Uchaguzi 2020 Gwajima, Kawe tunakupa miaka mitano!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Uchaguzi umekwisha.

Kwa jimbo la Kawe, Gwajima ndio kidedea kwa miaka mitano ijayo. Sasa Askofu Gwajima kaa chonjo, waingereza husema, you should hit the ground running.

Yule dada Halima katuweka solemba kwa miaka kumi. Kero hasa za barabara, zile alizozitamka hata Rais Magufuli, tunaomba zishughulikiwe toka sasa.

Barabara za Ndumbwi hadi Baraza la Mitihani, NSSF road, Kilongawima road, Salasala hadi Maranda, Tegeta hadi makaburi ya Kondo na hata barabara za Mbweni na Makongo.

Hilo ndo deni la ubunge.

Gwajima nenda Lobby, piga makelele, piga ua, barabara hizi lazima zijengwe.

Miaka mitano ni mifupi sana, lakini kama Mtoni Kijichi iliwezekana Kawe tutashindwa nini?
 
Gwajima kapigiwa promo ya nguvu na JPM mwenyewe.
Asipo perform Kawe hata JPM lawama hazita msamehe.
Lakini tunamfahamu JPM atatenda.
 
Magufuli ndio mwenye mamlaka yote sio wewe Mkuu
Inategemea jiwe ameamkaje
 
Siwezi hata mara moja kufumba macho nijidai sikumbuki uhuni uliofanyika, Gwajima kashinda kwa wizi wa kura zaidi ya 50% hilo halikwepeki, msimdanganye akajiita mbunge wa watu wa Kawe, huyo ni mbunge wa kura feki.

Askofu feki anaefumbia macho wizi kwasababu umemnufaisha.

#selfish
 
Sisi Kawe ni tunatoa miaka kumi kumi, hivyo ni mpaka 2030.
P
 
Chuki ni dhambi.zaidi ya yote chuki,hasira na kinyongo huzaa Kansa na presha.
Uwe na siku nzuri
Asante mkuu.
Kuna watu hawaelewi kuwa chuki humuumiza zaidi yule achukiaye na si anayechukiwa.
Ni kama tindikali, isipobebwa na kwenye glasi basi unaunguza mikono yako hata ukiweka kidole.
 
Why doubt him, mtu amefanya makubwa while he was nobody, sasa akiwa somebody?, Kawe itapaa!.
P
Mkuu sisi tunampa angalizo tu, kuwa Kwe tunataka nini.
Yule wa chama kingine katuchelewsha saana kwa miaka kumi ya bure aliyokaa.
Mimi Dar natembea sana.
Mton Kijichi ndiyo iliyonishangaza katika miaka mitano iliyopita.
Hata kule Tandika kuelekea Buza barabara za lami kibao.
Tulikuwa tunajiuliza mbona sisi....!
Tukajua wa kumtosa, na tumemtosa.
Gwaji Boy asipotenda miaka hii mitano atakuwa hati hati.
 
Hivi nani alimdanganyaga Mdee kuwa mbunge ni lazima uwe mbishi na kulazimisha kufungwa ili wananchi wakukubali? Mtu unasahau majukumu yako kwa kweli, miaka 10 hajafanya chochote jimboni kwake zaidi ya kukamatwa na kutiwa ndani mara kibao eti anawakilisha wananchi. Hatujamtuma afungwe kwa ajili yetu hata siku moja, tafadhali Gwajima karibu ila usiwe mpuuzi kama Mdee.
 
Wewe jamaa kama kuna mtu nachukia sana humu kama mnyama ni wewe.Umejaa sana unafki na njaa njaa. Huna msimamo hata kwenye ukweli unahangaika tu
Mkuu, mchukie kidogo kidogo usije ukajilete pressure na depression mpaka ukajitundika bure!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…