Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

"Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

"Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali," alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

"Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika," alibainisha Profesa Lekule
 
Hizi tafiti siku hizi kila kitu hakifai.Jana tu mwingine kanitumia kwamba tusiweke vyakula vya moto kwenye vyombo/vifaa vya plastik tutapata kansa hujakaa vizuri chumvi sukari sio nzuri mwishowe sasa tutaambiwa kulala kwenye nyumba ya bati sio nzuri kwa afya yako.
 
kimsingi hata ng'ombe wanao minyoo wa aina hii wenye cyst wanaokaa kwenye nyama/misuli na moyo, ambapo kwa ng'ombe wanaitwa cystercercuss bovis (CB)na kwa nguruwe wanaitwa cystercercus cellulosae (CC). hivyo ngoma droo, wote walao nyama kwa ujumla wanakuwa katika hatari hii.

Pengine kwa nguruwe inaweza kuwa hatari kwakuwa sijajua machinjio ya nguruwe na ukaguzi wake na inaweza kuwa sio hatari kwakuwa maambukizi hayajafika kwenye eneo la mfugaji husika vilevile sio nyama zote za ng'ombe zinazoliwa zinapita kwenye machinjio pia.
stop worrying and start living.
 
Hizi tafiti siku hizi kila kitu hakifai.Jana tu mwingine kanitumia kwamba tusiweke vyakula vya moto kwenye vyombo/vifaa vya plastik tutapata kansa hujakaa vizuri chumvi sukari sio nzuri mwishowe sasa tutaambiwa kulala kwenye nyumba ya bati sio nzuri kwa afya yako.

Tunapoelekea tutaanza kula vyura na nyoka kama nyama maana kila kitu hatar kwa afya
 
kimsingi hata ng'ombe wanao minyoo wa aina hii wenye cyst wanaokaa kwenye nyama/misuli na moyo, ambapo kwa ng'ombe wanaitwa cystercercuss bovis (CB)na kwa nguruwe wanaitwa cystercercus cellulosae (CC). hivyo ngoma droo, wote walao nyama kwa ujumla wanakuwa katika hatari hii. pengine kwa nguruwe inaweza kuwa hatari kwakuwa sijajua machinjio ya nguruwe na ukaguzi wake na inaweza kuwa sio hatari kwakuwa maambukizi hayajafika kwenye eneo la mfugaji husika vilevile sio nyama zote za ng'ombe zinazoliwa zinapita kwenye machinjio pia.
stop worrying and start living.

Nikukumbushe tuu hapa kuwa wale wa kwenye ng'ombe si kama wa nguruwe hivyo hawamdhuru binadmu (siyo zoonotic kwa lugha ya kitaalamu). Hpa ni kuwa makini na nyama iwe imeiva vizuri kabla ya kuliwa
 
ok
Nikukumbushe tuu hapa kuwa wale wa kwenye ng'ombe si kama wa nguruwe hivyo hawamdhuru binadmu (siyo zoonotic kwa lugha ya kitaalamu). Hpa ni kuwa makini na nyama iwe imeiva vizuri kabla ya kuliwa

mkuu unasema CB sio zoonotic lakini wakati huohuo unawaasa wawe makini wakati wa kula nyama kama imeiva vizuri hapa unamaanisha kitu gani?. huu ni ukigeugeu na una-jeopardize taaluma ya udaktari kwa kuongea uwongo wa waziwazi.

kimsingi minyoo hii ya tegu ni Zooanthroponosis, kwa maana kuwa inaathiri binadamu kutokea kwa wanyama tofauti ambayo ni na TB ambapo yenyewe ni anthroponosis ikiathiri wanyama kutokea kwa binadamu. like it or not, that's is the fact.

hydatid cyst ni mnyoo inayosababishwa na mbwa ambayo ni hatari pia kwa binadamu inaweza kuleta kifafa.
 
Hawajaisha na kitimoto kinaendelea kuliwa, hivyo watu lazima wajue namna ya kujikinga na ugonjwa ikiwa ni pamoja na elimu kwa wafugaji kuacha ufugaji huria.
 
Tunashukuru kwa taarifa na ushauri mkuu. Lakini cha msingi juu ya swala la afya zetu kwa ulaji wa nyama ya nguruwe na vyakula vingine ni kuzingatia kanuni bora za upishi na kiasi katika ulaji. kwani vitu vyote ni sumu endapo havitatumika kwa usahihi.
 
Back
Top Bottom