Uchaguzi 2020 Gwajima, dharau hizi hutafika popote

Acha uchochezi we jamaa kwasababu gwajima yeye ndo alisema kusiundwe magroup ya ukabila kwa kushirikiana na police.
Kuhusu mahakama ya kadhi, alikuwa sahihi kwaajili ya kuavoid udini kwasababu hi nchi haiongozwi kwa misingi ya kidini na itambulike gwajima hakuwa kiongozi wa serikali na sio yeye aliamuaisiwepo kwenye mamlaka waliangalia madhara yatakayotokea ndo maana ikazuiliwa
Kuhusu bibi kidude,katika uzinduzi alialifafanua kuwa kumuita bi kidude haikuwa tusi kwasababu bibi kidude ni mwanamziki mkongwe aliyeheshimika
Gwajima ni kiongozi pekee anayesimama kuwatetea wengine.
 
Nadhani unaposema Gwajima ni moja ya watu bora nchi hii na wewe unaghafilika.
Atakuaje bora na wakati huo huo Ni mkabila, mdini na mwenye dharau?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
Wewe ndo unadharua na hauna Adabu na unakuta unamuongelea Gwajima lakin hata haujawahi kukutana naye live sisi ndo tunayemfahamu hana hvyo vitu unavyosema coz Gwajima ameishi maisha magumu kabla hajafanikiwa n mjinga tu asiyemulewa Gwajima n kiongozi bora mwenye upendo na kila mtu Gwajima hana ubaguzi kabsa kama unavyomzania wewe hzo chuki zako binafsi hazitasaidia kitu
 
Wewe ni mpumbavu na hukunielewa. Mimi nilikuwa namjibu huyo aliyesema Gwajima ni bora lakini Ni mkabila, mdini na ana dharau.
Nimemwambia kama anayo hayo mapungufu basi yanaondoa sifa ya ubora.
Tena wewe unaweza kuwa msukule wake ndo maana hata jina unalotumia linathibitisha hivyo

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
 
Gwaji hafai kwa lolote , anafanya jina la Mungu litukanwe! Tupa kule Gwaji boy!!!!!

watu wa Kawe hatutompa kura, labda angeenda kwao Kolomije ambako hawajitambui, sio hapa town.


JESUS IS LORD!
We ndo hufai kwa lolote kile kura anapata na anashinda kwa kishindo chuki zenu mnaleta JF kwel nyie n wajinga wa mwisho
 
Kila unachoongea lazima uwe na uhakika na kumbuka mambo anayoyafanya gwajima sio ya kitoto anafanya mambo ambayo wananchi wanapenda

ukiachana na halima mdee mambo aliyoyafanya na hata sasa watu hawamtaki wanakawe wengi sana wamemchoka kwa mambo yake

gwajima ni mtu muungwana ambaye anafanya mambo kwa kujielewa saaana na watu wanamkubali
 
We kwel ndo maiti unahitaj kufufuka kwanza
 
Kuna hoja zingine inalazimika kuzijibu kwa faida ya watu wachache ambao wanaweza kuchotwa na upuuzi wa namna hii ambao unalenga kumfanya Askofu Gwajima ambaye kimsingi ni mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Kawe aonekane ni mtu hatarishi.
 
Gwajima ni kiongozi wa dini anayejishughulisha na maisha ya watu kuamua kuchukua vijana wa mtaani wenye vipaji na kuwasupport kwa kuwapeleka kwenye mafunzo waimbaji,wacheza mpira n.k hi nikuonyesha anasupport Sana na kuheshimu vipaji vya vijana mfano alipomwita bwakila na stanbakora kanisani bila kujalisha dini zao nikuonyesha kuwa anathamini wanachokifanya
Gwajima ni kiongozi asiye na dharau kwa mdogo wala mkubwa na kumuita bi kidude alifafanua kuwa nikumpa heshima kwasababu bi kidude ni mwanamziki mkongwe aliyependwa na kuheshimika na wengine ilawalioleta tafsiri tofauti ni mashabiki kama wewe kwenye kupaniki
Gwajima ni kiongozi wa Dini anayejishungulisha na maisha ya watu hasa vijana kwenye vipaji na kuwasapport bila kujali Dini zao mfano aliwaita vijana wasiosoma nakuwasikiliza nn wanataka kufanya na vipaji vyao na kuviendeleza hata kuwataftia vitendea kazi mfano wacheza Moira na bila kubagua Dini zao mfano mkubwa ni stani bakora na bwakila walialikwa kanisani kwako bila kujali Dini zao hi nikuonyesha anasapport sana na hana ubaguzi wa Dini wala kabila.
 
