Uchaguzi 2020 Gwajima, dharau hizi hutafika popote

Uchaguzi 2020 Gwajima, dharau hizi hutafika popote

Kusema mahakama ya kadhi ni kitu kisichomhusu Gwajima ni Uongo au ujinga wa kutojua!

Mahakama ya kadhi itawaadhiri wote wa-islam , wakristo, wabudha, mpaka wasiomini how?! Ukitafakari utajua.

Mahakama ya kadhi itaondoa umoja wa kitaifa, how?!, Ukishiba utajua

Imagine leo nyumbani kwenu kila mmoja aamue kuishi anavyotaka ndani ya familia eti kisa anayofanya ni yake binafsi?! Itakuwa ni familia(taifa)?

Unaweza kuwa uko sahihi kwa mengine ila kwa hili hapana

Nimeona nichangie tu hapo ulipoingiza udini kama vile wewe ambavyo umeona tu mabaya ya Gwajima ukaacha mazuri yake!

Hakuna aliyemkamilifu, kila mmoja na mapungufu yake!
 
Kawe hatutaki nuksi na laana kwa kuchagua kiongozi anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja
Ahaaa, unampenda Gwajima kwa kuwa anapenda ngono za jinsia tofauti kama alivyorekodiwa kwenye ile video? Kama ana tabia ya kula waumini wake si ataanza kula wapiga kura wake? Haya bwana naona umeshinda. Kilangila.
 
GWAJIMA AZIDI KUHARIBU, DHARAU KWA BIBI KIDUDE NANI ATAZIVUMILIA?

Na, Robert Heriel

Mwanzo nilisema Gwajima ni Mbaguzi na mdini, sikuwahi kudhani anaudhaifu mwingine wa kudharau watu ambao hata hawahusiani na yeye kwa lolote Lile.

Nilimhusisha Gwajima na Ukabila kutokana na tuhuma zake za kutaka kuanzisha kikundi cha kikabila kutoka kabila lake chenye lengo la kumtetea Mhe. Rais ambaye anatoka Kabila lake. Nashukuru Jeshi la Polisi lilimuonya.

Pia nilimhusisha Gwajima na Udini pale alipopinga waziwazi mahakama isiyomuhusu hata kidogo, Mahakama ya Kadhi ya ndugu zetu Waislamu. Hiyo Mahakama ya Kadhi haimuhusu yeye wala sisi Wakristo, inawahusu Waislamu wenyewe na mambo yao. Sasa kilichomuwasha Gwajima ni nini atoke hadharani kupinga kitu kisichomuhusu. Hilo pia nilimuonya miaka ile.

Mwisho ni kauli yake inayohusu ndoto yake ya kugeuza misikiti kuwa Sunday school, na mashehe na maimamu kupigwa maji na kusilimishwa mbele ya msalaba. Alisema muota ndoto hafi mpaka ndoto yake itimie, kumaanisha yeye kabla hajafa atahakikisha misikiti itakuwa Sunday School. Hiyo watu wengi walimpiga, hasa mashehe, na wadau mbalimbali, mimi nami nikiwepo.

Sababu hizo ndizo zilizonifanya nishawishike kuikubalia akili yangu kuwa Gwajima hafai kupewa ubunge kwa jamii iliyostaraabika, watu wenye akili, na wenye muono wa mbali. Nilisema Gwajima anyimwe kura na wana Kawe, na mpaka sasa kundi kubwa la watu kutoka KAWE limenihakikishia kuwa halitampa kura huyo aitwaye Gwajima.

Sasa juzi juzi Gwajima katoa tena boko bila ya yeye kujielewa. Kitendo cha kumhusisha Marehemu Bibi Kidude katika siasa zake za vijembe ni dharau kubwa kwa Bibi Yetu huyo.

Kumdharau Bibi Kidude ni kudharau sanaa ya muziki hapa Tanzania na Zanzibar.
Kumdharau Bibi Kidude ni kuwadharau wanawake wanamuziki.
Kumdharau Bibi Kidude ni kuwadharau wazee wa kike waliojenga nchi hii.
Kumdharau Bibi Kidude ni kudharau harakati za haki za wanawake zilizopiganiwa na Marehemu Bibi Kidude.

Gwajima, atamuhusisha vipi Mzee anayeweza kumzaa Baba yake, na kumzaa yeye?
Gwajima wakati unatoa kauli ya kumshambulia mpinzani wako(bila shaka Halima Mdee) Ulikusudia kuwaambia nini wanaokusikiliza?

Hivi Gwajima unamchukuliaje Marehemu Bibi Kidude?

