Habari ni taarifa kuhusu tukio au matukio fulani inayowasilishwa kwa mtu au umma kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Haki ni stahili alizonazo binadamu kutokana na asili ya utu alionao na sheria ni mfumo wa kanuni na taratibu zilizowekwa kwenye jamii na mamlaka kwa ajili ya kuongoza matendo na kuratibu mahusiano baina yaoili kukuza, kuendeleza na kudumisha amani, utulivu na utengamano.
Uhusiano kati ya habari, haki na sheria ni mkubwa, kwani katika maisha ya kila siku watu wanawasiliana na kupashana habari mbalimbali zinazohusu masuala ya jamii. Kutafuta, kupokea na kusambaza habari ni moja ya haki za binadamu, na ili kuhamasisha, kukuza na kulinda haki hii ya msingi ni lazima kuwe na utawala wa sheria zinazosimamia udhibiti wa habari na mawasiliano kwa umma.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya 18; kila mtu ana haki ya kuwa na maoni na kutoa nje mawazo yake, haki ya kutafuta, kutoa, kupokea au kusambaza taarifa ndani na nje ya mipaka ya nchi, haki ya kupata taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu yanayoendelea kuhusu maisha, shughuri za wananchi na masuala muhimu ya jamii, na haki ya kulindwa dhidi ya kuingiliwa kwa mawasiliano yake.
Katika mazingira yasiyo ya kawaida baadhi ya sheria zilizowekwa hapa nchini ili kudhibiti huduma za utoaji habari, vyombo vya habari na mawasiliano kwa umma, zinakiuka haki ya upatikanaji wa habari kwa watu na kuminya uhuru wa maoni na vyombo vya habari kinyume na katiba. Sheria hizo ni kama zifuatazo.
Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ya 2022. Sheria hii nambari 11, ya 2022 ilipitishwa na bunge mnamo Novemba 1, 2022 na kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani mnamo Decemba 2, 2022. Dhumuni la sheria hii ni kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya serikali na vyombo binafsi.
Sheria hii inaminya uhuru wa vyombo vya habari kutafuta, kuandika na kuhariri taarifa pasipo kuingiliwa na serikali ili kuweza kusambaza habari ndani na nje ya mipaka ya nchi, kwani sheria hii inamlazimu mkusanyaji au mchakataji wa taarifa ambaye anakusudia kusafirisha taarifa nje ya nchi kupata kibali kutoka kwa tume ya ulinzi wa taarifa binafsi. Pia sheria hii imeipa tume nguvu ya kutozingatia sheria yoyote pindi inapotekeleza majukumu yake. Hali kadharika tume imepewa nguvu ya kufika mahali popote na kuchukua kifaa au vifaa vyovyote ambavyo tume inadhani vina taarifa zinazohitajika kwa ajiri ya uchunguzi.
Sheria ya makosa ya mtandao ya 2015. Kufuatia ukuaji kwa kasi wa teknolojia ya habari na mawasiliano nchini, sheria hii ilipitishwa na bunge mnamo Aprili 1, 2015 na kuidhinishwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Daktari John Pombe Magufuli mnamo April 25, 2015. Sheria hii inaminya haki ya mtu kutafuta, kutoa na kupokea taarifa. Hii ni kutokana kuwa kifungu cha 8, kinazuia mtu yeyote kutoa taarifa za umma endapo serikali itasema taarifa hizo ni za siri hata kama taarifa hizo zina maslahi kwa umma.
Kadharika, sheria hii inakiuka haki ya mtu kulindwa dhidi ya kuingiliwa kwa mawasiliano yake. Hii ni kutokana na kifungu cha 21(1), kumlazimu mtoa huduma za mtandao kutoa taarifa za mteja wake kwa jeshi la polisi pale zitakapohitajika bila kibali cha mahakama. Kwa upande mwingine, sheria hii inamuweka mtumiaji wa mtandao katika mazingira ambayo si salama, kwani kwa mujibu wa kifungu cha 7(2b), mpokeaji wa ujumbe mtandaoni anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa jinai.
Sheria ya haki ya kupata habari ya 2016. Sheria hii ilipitishwa na bunge mnamo Septemba 7, 2016 na kuidhinishwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Daktari John Pombe Magufuli mnamo Septemba 23, 2016. Dhumuni la sheria hii ni kusaidia watu kupata taarifa, kueleza aina ya taarifa ambazo jamii ina haki ya kuzipata na kusisitiza uwazi na uwajibikaji kwa vyombo au watu wenye taarifa.
Sheria hii inaminya haki ya kupata taarifa. Kifungu cha 5 kinaruhusu raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee kupata taarifa. Hii ni kinyume na kanuni za kimataifa na viwango vinavyokubalika katika haki ya upatikanaji wa taarifa. Kwa upande mwingine, sheria ya haki ya kupata taarifa ya 2016 haielezi maana ya maslahi ya umma, swala ambalo linaweza leta mazingira magumu ya upatikanaji wa taarifa kwa watu na kuzuia kusambaa kwa taarifa za kidiplomasia kwa kigezo kuwa zinahusiana na usalama wa taifa.
Sheria ya huduma za habari ya 2016. Sheria hii ilipitishwa na bunge mnamo Novemba 2, 2016 na kuidhinishwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano hayati Daktari John Pombe Magufuli mnamo Novemba 16, 2016. Dhumuni kuu la sheria hii ni kuhamasisha weledi katika tasnia ya habari nchini.
Sheria hii inaminya uhuru wa vyombo vya habari kutoa maoni, na kuathiri mchakato mzima wa kutafuta, kuandika na kuhariri habari. Hii ni kutokana na vifungu nambari 6 na 7 kuipa serikali udhibiti mkubwa kwa vyombo binafsi vya habari kwa kuvitaka kutangaza kuhusu masuala yenye umuhimu kwa taifa. Kadharika, udhibiti mkubwa wa serikali kwa vyombo binafsi vya habari unakiuka haki ya watu kupata taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari kwani unaathiri upana wa vyombo binafsi vya habari kujieleza.
Katika nchi yoyote, athari zinazoweza kujitokeza kutokana na sheria zinazokiuka haki ya watu kutoa maoni, kupata habari, pamoja na uhuru wa vyombo vya habari ni; jamii kukosa utengamano, utulivu na amani. Hali kadharika mvutano kati ya mamlaka za serikali na wananchi katika utekelezaji wa masuala muhimu ya umma.
Ni wajibu wa serikali kupitia wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari chini ya waziri mwenye dhamana, kuwasilisha bungeni muswada wa marekebisho ya sheria za nchi, za udhibiti wa vyombo vya habari ili kukuza utawala wa sheria unaoheshimu haki ya watu kutoa maoni, haki ya kutafuta, kutoa, kupokea au kusambaza taarifa ndani na nje ya mipaka ya nchi, haki ya kupata taarifa wakati wote na haki ya kulindwa dhidi ya kuingiliwa kwa mawasiliano yao.

Upvote
6