Hi issue ya udini inayochochewa na watu ni ili kugawanya watu ambao kwa nchi ya kidemocrasia kama yetu visiwe vinachochewa. Askofu GWAJMA Alice a anandoto , haiku na kifungu cha sheria Au kifungu cha Katibu kinacho mzuia mtu kuota ndOTO. Kama ndio to Yake ni kugeuza Miskiti mbona his sio issue , miskiti ni Nyumba ya sala kama kanisa. kama imamu angekuwa na Mdogo pia yakugeuza makanisa ni sawa pia , mungu ni mmoja.
TUSIGAWANYE WATU, Tanzania ni yetu sote
 
Gwajima ndio kiongozi naye muona anaeweza kuongoza Jimbo la Kawe ,
Huyo halima tumempa miaka kumi hamna alichofanya ,Sasa tunamtupilia mbali ili ajifunze kuwa ukipewa nafasi itumie
 
Kuna mambo mengine ni makosa makubwa sana kumlinganisha Askofu Gwajima na Halima Mdee. Kimsingi issue ya Kawe na ubunge iliishaisha na Halima anajua hawezi toa kichwa kabisa hapo. Mtu pekee anayejua nguvu ya Gwajima ni Tundu Lissu na ndio maana propaganda zote zilizokuwa zimeandikwa na Absalom Kibanda kwenye uzinduzi wa kampeni ya Halima Mdee alikataa kuziongelea kabisa na akasema waziwazi kuwa hazina mashiko. Watu wa karibu sana na Tundu Lissu wanafahamu fika kuwa wabunge wengi wa CHADEMA wakiongozwa na MBOWE wamezira kuongozana na Tundu Lissu kwenye kampeni zake.
 
Gwajima ndio kiongozi naye muona anaeweza kuongoza Jimbo la Kawe ,
Huyo halima tumempa miaka kumi hamna alichofanya ,Sasa tunamtupilia mbali ili ajifunze kuwa ukipewa nafasi itumie
Naomba tu kuelimishwa kidogo kuhusu huyu Gwajima. Je ndiye huyu anayemtukana Pengo au mwingine? Kweli huyu anazo akili nzuri? Kama siye natanguliza samahani lakini kama ndiye, nitashangaa watu wa Kawe kumpa ubunge huyu fyatu.

Your browser is not able to display this video.
 
Tathmini zinaonyesha wazi wazi kwamba wamemzira. Huwezi kuwa unatembea nchi nZima na mwenyekiti wako hajulikani yupo wapi. TUNDU lISSU ALIKuwa mtu anayeheshimika lakini inaonekana chama kinamzamisha, yaan hawezi heshimika tena Amekuwa mtu wa uongo kutwa kucha.
Chama kinajua kabisa nguvu ya Gwajima , Halima anajua saana kwamba Gwajima hamuwezi na ndio maana Khatibu anapambana sana kumchafua Gwajima Mitandanoni, Halima Hana sera kabisa sikuhizi.
 
Gwajima sio mbaguzi wala sio mdini kwa sababu amechimba visima vya maji ya kufanyia ibada na hapo hata ajatangaza nia wala ajafikiria kuwa mbunge sasa ubaguzi wake uko wapi jaribu kufikiria
Na kuhusu misikiti Tanzania kila mtu ana uhuru wa kuongelea dini yake na kuinadi mbona waislamu wanawaita wakristo Makafiri na hawajawahi kuhoji na tena wanasema hadharani kwenye vipaza sauti hiyo ni kauli yake ya kanisani kwake sio kwenye jukwaa la siasa kwaiyo huna haki ya kumshtumu Gwajima
Kuhusu Bi kidude kwanza ilo si jina halisi la muhusika na hapa Gwajima hakulizungumzia jina la Bi kidude kama Bi kidude katoa kama mfano waa kuwaonesha wana Kawe kuwa huyu akilizzaake zimeshachoka yani hawezi tena kufanya chochote kwenye habari ya siasa maana alicho kifanya hakionekani ametoa ahadi ajatimiza sasa kwa nini asifananishwe na Bi kidude ambae mpaka mauti inamkuta alikua amechoka hawezi tena kuimba kufanya shughuli zake hivyo hana tofauti na Bi kidude
Gwajima hajakosea wala hana Dharau
 
Kwahiyo usaidiwe nini?
 

Hoja nyepesi mno na za kipropaganda.
GWAJIMA anakubalika na Wananchi wa KAWE hata mkipandikiza chuki zenu na uongo ukweli juu ya mapenzi ya wananchi wa KAWE utabaki palepale na Tarehe 28 October akipewa kura zote ndo mtajua hamjui na Huyo MDEE anaeonekana Jimboni wakati wa kuomba kura, Hajawahi kufanya chochote pale wakati wa Utumishi wake.
 
FREEMAN MBOWE NA HALIMA MDEE WANAVYOMHUJUMU TUNDU LISSU

Kwanza kabisa tukubaliane kwamba mtanange wa uchaguzi umepamba moto huku kila chama cha siasa kikijitahidi kunadi wagombea wake na kushawishi wananchi kuwachagua.

Kwa namna nyingine tumeona vituko vingi vya wagombea wakiwa kwenye harakati za kutafuta kura majimboni na kwenye kata zao. Wakati mgombea wa uraisi kupitia CCM akiendelea kuchanja mbuga kusaka kura za wananchi, mgombea wa CHADEMA naye anazisaka kwa nguvu zote kura hizohizo katika upande mwingine wa nchi.

