Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ukiamua kutaja maeneo ya jiji la Dar es salaam yanayo athirika na mvua za kila mwaka huwezi kusahau kutaja eneo la Basihaya linalopatikana jimbo la Kawe.
Basihaya ni miongoni mwa maeneo yanayojaa maji kila mwaka pindi msimu wa mvua unapofika. Barabara (Bagamoyo road) hufunikwa kabisa, maji na udongo hujaa na miundombinu mingine ikiathirika pia kwa kiasi kikubwa.
Chanzo cha tatizo hili ni nini?
Eneo hili halina mitaro ya maji hivyo maji yanayotoka upande wa Tegeta hujikusanya hapo. Aidha, kukosekana kwa udhibiti wa maji yanayotoka mlima wa wazo ambao huyatiririsha hadi barabarani ndiyo vyanzo vikubwa viwili vya tatizo hili.
Gwajima anahusikaje?
Pamoja na kutoa ahadi lukuki za kupeleka watu ulaya, kununua boti za uvuvi, Mchungaji Josephat Gwajima aliahidi kutatua tatizo hili sugu kwa wakazi wa Basihaya. Yeye ndiye mbunge wa eneo hili.
Miaka inakimbia, siku zinayoyoma. Gwajima haonekani.
Adha hii inazidi kuwa kubwa kila siku. Ni hadi watu hawa wafe kwa magonjwa ya mlipuko ndiyo wakumbukwe? Kwanini maoni na maombi yao hayasikilizwi? Lengo la Gwajima kusema uongo kuwa atashughulia kero hii lilikuwa ni lipi? Ufanisi wa bandari ya Bagamoyo utakuwaje kama sehemu ya barabara inayounganisha sehemu hii ina hali mbaya kiasi hiki?
Askofu Gwajima, tekeleza ahadi yako.