Green card lottery ni Umanamba mamboleo

Hivi wewe una critical thinking! Ama kweli! Critical thinking mngeishia kukimbiza Mwenge! Critical thinking ingekufanya kukosa umeme, maji ya mgao kuona sawa tu!
In short you thinking is in Primitive mode! Na wewe unawakilisha Watanzania wengi! Hamuoni mbele mnabakia mabeberu! Mabeberu! Mabeberu! Inasikitisha!
 
Urusi kakimbia Kharkiv,Kherson
Maana alichukua mkoa 1 tu wa Kherson na kakimbia
 
Kila watakapoona nchi mnapoipeleka watanishukuru milele! Miaka 60 ya uhuru mnachombiwa vyoo vya shimo! Watu ambao mnajiona na Critical thinking mnakwenda kuzindua!
In short mpaka Sasa wananishukuru, maana wameanza kuwatumia pesa wenzao ambao bado hawana kazi lichacya kumaliza chuo kuu!
Just this week my son provided $ 1000/ kwa mtu aliyekwama kabisa huko bongo! Ameahidi kurudisha, tunajua hawezi.
Mpaka they respect me a lot kwa kuwaleta US, singoji kufa wanienzi!
 
Nadhani mtoa maada dhumuni lake la namna mchakato wa Green card lottery umegubikwa na utumwa. kama una nia ya dhati ya kuishi usa kwanini usubiri bahati nasibu? utumwa tu
 
Mnasafari ya kupambana kubwa! Umeme umekuja kwa kupambana! Miaka 60 toka kupata uhuru! Critical thinker anaandika kwa ujasiri badala ya aibu! Mtambana na maji! Mtapambana ukosefu wa vyoo mashuleni! Mtapambana na opposition parties! Iko kazi
 
Mkuu tuna safari ndefu! Katika karne hii bado kuna upofu mkubwa namna hii wa kufikiri! Hebu niambie jamaa kama huyu awe wizarani na anatengeneza curriculum ya taifa!
Watu kama huyu mleta maada usiombe awe bank halafu una tatizo lako technical na yeye ndio anatakiwa kukupa huduma. Unaweza kulia.

The only reason ilinifanya nikaacha kutumia local banks ni kwa sababu ya uwepo wa wafanya kazi ambao wana akili kama za mtoa maada.
 
Kama ulifeli kutake chances zako usilalamikie watu kuwa maisha ni magumu.
 
Wewe ni mjinga sana.
 
Mnasafari ya kupambana kubwa! Umeme umekuja kwa kupambana! Miaka 60 toka kupata uhuru! Critical thinker anaandika kwa ujasiri badala ya aibu! Mtambana na maji! Mtapambana ukosefu wa vyoo mashuleni! Mtapambana na opposition parties! Iko kazi
Kaka sababu ya msingi (basic cause) kwanini Tanzania hakuna umeme ni ukoloni mamboleo. Western countries, marekani na our former colonialists ndio sababu hasa ya mataifa ya afrika kuonekana kama yalivyo sasa. Afrika chini ya jangwa la sahara inafanana kiuchumi na kihuduma, na Afrika juu ya jangwa la sahara pia inafanana kwa maendeleo yao. Hii haiwezi kuwa ni coincidence tu, au useme viongozi wote wa afrika ni wajinga na wapumbavu kwa wakati mmoja muda wote na mara zote. Lazima wanakutana na a common factor inayozaliza matokeo yanayofanana. Kujua hili kunahitaji mtu mwenye akili nyingi na critical thinkers. Hawa wazungu huko uliko mzee ndio wanaopanga nani awe rais wetu na nani asiwe rais wetu Afrika, wanapanga bei za vitu vyetu na wanapanga bei za vitu vyao, wanaamua sisi tumiliki nini na wao wamiliki nini kwa bara lote. Wanafanya haya yote kwa kuzingatia maslahi yao wao.

Kiongozi mwenye akili, mjanja, jasiri, mpenda nchi yake, na mwenye maono kama mimi hawamtaki na hawataruhusu atawale, watamuondoa atake asitake kwa kutumia sababu na njia mbalimbali. Juzi juzi wakatuambia tusijenge bwawa la mwl Nyerere, tusijenge barabara kupitia hifadhi za wanyama, tusijenge bomba la mafuta, tusijenge hoteli kwenye mbuga, turuhusu ushoga laa sivyo....Lakini sisi hatuwashauri kwa lolote. Hivi wee jamaa uwezo wako wa kufikiria uko sawasawa?

Hii ni elimu ambayo mtu kama wewe hupendi kuisikia kwakuwa tayari umeshachagua upande.
 
Kwa sababu akili hauna ndio maana unaona mgao wa umeme siyo tatizo.
 
Nairudia hoja yako inatisha hasa kwa mtuu ayejiita critical thinker! Nakuuliza tu mwisho wa mapambano yako ni lini! Kila mwaka lazima utoe mchango wa Mwenge! Bado mapambano ya kupata pensheni yako uzeeni!
Bado watoto wako watakua hawana ajira! Anyway labda wewe ni kama wa Chama wanaweza kujishikiza Lumumba!
Mwenyezi Mungu angetupunguzia makali ya Jehanamu sisi Waafrika!
 
