Gwajima siyo Kibwetere ni mfuasi wa Kibwetere aliyenusurika

Gwajima siyo Kibwetere ni mfuasi wa Kibwetere aliyenusurika

Gwajima ashamaliza mbna mnaendelea kupambana na kivuli chake wazee, na mapokezi yake kitaa ni makubwa Sana , namshaur akae kimya msije mkamuua kama mlivyofanya Kwa jiwe! Watachanjwa tu wale ambao itawalazimu kufanya hvyo ili upate vitu fulani fulani!
Kumbe jiwe walimuua pamoja na ukatili wake wote alikutana makatili zaidi yake. Mungu mkubwa
 
Kibwetere?!
sheed.png


pachah1.png
 
Wafuasi wa Kibwetere wamegawanyika makundi mawili, wapo wanaotaka kujifanya wanathamini afya zao na kwamba Kibwetere ailiwapotosha au walijua kabisa kwamba Kibwetere anawapotosha lakini kwakuwa walimdharau Mungu wakamthamini Kibwetere Basi kila alichofanya walimpigia makofi. Alipowaambia wafunge macho walifunga na alipowaambia wasujudi walisujudu.

Siku Kibwetere anaondoka Duniani na baada yakuchoma hekalu na kuwapoteza wengi waliomzunguka, ndipo wale walionusurika walipojitokeza nakuanza kumpinga wakiamini hatorudi Tena. Badala wawapongoze wale waliompinga Kibwetere akiwa hai wameendelea kupambana nao na kuwatia ndani waasisi wa vuguvugu lakumpinga.

Gwajima wa Kawe (nachelea kukubali Ni Mchungaji wa kweli) amebaki kumtetea Kibwetere akiamini ipo siku atarejea Duniani. Amebaki kupingana na Ulimwengu na anachofanya Sasa nikutafuta wafuasi ili awatie Moto Kama alivyofanya Kibwetere Senior. Ni kweli amejizolea waumini na atawachoma Moto maana waamini wake wameshindwa kupiga goti nakuhojiana na Mungu wanasubiri Gwajima ndiye aombe kwa niaba yao na Kisha awape maono. Nawakumbusha waumini, Gwajima anachokifanya nikuimarisha misingi iliyowekwa na Kibwetere ili wafuasi wengi waungue kwa Moto kwa maono yake anayoamini na kuwaaminisha watu kwamba ni maono kutoka Mbinguni.

Kwenye hii Vita si Vita yakuelekezwa kwa amri ni Vita yakuomba upewe ufunuo uchanje au usichanje maana hata mwisho wetu hapa Duniani hautotokana na Uvico tu Bali utaendelea kuhusianishwa na ajali, maradhi, sumu nk. Tukumbuke wapo vichaa awajawahi kuchukua taadhari na haukuna ambaye amewahi kututhibitishia kwamba wameathirika kiasi gani, tunawaona wapo kwenye maeneo yao kila siku, means anayewalinda Ni Mungu maana anajua sisi wenye akili timamu atupo tayari kuwawazia.
Dah umeniikumbusha mbali sana....Kibwetere alikuwa genious sana sasa sijui aliowapiga kibiriti walifika mbinguni kweli au la
 
Kwakiswahiki hii formu inasemaje yoyote anayejua kibeberu anisaidie nataka kuchoma chanjo nimekwama sieliwi kibeberu kabisaView attachment 1872422
Mimi (jina lako), Umri wangu miaka....., Ninaishi kata ya......Wilaya ya.....Dini yangu.......

Nimeambiwa na wataalam wa afya juu ya Usalama, ufanisi na Madhara mabaya yanayoweza kutokea kutokana na Chanjo ya Covid-19.

Niko Tayari kupokea chanjo ya Covid-19 na pia sintohusisha/sintoiwajibisha serikali ya Tanzania endapo nitapata madhara yoyote mabaya yatakayosababishwa na chanjo hii

Sahihi ya Mteja.......
 
Mimi (jina lako), Umri wangu miaka....., Ninaishi kata ya......Wilaya ya.....Dini yangu.......

Nimeambiwa na wataalam wa afya juu ya Usalama, ufanisi na Madhara mabaya yanayoweza kutokea kutokana na Chanjo ya Covid-19.

Niko Tayari kupokea chanjo ya Covid-19 na pia sintohusisha/sintoiwajibisha serikali ya Tanzania endapo nitapata madhara yoyote mabaya yatakayosababishwa na chanjo hii

Sahihi ya Mteja.......
Allah kumbe
 
Back
Top Bottom