Habari kwako ewe Mtanzania

Habari kwako ewe Mtanzania

Seth saint

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2020
Posts
1,115
Reaction score
2,464
Habari za wakati huu wana wa Adamu, wana wa Ibrahimu baba yetu wa imani.

Nipo hapa kukupa ujumbe ewe ndugu yangu kuwa ni wakati sasa tunahitaji kufanya mabadiliko katika mienendo yetu na maisha yetu hapa duniani.

Ni kipindi sasa tunashuhudia matukio mengi hapa duniani ambayo hakuna ajuaye nini chanzo chake nasio kama chanzo hatukijui bali tumefanya mioyo yetu migumu huku tukiamini katika akili zetu na kusahau hizi tunazoita akili chanzo chake ni nini.

Wakati tulio nao sio mzuri ndugu zangu.Mwenye kujua kusoma alama za nyakati atakuwa analiona hilo.Tizama bwana wako yu karibu hivyo anakukumbusha kufanya yale yaliyokuwa mema kabla hayajotokea yale ya Sodoma.

Sipo hapa kutoa shuhuda yoyote au kuwa mtume kati yenu bali kukumbusha kwamba huku tunakoelekea sio kuzuri.Kabla ya mwaka huu kuisha mwanadamu atapitia kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuelezwa sehemu yoyote katika vitabu vya historia ya mwanadamu.

Hakuna ajuaye ujio wa bwana si malaika wala mwanadamu bali yule tu mwana ndio ajuaye lini. Kwa wale mliokuwa UDOM mwaka wa 2016 kumbuka kilichotokea mnamo mwezi wa sita college ya humanities.Hesabu toka mwaka huo mpaka sasa imefika miaka mingapi.

Ewe mtanzania mwenzangu taifa lako limechaguliwa na bwana hivyo badilika na tenda yaliyo mazuri mbele ya macho ya bwana wako au utapitishwa kipindi kigumu kuanzia sasa.

Barikiwa ewe uliyetayari kubadilika. Ombea taifa lako, ombea dunia nzima. Ni katika jina la Baba, la Mwana na la roho Mtakatifu. Amina. Mfungo mwema kwa ndugu zetu mnaondelea na mfungo.
 
Habari za wakati huu wana wa Adamu, wana wa Ibrahimu baba yetu wa imani.

Nipo hapa kukupa ujumbe ewe ndugu yangu kuwa ni wakati sasa tunahitaji kufanya mabadiliko katika mienendo yetu na maisha yetu hapa duniani.

Ni kipindi sasa tunashuhudia matukio mengi hapa duniani ambayo hakuna ajuaye nini chanzo chake nasio kama chanzo hatukijui bali tumefanya mioyo yetu migumu huku tukiamini katika akili zetu na kusahau hizi tunazoita akili chanzo chake ni nini.

Wakati tulio nao sio mzuri ndugu zangu.Mwenye kujua kusoma alama za nyakati atakuwa analiona hilo.Tizama bwana wako yu karibu hivyo anakukumbusha kufanya yale yaliyokuwa mema kabla hayajotokea yale ya Sodoma.

Sipo hapa kutoa shuhuda yoyote au kuwa mtume kati yenu bali kukumbusha kwamba huku tunakoelekea sio kuzuri.Kabla ya mwaka huu kuisha mwanadamu atapitia kipindi kigumu ambacho hakijawahi kuelezwa sehemu yoyote katika vitabu vya historia ya mwanadamu.

Hakuna ajuaye ujio wa bwana si malaika wala mwanadamu bali yule tu mwana ndio ajuaye lini. Kwa wale mliokuwa UDOM mwaka wa 2016 kumbuka kilichotokea mnamo mwezi wa sita college ya humanities.Hesabu toka mwaka huo mpaka sasa imefika miaka mingapi.

Ewe mtanzania mwenzangu taifa lako limechaguliwa na bwana hivyo badilika na tenda yaliyo mazuri mbele ya macho ya bwana wako au utapitishwa kipindi kigumu kuanzia sasa.

Barikiwa ewe uliyetayari kubadilika.Ombea taifa lako,ombea dunia nzima.Ni katika jina la Baba,la Mwana na la roho Mtakatifu. Amina. Mfungo mwema kwa ndugu zetu mnaondelea na mfungo.
Amen, Mungu atusaidie tuweze kuzitambua nyakati hizi za mwisho na tutende yaliyo mema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom