Gwajima: Kama waliutenda hivi mti mbichi, utakuwa wewe mti mkavu?

Ahsante sana kwa maandishi mazuri yenye nukuu mbalimbali. upo vizuri
 
Jadili hoja usimjadili mtu.

Mtu hata akishindwa keo, hilo halina maana hoja yake haina maana, pengine role yake ni kufungulia geti wengine wapate urahisi kupita.

Hata Musa alianza safari ya kwenda nchi ya ahadi lakini vitabu vinasema hakufika.

Sasa utasema Musa alishindwa mission kwa sababu hakufika?
 
Kwa kua umemaliza na Chinua Achebe nakumbuka anasema " when Okonkwo returned from exile he found kinsmen have become soft like women"
 
Ru
Tungo nzuri sana inavutia kuisoma,ila ungekuwa enzi za Musa na Yoshua ungeshakufa,Mungu asingeruhusu roho dhaifu kama yako kwenda kuichunguza Canaan.
 
Ndugu dakatari umeandika Mengi sana.. Ila tambua hata katika Biblia kila mtu alikuja kwa assignment yake.

Ukiwa umesikia Gwajima utakuwa umenielewa..
 
Ndugai na Watanzania wengine waliowahi kuwa kwenye nyadhifa shida yao kuu NI maisha baada ya uongozi, hilo ndio huwapa uoga na kushindwa kusimamia kweli maana hofu yao iko kwenye supply ikikatwa.
Hili Kwa kiasi kikubwa huchangiwa na wengi wao kutokuwa na income nje ya siasa au kutojua kutafuta hela nje ya siasa.

Gwajima ana faida ya kujua kuishi kabla ya siasa, kumiliki hela kabla hajawa mwanasiasa.
Ukola na kutojali kwake na tabia yake vinaweza kufanya asiwe muoga na baadala yake akapigana upande wa haki kama kweli dhamira yake ni kupigania haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…