huwa mara zote nina compare na ku contrast kati ya green card na manamba, similarities ni nyingi kuliko differences, naama zote zilikuwa zinatafuta basically wafanyakazi wa bei rahisi, zote zilikuwa zinahusisha kuhama kutoka kwenye homeland yako, yaani Waha, wanyamwezi, wasukuma walihamishwa kutoka kwao kwenda kufanyakazi kwenye mashamba makubwa ya mkonge, wanyama na migodi, wote wanalipwa kwa kupunjwa, wote wanakuwa mbali na kwao, wote wanalipa kodi kulekule ugenini waliko, wote wakifa wanazikwa hukohuko unambani, wote wana maendeleo kuliko familia zao walikotoka. Lakini tofauti zao kubwa ni kwamba Manamba walikuwa wanapelekwa kwa nguvu lakini green card wanaenda wenyewe, green card wanatakiwa awe na elimu na ujuzi kwaajili ya kufanyakazi za wakati huu lakini Sifa kuu ya manamba ilikuwa kuwa na nguvu na umbo kubwa kwasababu ya kufanyakazi za wakati ule, na tofauti nyingine green card anaweza akaishi mtaani lakini manamba walikuwa wamejengewa kambi waishi hapohapo karibu na kazi husika.
 
umeme huko umekuja kwa mapambano ]makubwa kati ya wananchi na wanasiasa,. Hivi ni kweli unataka wajukuu na vitukuu vyako vije vikujue kama mtu aliyekimbia nchi yake kwasababu ya kukosa umeme na maji ya uhakika. Hakika watakukuona kama babu ambae hakuwa na maono, muoga, asiyeaminika, na asiyekuwa mzalendo na mwaminifu?

Kavulata: Watoto wangu wananiona ni super dad! genius dad! Kila mara wananiuliza niliwazaje kuwatoa Tanzania
Almost 75% ya wenzao hawana kazi, wanangu walichukua P3 zao na kutuma kwa mtu ambaye ni graduate ili awe anachezesha game kupata pesa!
Huwa wanashangaa kuna baadhi ya ndugu zao hawako Wassup, kisa hawana smart phone, na wakiwa na smart phone hawana bundle! Inakuwa ni kazi kuwaeleza!
Nimekwambia single kufa wanipongeze! Wanaona wenyewe nimewaepusha na maisha gani!
Pambana mkuu!
 
Mkuu najua bongo ni tough, nina ndugu Dar hadi vijijini, kila siku ni vilio, naangalia exchange rate ya $ kwa Tanzania shilling, inaniumiza sana, yaani nikimpa mtu dola 47,tayari ni laki.
Sasa kwangu hiyo ni kitu kidogo sana!
Nikiwatumia nakua kama mfalme!
Kinachoumiza ni huu upumbuvu wa Watanzania wenzetu,tunapotoa options za kujaribu nje wanaona ni umanamba! Na hawa wanadai wasomi! Critical thinker, unabakia unashangaa kama wanajua maumivu ya Watanzania.
Labda wako katikati ya jezi ya kijani, hawaoni maumivu ya Watanzania!
 
Unapotaka kubadili hali yako ya maisha, inabidi ufanye uamuzi mgumu, mojawapo ni ka kuondoka nchini kwako, jamaa zangu hawaoni hilo!
 
Kabisa mzee, kuna wana wanahustle kichizi mlo wanapata kwa tabu.
Watu wakifanya biashara za umachinga wanatimuliwa wengine wanapigwa na polisi na migambo mpaka wanapata ulemavu wa kudumu.

Mzee mbele ni mbele tu aisee, japo naskia kuna ubaguzi lakini ubaguzi hauui kama hawa polisi na migambo wetu.
 
Kwa sababu akili hauna ndio maana unaona mgao wa umeme siyo tatizo.
Mkuu jamaa hana laptop,kindle au tablet,au hana project yoyote akirudi nyumbani! Kaenda shule but he still a cave man! Primitive to the core! Na rafiki yangu ni Architect, yuko nyuma mno katika projects zake! Mara ofisini haupo mara nyumbani haupo!
Lakini anayejiita critical thinker haoni tabu kuwasha mshumaa!
Bado DNA ya mababu zake waliotumia kuni iko kwenye damu!
Unategemea mtu kama huyu atawavusha Watanzania katika karne hiii?Thubutu!
 
Mkuu nina miaka US, sijabaguliwa! Watu wanasahau kabisa sheria za US ni kali sana kuhusu ubaguzi wowote ule! Ukiwa na evidence mtu kakubagua kazini kwa dini, rangi, jinsia ni ngumu sana.
Na jamaa zangu Waarabu, saa za swala wanatoa Mike kama yao wanapiga swala zao hakuna anayewabughuzi!
Achana na media. Kama ubaguzi upo wangapi wangeondoka Marekani!
 
Sasa mbona jamaa anaktisha tamaa watu kwenda huko akidai huku ni bora kuliko huko!??

Wabongo tuna roho za wivu sana sijui kwanini asiee, kisa ye kafeli basi hataki mwingine ajaribu akiamini akifaulu basi yeye ataonekana hamnazo.
 
Sasa mbona jamaa anaktisha tamaa watu kwenda huko akidai huku ni bora kuliko huko!??

Wabongo tuna roho za wivu sana sijui kwanini asiee, kisa ye kafeli basi hataki mwingine ajaribu akiamini akifaulu basi yeye ataonekana hamnazo.
Kwa kifupi sijui lengo lake! Sijasema kila mtu lazima akitaka kufanikiwa aje US, nalosema ukiona options za nyumbani ngumu jaribu nje! Wanageria, Wakenya na watu nje ya Afrika wanafanya hivyo!
Jamaa hataki kabisa kusikia, na anakuja na very primitive arguments! Eti uzalendo! Uzalendo utasomesha watoto wako? Uzalendo utakupa mahitaji yako unayotafuta maishani?
Ukishindwa jambo unatafuta options nyingine,ndio nacho jaribu kusema hapa! Lakini naona nazungumza Kichina!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…