Green card lottery ni Umanamba mamboleo

haha haha haha hahaaaa!!! yuhyu dada mwenyewe anaonyesha rangi ya mkono wake wakati wa maongezi na yule mwanamke mzungu waliokuwa wakishangaa pamoja kitendo kile, angalia tena hiyo picha, "wamarekani wenzako" wasingeituma hiyo picha kama isingekuwa na tatizo. Manamba hajui kama ananyonywa bali anaangalia shida zake nyumbani zilizomsukuma kufanya kazi za kimanamba. Yaani analinganisha kazi na shida.
 
Unaweza ukamuita manamba, lakini shida zake hakuletei wewe, ulitaka aje mkae naye ili iweje? Kuna mtu hawezi kuishi Mwenge au popote zaidi ya Temeke. Kila mtu akae panapomfaa, huyo akirudi huko, bado mtambagua tu, ajira zinayaka connections au uwe na card ya Chama fulani, akiingia kwenye siasa akawa upande wa upinzani bado mtamuibia kura au mtamteka au kumuua. Au unadhani huko mpo salama? Au kwa kuwa wewe hayakukuti?
Wakina Tundu Lissu walipigwa risasi Marekani na Ulaya? Roma, Ney wa na wengineo, hao wote walitekwa Marekani?
Angalia wasanii walivyo kama watumwa, wote hawana maamuzi binafsi, wanalazimika kisiasa kushabikia Chama fulani sanabu bila hivyo wajiandae kutengwabau kufilisiwa.
Bado mnajiona mpo sawa, only mwenye matatizo ya akili ndiye atadhani mpo sawa.
 
Inabidi kupajua nyumbani kwa kila mtu aliekua nje ndo uwashauri warudi
 
kuna ilivyo na inavyotakiwa iwe. Kuna wakati traffics barabarani wanahangaika na kugombana na madereva na abiria ambao hawakufunga mikanda. Utajiuliza kwanini dereva hakufunga mkanda ambao uko kwaajili ya usalama wake mwenyewe? Kuna wakati najikuta nahangaika na watu wanaotumikishwa na mataifa mengine kwa kigezo cha tofauti umaskini na utajiri wa mataifa yao (manamba). Vijana hawa wananyonywa kunyonywa na kunyonjwa na mabepari kwa kuuza nguvu na ujuzi wao (labor). Nguvu na ujuzi ambao hata familia zao, ndugu, jamaa na mataifa yao wanazihitaji. yaani wanatengeza vicious cycle ya utajiri na umaskini kati ya mabepari na mataifa yao.

Mimi niko kama traffic kuhangaika na madereva wasiokuwa na vifaa vya kuzimia moto kwenye magari yao.
 
Mwaka Jana Kenya diaspora walichangia almost 4.5b USD kwenye uchumi wa nchi. Hiyo ni % ngapi ya total budget ya Tz?

Meanwhile kuna watu humu wameshiba uji wa chumvi wako busy kukwambia kwamba kuishi nje ni unamba! Bottomline, masikini tuna roho mbaya sana. Sijui kwa nini.

Poverty is a disease 🦠
 
Nafikiri wewe ulienda huko kwa kuzamia. Elimu yako ilikuwa duni na uwezo wa kwenda (kiakili) shule hukuwa nao. USA ukiomba kazi wanataka high school diploma na wewe huenda ni darasa la saba. Watanzania wengi walioenda USA na elimu zao wana nafasi nzuri. Waliyo na bidii wanafanya kazi viwandani ingawaje kazi za nguvu lakini wanaanzia $15 (Tsh 42,000) kwa saa. Kama wewe ulikuwa vijijini basi huenda ni darasa la aba na kazi pekee ungeweza kupata ni ya kuvuna mazao mashambani, na mtu kama huyo hata kujaza green card lottery haruhusiwi/ha"qualify". Minimum qualification ni form six au forn four with two-year work experience.
 
Hiyo haikuondolei jina lako la cheap labor kwao. Yaaani kazi hiyohiyo unayofaanyia ina malipo tofauti kwa watu wa rangi na asili tofauti. Africans are the lowest in payment rates. Mimi saloon nanyoa kwa sh.2000 huku, je huko unalipa ngapi?

Wanaolipa sana na wanazichukua Tena kwanjia ya Kodi na mapato na high prices. Najua wewe unavizia clearance paleee kwenye kona ya Mall,
 
Kaka wao tayari wako huko, haina neno wacha watafute liziki maana hawakujuwa kuwa kuna mateso yake. Uzi huu ni kwaajili ya wale wanaotamani kwenda kuhaso kule wakifikiri kila kitu ni tambarare, Hapana, angalia hiki


View: https://youtube.com/shorts/1u_MG5vFrbc?si=ZXPYiGcOLDQa3KUM
 
Kwani shida nini? Kukamatwa ni mateso? Mbona bongo kutekwa na kuuawa na wanausalama ni jambo la kawaida mno?
Sasa hiyo clip haionyeshi chanzo wala nini. Inaonyesha mtu anatakiwa kuwa arrested na yeye ana resist, lakini wakamkamata na watu wanachikua video bila kubughudhiwa au na huyo walienda kumuua?
 
Wakenya ni wakimbizi ndani na nje ya nchi yao hata baaa ya uhuru, sio mfano sahihi.
 
Omba Mungu Kamala ashinde, la sivyo tutaona mengi.
 
Nilikuwa nagombaniwa nibaki, na social security number yao ninayo. Lakini kwani nataka nini hasa? Madeni kila sehemu kwa kila kitu?
 
Mi nilidhani kazi za majumbani kumbe za kitaaluma, basi mshauri Ndugulile kapata kazi WHO
Mimi nilidhani kazi za majumbani kumbe za kitaaluma, basi mshauri Dk. Faustine Ndugulile Mkurugenzi kikanda wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO). asitishe ajira yake abaki na aendelee na kuitumikia nchi kama Mbunge kabla hajajiuzulu, maana sharti aache kazi nchini ili akaitumikie nafasi yake hiyo.
 
American life is harder, Tanzania life is harder too, so choose your hard but I will do whatever it takes to get better life this is my slogan. Umaskini ni mbaya sana halafu masikini Hana kiapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…