Greenland Yapendekeza Mazungumzo ya Moja kwa Moja na Marekani Bila Denmark

Greenland Yapendekeza Mazungumzo ya Moja kwa Moja na Marekani Bila Denmark

Fascinating

Senior Member
Joined
May 14, 2025
Posts
146
Reaction score
351
Hali ya kidiplomasia katika eneo la Arctic imezidi kupamba moto baada ya Greenland kupendekeza kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mustakabali wake. Hatua hii inakuja huku Washington ikiendelea kusisitiza nia yake ya kutaka kuidhibiti ardhi hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya ufalme wa Denmark.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Greenland, Vivian Motzfeldt, alidokeza hivi karibuni kuwa mazungumzo hayo yanaweza kufanyika bila ushiriki wa Denmark. Akizungumza na shirika la utangazaji la Denmark (DR), Motzfeldt alisema:

"Inapokuja suala la Greenland, inapaswa kuwa Greenland ndiyo inayoongoza na kuzungumza na Marekani... Kuna kosa gani ikiwa tutafanya mikutano na Marekani peke yetu?"

Kisheria na Uhuru wa Greenland suala hili limekaaje?

Ingawa Greenland ina mamlaka ya ndani na bunge lake, masuala ya sera za kigeni na ulinzi bado yanadhibitiwa na serikali ya Denmark. Motzfeldt alikiri kuwa kisheria, Greenland bado haina mamlaka ya kufanya maamuzi hayo pekee yake, akisema kuwa kuna sheria na taratibu za ufalme ambazo lazima zifuatwe hadi hapo watakapopata uhuru kamili.

Tishio vya Trump kufanya Uvamizi wa Kijeshi
Kauli hizi zinakuja wakati Rais wa Marekani, Donald Trump, akikariri nia yake ya kutaka kuidhibiti Greenland kwa sababu za kiusalama na utajiri wa madini. Ikulu ya Marekani imekwenda mbali zaidi na kusema kuwa "hatua za kijeshi ni chaguo lililopo mezani wakati wowote."

Hofu ya matumizi ya nguvu imeongezeka barani Ulaya, hususan baada ya Marekani kumkamata kijeshi kiongozi wa Venezuela, Nicolás Maduro, wiki iliyopita. Ingawa Denmark ni mwanachama wa NATO, Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen, ametahadharisha kuwa vitisho vya Trump vinapaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.

Msimamo wa Mataifa ya Ulaya
Mataifa kadhaa ya Ulaya, yakiongozwa na Poland, yamepinga vikali nia hiyo ya Marekani. Nchi hizo zimesisitiza kuwa mustakabali wa Greenland unaweza tu kuamuliwa na watu wa Greenland wenyewe na serikali ya Denmark, na si kwa shinikizo la nje.

Screenshot 2026-01-11 172729.jpg

Licha ya mvutano huo, Motzfeldt anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, wiki ijayo akiwa na mwenzake wa Denmark, Lars Løkke Rasmussen. Motzfeldt ameeleza kuwa matumaini yake makubwa ni kuona uhusiano kati ya nchi hizo unarejea katika hali ya kawaida.
 
Back
Top Bottom