Nyie Wapambe wa Mengi,
Haya yambo kayapigia sana kelele humu ndani Mzee Mwanakijiji. Haya mambo ya ohh mbona siko peke yangu, ohh ni jukumu la serikali, ohhh kifo cha wengi harusi, ndiyo yanayotufanya milele tubaki palepale.
Mengi ni mtu maarufu sana na milele popote alipo ataonekana yeye. Kusema kuna wengine pale basi si awaite na kuwaambia wachangie kujenga hiyo barabara? Anasubiri na yeye kila kitu maana kashalipa kodi?
Nikiwa naishi Ilala Flats, tulikuwa na jirani yetu mmoja Mhandisi, Mzee Ngonyani. Kutokana na mabomba ya maji machafu kuziba, maji taka yalikuwa yakimwagika nje na kutoa harufu mbaya sana, wenyewe wakisema MAFURIKO. Yakitokea kinachofanywa mnafunga madirisha ya upande huo. Mhandisi huyo alifika point akachoka, akaja kuitisha mkutano kuwa ataenda kununua mabomba na kugharamia ujenzi wake. Wanaotaka kumsaidia wamsaidie na wasiotaka waache. Huwezi amini, wote walitoa hela. Tatizo dogo lipo kwa Msomali, yeye siku zote anasema "hana muda, wampe gharama na yeye atatoa pesa - Yes alitoa hela..." Wakati mwingine ni vitu viko ndani ya uwezo wetu ila tunakosa KIONGOZI. Kila mtu au anaona hilo HALIMHUSU au anasubiri FULANI aanze.
Tusiwe waoga namna hiyo. Mwambieni Mzee ashirikiane na jirani zake hao wenye mashine za kufulia sijui, na wenye viwanda wengine, unaweza kukuta wakapata hata msaada kutoka EU kama wao ni masikini saana na ile barabara ikajengwa kwa Zege ili kuhimili mizigo mizito kutoka kiwandani. Cement Tanzania ipo, mawe na mchanga upo, shida iko wapi? Ni pesa tu. Hao watu kama wameweza kuwa na Viwanda, kinawashinda nini kujenga barabara au Parking?
Mnaweza kumtetea sana ila ukweli ni kuwa UJUMBE UMEMFIKIA. Na kama nyie ni Wapambe wake basi MFIKISHIENI. Siku anafungua na aseme kuwa wameijenga kwa ushirikiano na wenzake. Labda itakuwa mfano kwa watu wengi huko mitaani kushirikiana na kuweka mazingira yao katika hali safi. Tunaisubiri saana serikali wakati serikali yenyewe ni ya CCM (Chama Cha Mafisadi).