dindilichuma
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 1,736
- 2,699
Kila siku nikifuatilia nyuzi hapa JF nakutana na nyuzi nyingi zikimzungumzia Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kawe askofu Josephat Gwajima.
Nabaki najiuliza kwa majimbo yote ya Tanzania na hata majimbo tu ya Dar kwanini yeye tu anazungumziwa zaidi Kwanini nguvu kubwa inatumika kumzungumzia?
Nimefuatilia na kukuta Hoja nyingi anazosemwa Gwajima ni mambo binafsi na ya kazi zake Za kila Siku binafsi. Sioni akipigwa kwa Sera zake Kama mgombea ubunge. Anafunguliwa nyuzi nyingi Sana kuliko mgombea ubunge yeyote.
Nimeanza kuamini Gwajima inawezekana anauwezo mkubwa na kama asingekuwa nao wapinzani wake wangempuuza na wasingehangaika nae. Ila Gwajima ni tishio Sana kwa nafasi aliyogombea.
Unaweza kuona mtu anaanzisha uzi kuhoji ujenzi wa kanisa linaloongozwa na Gwajima na mtu huyohuyo akashindwa pengine kuhoji ujenzi wa ofisi ya Chama chake kianachopokea ruzuku. Hapo unapata picha ni nini kinaendelea kwa anaehoji.
Tujaribu kuwahoji wagomhea wetu kwa sera na ahadi zao bila kuwabagua. Ubunge ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania na Jimbo lako wanajipatia maendeleo na Maisha yao yanakua rahisi. Mbunge ashirikiane na kuiambia serikali na taasisi na yeyote mwenye Masaada juu ya kero na mambo Mazuri yanayopaswa kufanyika jimboni kwake.
Baada ya Tarehe 28/10/2020 tunaweza kupata jibu ni kwanini Gwajima anazungumzwa Sana hasa na wasio penda awe mbunge na wanaopenda awe mbunge hawazungumzi Sana.
Hamkani Shwari si Shwari tena.
Naamini tutaenda kupiga Kura.