cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
Hivi wewe una critical thinking! Ama kweli! Critical thinking mngeishia kukimbiza Mwenge! Critical thinking ingekufanya kukosa umeme, maji ya mgao kuona sawa tu!Hoja yenu ni kuwa Tanzania hakufai kuishi, hakuna social services nzuri kama huko hivyo unapiga debe vijana waichukie hadi kuikimbia nchi yao waje huko kufanyakazi za umanamba.
Kaka mimi nakumbuka hata tz manamba kwenye mashamba ya mkonge, mpira, ngano, chai, kahawa, ranch za mifugo walikuwa wanalipwa hela za kuwawezesha kuishi, kulipa kodi ya mkoloni bila shida na hata kusomesha watoto wao hadi ngazi ya middle schools shida sana. Japo walikuwa wanapunjwa lakini manamba walikuwa na nafuu kiuchumi kuliko wale ambao hawakufanya kazi za umanamba. Ambao walikuwa hawafanyi kazi za umanamba walikuwa wanalala porini kujificha kukamatwa kwa kushindwa kulipa mkodi.
Kwahiyo unachosema wewe ndio tabia na sababu halisi ya umanamba. Unaweza sasa kujengea wazazi, kulipia ada za wadogo zako, nk kwa kufanyakazi za watu wengi, kulipa kodi kwa nchi nyingine, kukuza uchumi wa nchi nyingine halafu wewe unaambulia kulipwa posho inayokatwa kodi kubwa, kodi ambayo anaenda kuzikopesha nchi nyingine ikiwemo tz kwa riba kubwa na kugharamia vita vya dhuluma kwa nchi changa, nk. Shida yetu kwenye mitaala yetu hakuna somo la Critical thinking kwa watoto wetu.
In short you thinking is in Primitive mode! Na wewe unawakilisha Watanzania wengi! Hamuoni mbele mnabakia mabeberu! Mabeberu! Mabeberu! Inasikitisha!