Fatuma Binti Baraka ndiye huyo Bidi Kidude anayoheshima kubwa sana katika nchi yetu kuliko hata wewe unavyodhani. Ni mwanamke aliyeweza kukomboa fikra za wanawake wengi, akaondoa dhana potofu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni ambapo akiwa na miaka 13 alitoroka kwao kwa kuepa kuolewa akiwa na umri mdogo. Bibi Kidude pia aliweza kufungua njia kwa wanawake wengi ambao walitamani kuwa wanamuziki, ukizingatia kwa zama za zamani mwanamke kujiingiza kwenye masuala ya muziki ilikuwa ni nongwa.

Bibi Kidude pia ni moja ya wanamuziki walioupaisha muziki wa Taarabu kimataifa kwa nyimbo zake za mikogo ya kipekee. Bibi Kidude pia mwalimu, kungwi wa unyago kwa mabinti wa zama zile ambao aliwafunda na mpaka anakufa hakuna ndoa iliyovunjika ambayo yeye alimfunda mwali.

Bibi Kidude anatuzo nyingi za kimataifa, siajabu wewe huna hata tuzo moja lakini unamshushia heshima Bibi yetu kwa mambo yenu ya siasa.

Bibi Kidude kaitangaza sana Zanzibar na Tanzania bara kimataifa, watalii wengi walikuja na kuburudika kwa nyimbo zake. Alafu wewe unaleta dharau za Rejareja.

Bibi Kidude anafahamika na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa. Pengine wewe sio msikilizaji wa Redio, ungekuwa msikilizaji wa Redio huenda ungemsikia Bibi Kidude kwenye Idhaa ya Kiswahili ya DW, wimbo wake wa Mhogo wa jang'ombe. Wewe Unaleta dharau zako.

Bibi Kidude ni ICON ya kimataifa wakati wewe ni Icon ya kanda ya mashariki hapa nchini.

Bibi Kidude alitunza na kuhamasisha utamaduni wa kiafrika kwa kutumia muziki wa Taarabu, Unyago, kuuza hina, kucheza ngoma na kuzipiga, wewe unahamasisha utamaduni wa kigeni kupitia dini yako hiyo.

Dharau zako zinakunyima mambo mazuri, Gwajima unamambo yako mazuri mengi lakini kinachokuharibia ni Udini, ukabila, na dharau.

Hayo mambo matatu yatakusumbua sana wewe mwenyewe.

Lakini yanaweza kuja kutusumbua sisi watu wengine endapo utapata nafasi za juu katika maamuzi na mamlaka.

Je Kawe watakuchagua ili uwadharau?
Je Kawe watakuchagua ili ulete mambo yako ya ajabu?

Pengine hujui siasa vyema, au unajua lakini hujui namna ya kuzungumza.
Mwenzako alikuita mrembo, yaani alikushambulia wewe binafsi kwa kutumia nomino ya jumla kwa kutaja neno "Mrembo" Wewe umetumia Nomino ya Kipekee kwa kutaja jina la Bibi Kidude. Hilo ndilo kosa lako.

Ulidhamiria kumdhalilisha au kumkejeli mtu mmoja lakini umetumia mtu mwingine yaani asiyehusika(Bibi KIdude) Matokeo yake umewadhalilisha wote wawili au kuwakejeli wote wawili. Yaani Hasimu wako na Marehemu Bibi Kidude.

Ushauri wangu;
Siku nyingine ukiamua kumtukana au kumtupia mtu kijiwe/kijembe basi tumia nomino au kitu kisicho na majina ya watu waliopo nchi hii. Kwa kufanya hivyo hutaleta mgogoro kama ulivyofanya wakati huu.

Mwisho: ACHA DHARAU KWA WATU WAZIMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

Taikoni wa Fasihi my class mate kisiwani high school Same
 
tatizo lako uliyeandika huu uzi una ushabiki wa chama ,alivvyosema bibi kidude nadhan ulielewa alimaanisha nini,ila kwasababu ya ushabiki wako unakuza mambo....

hiyo ni lugha ya kisiasa
 
Kwani huyu "MREMBO" katoa kauli gani kwa Bibi yetu??

Sijawahi kumkubali hata siku moja na huwa simsikilizi maana huwa anaongea UHARO.
 
Gwajima ana akili nyingi usije ukamfananisha na huyo mwanamke anayeishi kihuni
Subpost 2 - @kumbushodawson naona una Kazi maalumu na amfifiro ( 640 X 640 ).jpg
 
tatizo lako uliyeandika huu uzi una ushabiki wa chama ,alivvyosema bibi kidude nadhan ulielewa alimaanisha nini,ila kwasababu ya ushabiki wako unakuza mambo....

hiyo ni lugha ya kisiasa

Aliyetamka ameelewa alichokisema,
Kama hakuwa na nia mbaya unafikiri ni kwanini kaomba msamaha?

Unajua maana ya kuomba Msamaha ni kukiri kosa? Kutubu ni jambo jingine
 
Back
Top Bottom