Kilichotokea si cha kushangilia bali kulia na kusaga meno. Wapo waliotegemewa wakashindwa na waliokuwa hawategemewi "wakashinda" kama akina Gwajima. Natabiri machafuko nchini. Kwa taifa linalotaka kusonga mbele, hutanguliza haki. Unapoona matapeli na wachumia matumbo kama Gwajima "wakishinda"jua kuna tatizo. Ni bahati mbaya kuwa busara na hekima vimetukimbia. Tushangilie maangamizo na vilio vyetu baadaye. Ama kweli wazungu walituweza walipotuletea udikteta uitwao demokrasia. Ni mawazo tu. Nikita Khrushchev imla wa Urusi aliwahi kusema kuwa kilicho muhimu si kura bali azihesabuye. Hili limejidhihiri shahidi Tanzania. Laiti Mkapa na Nyerere wangekuwa hai, huenda wangetusaidia kuiona hekima iliyotukimbia mchana kweupe. Nawalilia wahanga wa Zanzibar.