondoa wazazi wangu kuna mikono ya wengi! Na hata wengine waliisha ondoka duniani sijui jinsi ya kuwalipa! Walinipa mawazo, moral support nk! Niliwahi kukwama Bangkok, Thailand ( Nili over spend) Nikaishwia kabisa! Na ATM Card yangu iligoma, Aliyenikwamua ni Mkenya nisiyemjua! Alinipa pesa nikaondoka haraka! Sijui hata nitampata wapi kutoa shukrani! Hakujibu contacts alizonipa.

Na kwenye hii post najaribu tu kutoa chochote au hata kuwapa watu matumaini kuwa kuna njia mbadala kama options za nyumbani zimefungwa, ni hilo tu. Sasa huo ndio unaitwa Usaliti na kukosa uzalendo!
 
Nakubaliana na wewe ila watz tuna chuki mtu roho inamuuma kisa fulani anaishi USA,
 
Wewe goal yako kuu ni kupambana kwa hali na Mali hata kwa kuu tako lako moja ili kupata financial freedom. Sisi wenzio tunapqmbania kupata total freedom yetu, jamii na taifa lote kwa do or die tukiwa humuhumu. Hata hako kaahueni wanakokapata weusi pale Marekani ilikuwa ni kazi ngumu ya akina Martin Luther king na wenzake, kalipatika kwa jasho na ujasili sio kwa kuwaza kiboyaboya kama wanavyowaza watafuta greencard ili kukimbia matatizo kwao, huo ni uboya uliokithili kiwango. Huwezi kukimbia tatizo labda uwe umebemendwa akili. Mungu hakuwa mjinga kutuweka sisi Tanzania.

Do not uproot the pumpkin at your home state (Chinua Chebe)
Naona una mawazo ya ajabu sana! Hujui hapo bongo kuna wanaoshikishwa ukuta! Na unajua kabisa maana umeelimika, huo ushoga ni tabia tu, nothing to do with poverty! Naona wewe hujui mambo mengi na kijana wa leo uliyetoka vijijini ukaja Dar! kuna baadhi ya wenye tabia hizo Tanzania walikuwa wenye nafasi kubwa serikalini na watoto wa matajiri! Siwezi kutaja majina yao, wanafahamika!

Na hata huku walio katika ugonjwa huu ( mtazamo wangu) ni watu highly educated and financially well off!

Halafu naona una ugonjwa wa kusahau! Huyu sio Chinua Achebe aliyeandika usemi huu " Do not uproot pumpkin in the old homestead" Ni Okot P Bitek - Song of Lawino

Weekend Njema
 
Mkuu tofauti na Green card njia gani nyingine salama na ya uhakika naweza kutumia kufika hiyo nchi ya ahadi?

Green card nimeapply, nasubiri tokeo japo hiyo siwezi kuitegemea sababu ni bahati nasibu
Kaka hiyo sio bahati na sibu bali ni vigezo kama vitatimia. Wakati ulee wa utumwa vigezo vilikuwa uwe kiji pandikizi la Mirada 4, yaani jitu refu kama Hashem Thabiti na lenye nguvu kama Schwarzenegger na R Kelly kwakuwa kazi zilikuwa ni mashambani, viwandani na bandarini, Lakini Sasa hivi vigezo ni elimu (masters, PhD) kwenye maeneo wenye uhaba nayo wa watumishi, lottery inabakia kwa watu wasiokuwa na elimu ya juu kwa blue collar kama za mashambani
 
Kavulata: Unajua unachokisema au umekaririshwa? Niko Marekani, sikuja kwa kufungwa mnyororo,na hata nikitaka kuondoka hakuna kamba iliyonifunga.
Ushauri kila siku kwa vijana wa kitanzania, kama unaona opportunities zimebana Tanzania jaribu popote, nina mifano mingi mno, na nimeona kwa watu toka mataifa mbali mbali niliokutana nao US!
Ukiwa na focus, na documents halali na yote unayoyasikia kuhusu Marekani, ni mahali unaweza kufikisha ndoto zako, sisemi ni rahisi, lakini kuna nyenzo ambazo hupati katika nchi nyingi za Kiafrica.
Sijahonga au kumuona yoyote watoto wangu kupata mikopo ya vyuo vyao, sikuwa na connection zozote zile watoto wangu kupata white color jobs! In short mtoto wangu alikuwa recruited akiwa bado chuoni, na leo akiwa na miaka24 is making almost $ 85,000/ Wenzake aliowaacha bongo waliomaliza chuo wanasaka ajira!
Sasa sijui ni utumwa wa aina gani huo!
Ni kweli Marekani/ Canada zinataka nguvu kazi, lakini ukiingia huku ni juhudi zako na akili yako! Wengine wataenda juu, na wengine chini, sawasawa na wazawa! Anayenifyekea majani nyumbani kwangu ni mzungu! Maana sina muda! Na kila baada ya wiki mbili au tatu ananipigia simu kama yameota aje kufyeka! Na ameniambia ni fundi katika serikali yetu ya mtaa anatafuta pesa ya ziada! Hii ndio Marekani, simdharau najua anachotafuta!
Hivyo usikaririshwe na akina Lumumba.
Hulazimishwi ni akili yako tu! Wengine wanatumia hapo bongo wanatoka! Wengine mambo yanakataa! Maisha popote pale!
Watu wa kanda ya kaskazini ndio wako after financial freedom zaidi kuliko hata usalama wao, ndugu, jamaa na hata taifa. Nonsense
 
Back
Top Bottom