Daah! umenena, nini nafahamu kuwa furahi ya mtu haitokani na kuwa na pesa nyingi tu bali mjumuiko wa mambo mengi na hela ikiwemo. Nimekutana na kijana ambae huko majuu ambae analala kwenye gari yake maisha, nilipomuuliza kwanini kwanini huna chumba chako aliniambia ninafanya kazi shift 3 kwa siku hivyo muda wa kulala sina, hata hiyo nyumba naona nitapoteza pesa zangu bure wakati silali humo. Akanambia ana madeni mengi yanayohitaji ku service (kulipa) hivyo lazima afanye kazi zaidi ya 1 ili apate ziada. kaka kijana huyu hajawahi kula chakula cha nyumbani kwake zaidi ya kule fast foods mitaani, makato mengi na anashindwa kutuma pesa nyumbani maana wafyeka hela nyingi sana. kaka kuna mitaa/maduka/malls ukiingia mwenye ngozi nyeusi wanadhani huna pesa ya kuingia hapo bali unataka kuiba, ubaguzi bado haujakwisha tunalazimisha tu.
Nguvu, muda, juhudi, maarifa na akili mnazozitumia kumudu kuishi huko hata zingewekezwa japo nusu tu kwenye jangwa zingetoa matunda. Vijana wetu huku ni wavivu sana ni wavivu sana na ni wavivu sana ndio maana wanapata tamaa ya green card wakidhani huko US pesa ziko kwenye viroba tu ni za kuzoa na kutumia.
Kama asili na chanzo kikuu cha ushoga huko ni maisha magumu, watu wanaunganisha nguvu ili kumudu maisha bila kulazimika kuwa na watoto wa kutunza, yaani kuona mwanamke ni kuongeza ugumu kwenye ugumu. bahati mbaya mimi nimeishi huko sana tena vijijini kabisa ambako maisha ni kama haya hapa ya tandika na kwamtogole, kuchafu na idadi kubwa ya ombaomba wazungu mitaani ambao wanapatiwa nguo kule salvation army na kwingineko kwenye malls kama vile Walmart zenye madirisha ya watu maskini (wazungu) kupatiwa misaada.
kaka usiwadanganye watu ukawapa hope na kuja kuishia kuolewa na wanaume wenzao, wanaofanikiwa ni watu kidogo sana kati ya hao wahamianji. Wengi wao wanaishia kwenye vyombo vya usalama kufungwa na hata kuuliwa.