Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Kwakuwa ushauri huu umekulenga wewe Baba Askofu, nitazingatia maandiko matakatifu kukushauri. Ukisoma Mithali 22:3 imeandikwa "Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara."
Desemba 27, 2021, Job Ndugai alitoa hutuba yake kuhusu Deni la Taifa. Maelezo yake yapo kwenye public record, hivyo sina sababu ya kuyarudia. Kuhusu usahihi au kutokuwa sahihi kwa aliyoyasema si mjadala wa leo. Mjadala wa leo ni nini kilimkuta baada ya hiyo hutuba yake.
Januari 3, 2022, Ndugai alinukuliwa akisema "Kama kuna neno lolote nililosema ambalo limeonekana kumvunja moyo Mheshimiwa Rais katika juhudi zake za kuijenga nchi, naomba radhi kwake na kwa Watanzania wote."
Hadithi hii ili hitimishwa na Job Ndugai mwenyewe kwa kusema "Ninapenda kuujulisha umma wa Watanzania kwamba leo, Januari 06, 2022, nimeandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), nikijiuzulu wadhifa wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni uamuzi binafsi nilioufanya kwa hiari yangu mwenyewe kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa langu, serikali, na chama changu CCM."
Karl Marx katika essay yake ya "The Eighteenth Brumaire of Louis Bonaparte1852" anaandika "History repeats itself, first as tragedy, second as farce." Katika himizo lake juu ya ukweli huu, George Santayana katika kitabu chake "The Life of Reason 1905" anaandika "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it."
Ni jambo lililowazi kuwa ww ni mtu mashuhuri na unao ushawishi ambao hauwezi kubezwa. Hata hivyo pamoja na nafasi yako ya ubunge na ujumbe wa NEC, sitakuwa nimemtendea haki Job Ndugai nikimlinganisha na ww. Ndugai alikuwa mkuu wa mhimili, spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Kamati kuu, Mjumbe wa NEC na Mjumbe wa mkutano mkuu. Lakini ilichukua siku 10 tu, habari yake ikawa imeisha. Kama historia hujirudia ww utaponaje?
Katika Luka 23:28,31 tunasoma "Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?"
Kwenye riwaya ya "Things fall apart" ushauri wa Obierika kwa Okonkwo ulikuwa "If I were you, I would have stayed at home. What you have done will not please the Earth."