Guys kuweni makini na wake za watu.

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2016
Posts
2,584
Reaction score
1,885
Katika kutimiza majukumu kadha wa kadha nilipita wizara flani, sasa hapa nimekutana na officer wa hiyo ambae pia ni mshikaji wangu kitambo sana.

Huyu jamaa ni mate wangu wa chuo enzi zile tulikua tukimtania kwa kumuita sadam husein, jamaa ni mwenyeji wa mafia yani ni mtu wa dini saaana.

Sasa katika story nikawa namuuliza vipi kaka mbna kama hauko sawa kuna tatizo, au magu anakupumulishia mirija, tukacheka na nini ila bado ilikua wazi jamaa anasumbuliwa na kitu.

Sasa katika maongezi na udadisi juu ya wizara yao nikamgusia kuna mshikaji flani ambae hapo ni bosi..

Jamaa si akapasuka kua huyu jamaa anapiga mke wake yeye anajua ila wao hawajui kama anaelewa kinachoendelea na jamaa kakili anampenda mke wake hawezi kumuacha kwani amezaa nae ndicho kinachomuuma.

Nikamshauri kua si akae wazungumze na mke wake kau hapendi hayo mambo, heee jamaa kakataa katakata akawa anasema wa kuongea nae si mke wangu dawa ni huyo anaejidai kidume, yeye amepanga kumsafiria tu kwenda kwao mafia ili amuadabishe, nikabaki mdomo wazi.

Nikachoka zaidi aliposisitiza kua unafikiri namuua wala hata simuui kaka, wala kumnyong'onyesha ila namtia upofu kwani hayo macho ndio yanampa kiburi sasa tuone, kama atafanya kazi, au ataitajika tena hapo wizarani.

Nikabaki duuh kaka dhambi unafanya, akawa ananiambia sasa unapochokoza vita ya mawe na nyumba yako ya vioo unatakaje.

Nikabaki kumuonea huruma tuu jamaa kua si muda mrefu upofu unamuingia.

Nb: kama upo humu kaka jipange au peperusha bendera nyeupe jamaa,nimeileta humu makusudi maana upofu usawa huu duuh.
 
Mshauri huyo mtu wa Mafia,atumie busara alizopewa na mwenyezi Mungu.

Kama ni ukipofu anapaswa kumpa mke wake ambaye hajitambui.

Anahangaika na huyo mmoja anayemjua,kama wapo wengine asiowafahamu je.???

Na vipi akianzisha mahusiano na wanaume wengine,nao ataenda kuwapofoa macho...???
 
Aaaah jamaa kiburi, si unajua wale itakad kalii hawataki ushenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…