Je, nani alipiga picha ya Tundu Lissu akiwa ameachama (amepiga miayo) ambayo kwa jinsi wengi tulivyozoea hiyo huwa ni ishara aidha ya njaa, usingizi au uchovu? Ikumbukwe wazi kuwa wapiga picha wanaoambatana na mgombea ni wa chama husika na huweza kunasa matukio yote ya mgombea popote anapokuwa. Nimejithibitishia pasina shaka kuwa picha hiyo imepigwa na kusambazwa na mpiga picha maalum wa mgombea urais Tundu Lissu.

Nitarudi nyuma kidogo kuweka mtiririko sawa kutokana kile kilichotokea kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge Jimbo la Kawe zilizofanyika tarehe 29.08.2020 Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam.

Siku ya uzinduzi wa kampeni kulikuwa na makabrasha yaliyojaa uzushi mwingi kuhusu mgombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima yenye lengo la kumchafua na kuharibu taswira yake kwenye jamii. Makabrasha hayo ambayo yaliandaliwa na Absalom Kibanda pamoja na mwenzake ambaye hana hadhi ya kuongelewa, wakiwa wamepewa kazi hiyo na Halima Mdee yaligonga mwamba jukwaani baada ya Tundu Lissu kukataa kabisa kuyasoma alipokaribishwa kuongea.

Mtu mmoja aliye karibu na Halima ambaye nalihifadhi jina lake kwa sasa alinitonya kuwa Halima alisikika akiongea na watu wake wa karibu kuwa amechukizwa na kitendo cha Lissu kutokumsaidia kumshambulia mshindani wake Askofu Gwajima anayegombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kawe. Katika maongezi hayo Halima alimshutumu Lissu kuwa ana urafiki wa muda mrefu na Askofu Gwajima na sababu ya kutokumshambulia Askofu Gwajima ni kutokana na urafiki huo. Katika maongezi hayo Halima alihoji iweje mgombea Urais ashindwe kumwongelea mgombea mbunge wa chama chake na kumwombea kura sambasamba na kuwaonyesha wapigakura kuwa mpinzani wake hafai hata baada ya kuwa ameandaliwa mambo ya kumponda mgombea wa chama pinzani. Halima alijiapiza kulipiza kisasi kwa kutopigania kura za Lissu katika jimbo la kawe akisema kila mtu abebe msalaba wake.

Mkutano huo wa Kawe ulikuwa na watu wachache sana waliojitokeza kushangaa kile kinachoendelea baada ya picha ya uzinduzi wa jana yake uwanja wa Zakhiem Mbagala kusambaa ikiwa na watu wachache sana mpaka kupelekea TBC kufukuzwa uwanjani.

Kwa upande mwingine taarifa zilizothibitishwa zinasema kuwa kumekuwepo na mvutano na kuhujumiana kati ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho Tundu Lissu. Mikutano mingi inayofanywa na Tundu Lissu imekuwa ya hali dhaifu yenye maandalizi duni mpaka kupelekea picha za uchaguzi wa 2015 ambao Lowasa aligombea kutumika kuhadaa umma kuwa mikusanyiko ni mikubwa kwenye mikutano yao.

Mvutano mkubwa uliopo kati ya Tundu Lissu na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe unatokana na majibu ya hovyo yanayotolewa na Mbowe pindi anapoombwa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni ambazo ni makusanyo ya makato ya mishahara ya wabunge kwa kipindi cha miaka mitano. Hii ndio sababu kubwa ya miayo anayopiga Tundu Lissu huku mpiga picha wake akiwa tayari kusambaza picha hiyo ambayo inapeleka ujumbe unaosema UTAKULA JEURI YAKO.

Ni jambo lililo wazi kuwa kampeni za Tundu Lissu zinafanywa katika mazingira magumu sana ya kifedha na kupelekea kampeni hizo kukosa sura ya mgombea uraisi. Majukwaa anayotumia Tundu Lissu pamoja na PA system vyote ni hadhi ya chini sana kana kwamba anafanya kampeni za ubunge. Ukata wa fedha pia umedhihirishwa na tabia ya omba omba inayofanywa kwenye mikutano ya Tundu Lissu ambapo wananchi wanaohudhuria mikutano hiyo huombwa kuchangia fedha ili kusaidia gharama za kampeni kana kwamba chama kimeshituliwa na hakikuwa kimejiandaa kufanya kampeni za uchaguzi mkuu.

Ni jambo la fedheha kuwa Tundu Lissu katika hotuba zake akiwa kwenye majukwaa anasema wananchi ni masikini kwa sababu serikali ya Magufuli imeharibu uchumi lakini baada ya hapo anatembeza bakuli kuwaomba mchango wananchi hao anaowaita masikini.

Dr Alphonce Mwang'onda

alphoncejohn@gmail.com
 
Awe makini asiwafanye wapiga kura wa KAWE kama vile wale waumini wake wanaokubali chochote anachowaambia bila hata kitafakari.

Kawe ima watu makini wanaojitambua!!

Uzuri ni kwamba Kawe hamna Waikiki wa Gwajiboy! Waumini wake wanatoka nje ya Kawe!! Watu wa Kawe sio mafala Kama anavyofikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…