angalia encounters zote za Yesu kama aliwaonya kwa upole. of course wale aliowaonya kwa upole ni wale raia wa kawaida, ila hao viongozi matapeli wanaopoteza muda wa raia raia wanaamini wanamwabudu Mungu kumbe wanaelekezwa kuzimu, ni wa kuwakemea kwa namna yeyote ile, na Mungu atatusaidia.
Mtu yeyote mkali huwa sio mtu wa upendo
Mungu aliupenda ulimwengu wenye dhambi akamtuma Mwanawe wa pekee afe kwa ajili ya ulimwengu hakuja kwa ajili ya wenye haki watakatifu alisukumwa na upendo sio ukali Yohana 3:16
Ukiona mhubiri yeyote mkali huwa sio mtu wa maombi yaliyojaa upendo akiwa na upendo wa ndani kabisa wa kuomba waliopotoka wabadilike .
Hata kwenye maombi hufoka foka tu akilaani waovu wawe ndani ya kanisa au nje
Cha kwanza mtu akipotoka ni kuingia kwenye maombi kwanza yaliyojaa upendo kama ya Musa alivyomsihi Mungu kuwa usiwaangamize wana wa Israel
Mhubiri yeyote mkali wa kufoka foka roho ya upendo wa Kimungu ule wa Agape huwa hana
lililo kuu kwenye mambo yote iwe huduma tano au karama zinatakiwa kutawaliwa na roho ya upendo wa ndani kabisa wa kutaka watu kubadilika na sehemu ya kuanzia sio kwenye mahubiri ni magotini kuongea wawili na Mungu kama Musa aliongea na Mungu kwanza maombi yaliyojaa upendo sio hasira .Mtu wa kuombea wengine kwa maombi ya upendo huwa hana Hasira madhabahuni akihubiri nj
Roho ya upendo ndani yako haimo.Muombe Mungu akusaidie hilo .
Kufoka foka ni ufarisayo mhubiri mfokaji fokaji huwa ana messianic syndrome kama kuwa yeye tu ndiye mwenye haki na Messiah pekee aliyebaki kwavajili ya kanisa nk hakuna Mwingine kwenye kanisa Hiyo sio nzuri kabisa ni hatari kwako binafsi na kwa kanisa na umoja wa Kanisa na mwili wa Kristo
Hili tatizo liliwakuta hata manabii akiwemo Eliya akamwambia Mungu nimebaki mimi tu mwenye haki nataka kuuawa
Mungu alivyomuona ana kiburi akamwambia ninao 750 ambao hawawezi piga goti kwa mabaali .Mmojawapo alikuwa Obadia ambaye alimpa taarifa ya manabii kibao waliofichwa mapangoni huko.Mungu akamwambia sikukumbelezi nenda kakabidhi kazi kwa Elisha wewe ondoka
Mitume pia walikuwa na hiyo jeuri ya messianic syndrome kuwa wao tu ndio wameitwa na wanajua kuliko yeyote siku hiyo wakamkuta mtu anatoa pepo na hajawahi kuwa mmoja wa wanafunzi wa Yesu chuo chao cha Biblia au kadini kao wakamzuia Yesu akasema acheni namjua
Ninataka kusema mwenye kazi ni Mungu wewe una Messianic syndrome acha .Kila kitu sukumwa na upendo zaidi kufoka foka acha na kujiona wewe ndio masihi pekee unaejua kila kitu acha.Mwili wa Kristo una viungo vingi na kila moja tumepewa tu kujua kwa sehemu kwa kadri ya neema ya Mungu aliyotujalia kasehemu kadogo na tukafanye kwa unyenyekevu sio kwa kufoka foka na kiburi cha uzima
Siku ukijua yote ya Mungu utakuwa Mungu na Mungu hakubali hata siku moja kuwa sawa na Mwanadamu Ndiko unakoelekea wewe
Acha ukali na kufoka foka jikite zaidi kwenye upendo iwe kwenye maombi,au mahubiri nk uwe mnyeyekevu na mpole uliyejaa upendo kwa uombayo na uwaombeao usiombe kama yule farisayo kuwa ohh Mungu unanijua niko vizuri kuliko watumishi wengine wawe wachungaji au masskofu ,kanisa zima nk
Shuka chini shuka nakemea Roho ya kujikweza iliyoko ndani yako na ya messianic syndrome ikutoke kwa Jina Yesu