BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 779
- 1,269
Wasalam
Nianze kwa kusema mjadala wa nani zaidi kati Lionel Messi na Ronaldo CR7 haujawahi kupata mshindi.
Pia sijawahi kuona upande gani ukiibuka washindi, pale walipopambanishwa kati ya Mourinho na Guardiola.
Pengine ninaweza kuonekana nimetoka nje ya topic, lakini ni ukweli usiopingika kwamba asingekuwepo mmoja kati ya CR7 na Messi au Mourinho na Guardiola basi kusingekuwa kabisa na mjadala juu ya uwezo wa hao magwiji wa soka, hususani katika kipindi cha hivi karibuni. Kwani always ambaye angekuwepo ndio angekuwa mfalme na kuwaacha wengine kwa mbali sana.
Turudi kwenye mada. Kwanza ninampongeza sana Guardiola alivyoamua kutoka nje ya Barcelona na kwenda kufundisha vilabu vingine na ligi nyingine (japo kwa Ujerumani bado hakujipima vizuri). Kwa kufanya hivyo alionesha kwamba haogopi changamoto tofauti.
Sote tunafahamu kwa sasa yupo Man City katika ligi shindani kuliko ligi zote ulimwenguni, na anafanya vizuri kwa sehemu yake.
Lakini sote tutakubaliana kwamba Guardiola hajafanya vizuri kiasi cha kutosha katika ligi shindani zaidi duniani, yaani EPL. Katika possible trophies 8 kwenye miaka hii miwili aliyokuwepo uingereza anaonekana atabeba vikombe 2 tu, vyote msimu huu. Wakati akiwa Barcelona katika possible trophies 19, alifanikiwa kubeba 14. Huu ndio uwezo halisi wa Guardiola.
Kwa upande wa Lionel Messi la Purga, maisha yake yote ya soka yameanza na yanaonekana yataishia Barcelona. Sina mashaka na uwezo wake, lakini nina mashaka na uwezo wake pale watu wanapoanza kumlinganisha na magwiji wengine kama akina CR7.
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda, tutazidi kujifunza kuhusiana na ubora wa hawa wawili. Lakini ninaamini, Messi na Guardiola ni bora, lakini si bora kama wanazi wao wanavyotaka kutuaminisha.
Kiukweli hawa jamaa nje Barcelona wameshindwa kuni prove wrong mtazamo wangu. Na mimi ninaona hawa jamaa wawili wamebebwa zaidi na Barcelona kuliko wao walivyocheza Barcelona.
Karibu kwa mjadala.