Guys tunachohitaji toka kwenu ni kidogo sana....................

hahahaha Bigirita acha visa wewe...yaani umenichekesha mpaka H/G anashitukia hali yako ..
lakini pia nayo ni nzuri kuna watu wanajua kuchonga mdomo kama mpiga filimbi wa Amelini
Ndo hivyo tena FL1, mi nachuna tu! naongea inapobidi...
 

Mwanaume pia huchangia kuibomoa ndoa yake sio kila jambo mwanamke ndio anaanzisha kuna wanaume wengine wamezidi gubu,kuna wengine wanataka wasikilizwe wao tu,kuna wengine kuomba samahani kwao ni kitendawili.....ndoa au mahusiano hayajngwi na mtu mmoja bali pande zote mbili zikishilikiana
 


Kama usemavyo Klorokwin dawa ya maralia sisi pia wanaume tunashindwa hasa kuwaelewa na kuwaweka kundi gani ndo hapo tatizo linapoanzia
 
Sina utaalamu sana katika masuala haya lakini nafikiri jambo la msingi ni kuwa na upendo wa kweli na mtu. Hayo mengine yatajipa. Ukimfuata mtu kwa mambo yasiyo ya msingi au ukilazimisha mapenzi basi kuna hatari ya kukutana na rabsha nyingi zitakazokuweka roho juujuu siku zote. Ndio maana kuna kauli za utani kama: mwenzio akizoea kukukera kwamba umezidi uzito/unene, usibishe; mpunguze yeye ubakie mwepesi! It's complicated.
 

hapa umejiongelea wewe, haujawaongelea wanawake wote, kwasababu si wote wako kama wewe, na si wote wameolewa kwa mwanaume kama wako, hivyo experience ya mtu mmoja haiwezi kuwa shared na watu wote kwa kundi lile. Kuna wakati wa maneno matamu ya nyama ya ulimi kama unavyosema, na kuna wakati wa pilipili endapo itasaidia....kila jambo na wakati wake. mnajijua ninyi ni viumbe dhaifu, hilo halina ubishi, wakati mwingine tunatakia kuwalisha pilipili kama nyama ya ulimi haisaidii..kwasababu kama tukiishia kutoa nyama ya ulimi tuuu kwa nia ya kuwafurahisha ninyi tuuu, hatuishi hapa duniani kwa sababu ya kumfurahisha mwanamke tu kwa kila kitu....ukimsikiliza sana mwanamke kwa kila kitu, utaishia kuwa na mawazo ya kike na mapotofu ya kabisa ya saloon kwao. FIRST LADY ongelea lingine, hili nafikiri unatakia ukaongee na wanawake wenzio lakini si wanaume kama sisi. sorry!
 

Kumbe !
 

LOVELY POST MADAM, i wish na nyie mngekua hivyo... yaani sie ndio kabisaaa, tusingefika huko tulipo

mapenzi ni mzani mamaa
 

Kumbe wewe ni baba?? siku zote najua wewe ni mama sorry lakini:A S confused:
 
Nakupa Tano Klorokwin!!!

Kifupi Wanawake hawaeleweki, mpe yote, mfanyie yote atakugeuza mpumbavu! Tumesikia mara ngapi mwanamke anasema nimemuweka mume wangu kiganjani, hafurukuti? Kumbe jamaa ni respect tuu inamtuma kuwa mpole.

Zaidi ya hapo ni respect kwenu
 
ukiwa na maneno ya nyama ya ulimi muda wote wakati mwingine hata uyo mkeo anaweza kukuona zoba fulani hivi, hataona kama wewe jabali lake, mlinzi wake mtu unayeweza kumtetea hata akiwaanashambuliwa na wengine, atakushusha hadhi...ndo maana nilisema kuna wakati wa maneno ya nyama ya ulimi na wakati wa pilipili..na wakati mwingine wake zetu huwa wanakuja kutushukuru baadaye kuwa "kwakweli baba, pale bora ulitumia pilipili", manake anakuja kuona faida yake badaye kwa kile ulichofanya. it all depends you know!
 


Nakupa tano mkuu, mwanamke mpe yote, mfanyie yote but still atakufanya pumbavu!!

Kwani ni mara ngapi tumesikia wanawake wanajisifu kuweka waume zao viganjani hawafurukuti wala hawakohoi kisa tu unakuta labda wanaume ni jamaa wapo fresh.

Kiukweli ladies hawaeleki kabisaaaa!!!
 

Sorry, wanaume kama nyie na nani? Unawaongelea wanaume wote au nyie wepi?!!
 

Nimekubali 1st Lady! Inabidi tuanzishe semina ya ndoa.
 
Niliwahi kuwaelewa wanaume zamani sana na niliwaelewa kidogo ...lakini sasa hata hiyo Nyama ya ulimi sijui maneno matamu kwangu marufuku:sick:
 
Utadhani unachoongea ni kweli. Mungu aepushe mbali tu. Hiyo nyama ya ulimi huja baada ya kuwa nacho. Na hiyo nyama ya ulimi ni pumbazo la muda kwani tunajua wanawake wana matamanio yao yakisukumwa na hisia na mkumbo. Yaelekea nadharia ina nafasi sana akilini
 

kumbe mfalme unadhani nimelala nikaota:A S 114::bounce:
 
FL1 huna sababu ya kunyanyua jembe kwenda kulima
Elimu unayotoa hapa asilimia mia imesimama
Wanaume ubabe kutembeza kila siku kulalama
Nyama ya ulimi tamu lakini akili kumkichwa
Ndoa hailindwi na shoka FL1 anatuasa

Nyama ya ulimi pasipo mfuko kutuna Kingi anabisha
Maisha yamebadilika nyama ya ulimi miaka ya arobaini
Leo kiama kimewasili ndoa kama kampuni inaendeshwa
Jaribu yako bahati nasibu yako kuendesha
Tamati nafikia Mungu atangulizwe nyama ya ulimi inyumbulishwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…