Ni kaka yangu ninaye mfuata kwa mara ya tano. tulitofautiana tangu mwezi wa sita mwaka huu kutokana na kushindwa kutimiza ahadi ya kumpatia pesa ya mradi wa kufuga ng'ombe wa maziwa.
Nikiwa likizo ya desemba mwaka jana kaka yangu huyo alinipa wazo hilo katika mchanganuo wake alisema anahitaji kiasi cha milion 3 na laki tisa kukamilisha kila kitu. Nili haidi kuchangia sh. milioni 1 na laki 5 kwa kipindi cha miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu. Ahadi hiyo ilitokana na matumaini ya barua ya kupandishwa daraja la mshahara wangu (mimi ni mtumishi wa halmashauri idara ya afya) kiasi kilicho oneshwa kwenye baruwa hiyo kingeniwezesha kutekeleza ahadi yangu kwa kaka, lakini la kusikitisha ni kuwa tangu nipokee barua ile, novemba mwaka jana sijaona badiliko lolote la mshahara wangu na hivyo kushindwa kutekeleza ahadi hiyo. wenzangu sita nilio pokea nao barua ni wawili tu walio badilishiwa mishahara na mwezi wa tatu watumishi wengine walipewa baruwa zenye kuwapandisha madaraja pasipo mishahara kubadilika.
Ndugu zangu kushindwa kutimiza ahadi ile kaka yangu hakunielewa hasa pale nilipo punguza kiasi kidogo cha pesa nilicho kuwa namtumia kusapoti vijana wake wanao soma (mwanzoni aliweza kusomesha vijana wake kwa kulima pamba ambayo bei yake kwa sasa imeshuka na haitabiliki), nilipunguza msaada huo kwani nami humo katikati nilianzisha familia yangu.
Juzi nilikuwa kijijini kumsalimia mametu, nilikuta kakangu kanishitaki kwa mama jinsi nilivo mdanganya, kakangu ni mtu anaye aminika sana na ni kiongozi wa ccm, nyumbani kapamba bendera za kijani za kutosha. mama alinieleza malalamiko yale nikawaeleza jinsi selekali ya ccm ilivyo tutapeli,jinsi tunavo lishwa ugali kwa picha ya samaki, niliwaonesha na baruwa ile yenye figure ambazo sikuwahi kupokea. nili mwambia kaka yangu kwa kuikumbatia ccm ndo anakuza matatizo haya, nilimweleza jinsi selekali ilivyo na wajibu wa kumtafutia soko zuri la pamba yake hivyo tupambane kwa pamoja kuiondoa serekali ya ccm inayo tuhujumu. nime mweleza wazi kuwa sitaweza kumsaidia hasa akiendelea kuikumbatia ccm. Barua ya kupanda daraja ilimgusa sana, hadi akaniuliza kuwa nimecheleweshwa kwa muda gani nikamwambia asome tarehe kwani hadi sasa salio linasoma la zamani,akatikisa kichwa akiashiria kusikitika. Jana jioni nimepokea taarifa kuwa bendera zote pale nyumbani kazishusha!.
Natoa rai kwa watumishi wengine wa idara zote wanao lishwa ugali kwa picha ya samaki, ambao hawajapanda daraja ingawa sifa za kupanda wanazo (maana hata baruwa ya kupanda daraja hadi itoke ni mbinde) wawaelimishe wategemezi wao jinsi serekali ya ccm inavyo sababisha bajeti zao kuwa ngumu, wawaambie kwa vielelezo kama vipo wataeleweka zaidi, wawaeleze chanzo cha tatizo kilipo nao watawaelewa.