Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Hapa cha muhimu ni namna ya kuindaa kabla ya kuila! Inatakiwa ikaushwe kwenye mafuta mpaka cell zote zife zikiwemo za wadudu mbalimbali; na siyo nguruwe tu nyama zote zinatakiwa zipikwe vizuri ziive hasa!
 
Kifafa ni ugonjwa wa kurithi kama babu alikuwa analamba misamba barabarani na mjukuu lazma atailamba tu achana na kiti moto(EKITI KYOMULILO) We hakuna kiburudisho kama kitimoto mpaka Mizungu ikija Tanzania inashobokea kitimoto ACHA ELIMU ZENU ZA AJABU AJABU DEGREE MBILI AJILA HAKUNA KILA SIKU MAISHA MAGUMU. Acha tufe kwa kitimoto sio maisha magumu
 
kimsingi hata ng'ombe wanao minyoo wa aina hii wenye cyst wanaokaa kwenye nyama/misuli na moyo, ambapo kwa ng'ombe wanaitwa cystercercuss bovis (CB)na kwa nguruwe wanaitwa cystercercus cellulosae (CC). hivyo ngoma droo, wote walao nyama kwa ujumla wanakuwa katika hatari hii. pengine kwa nguruwe inaweza kuwa hatari kwakuwa sijajua machinjio ya nguruwe na ukaguzi wake na inaweza kuwa sio hatari kwakuwa maambukizi hayajafika kwenye eneo la mfugaji husika vilevile sio nyama zote za ng'ombe zinazoliwa zinapita kwenye machinjio pia.
stop worrying and start living.

Tegu wa nguruwe ni hatari zaidi kwa kuwa wakipata chance ya kuingia kwenye ubongo wanaharibu network ya ubongo na madhara yake ndio kifafa na hata kichaa. Tegu wa ng'ombe wanaishia kwenye tumbo na kusababisha maumivu ya tumbo na kuharisha. Wao hawaingii kwenye ubongo. Hiyo ndio tofauti.
 
mie naona blue tu ka vp nyie endeleeni 2 kula mtajuana na mungu kesho
 
Japo topic ya Zamzani, Ina maana hawajaanza kuleta kifafa siyo? Nguruwe kaanza kuliwa lini na ni miaka mingapi na ni wangapi wamepata kifafa? Utafiti unaofanywa Tanzania una mashaka sana sometimes
 
Kila kitu kina madhara hadi mi sitaki kusikia hii kitu inaitwa UTAFITI kwani kuna mtu ambaye hatakufa
 
Hapa hatusemei kifafa cha kurithi, hivyo nacho kipo. Hiki cha tegu wa nguruwe kinashambulia mfumo mkuu wa fahamu ulioko kwenye ubongo
 
sawa mkuu, hata hivyo bado hakuna hatari kwani dawa za minyoo zipo kwenye maduka ya dawa za mifugo, hata ngombe wanadungwa dawa hizi, na zaidi ya yote nguruwe ni white meat ambayo ni nzuri na salama kiafya ukilinganisha na ya ng'ombe ambayo ni red meat.wala red meat wapo kwenye hatari zaidi kuliko white meat
 
Nadhani anazingatia kanuni bora za ufugaji na pia upishi...

Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa

kuwa ni haramu: "Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao" (Walawi 11: 7 – 8).

Agizo hilo limerudiwa katika Kumbukumbu la Shari'ah 14: 7 – 8 na pia Isaya 66: 17.

Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema kuwa hakuja kutangua shari'ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha (Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.
 
Eti huenda.... Narudia ... Huenda wengi tukapata kifafa.... Haya bana, .... Habari mpya...Huenda watembea kwa miguu wote wakagongwa na magari.... Huenda.... Hili neno hili haliwezi kuniachisha kitimoto.

Nini kifafa banaaaaaa....... Wakati kuna watu wanakunywa sumu kabisaaaaaa itakuwa kitimoto banaaaa...??? Wewe ogopa kifafa cha kwenye kitimoto, uje ukipate kichaa cha bangi, unga etc etc
 
Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa

kuwa ni haramu: “
Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao” (Walawi 11: 7 – 8).

Agizo hilo limerudiwa katika Kumbukumbu la Shari’ah 14: 7 – 8 na pia Isaya 66: 17.

Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema
kuwa hakuja kutangua shari’ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha (Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.

Kwa hiyo aliharamisha kwa sababu ya HUENDA TUTAPATA KIFAFA...???
 
Kama ni hivo basi waTanzania wote milioni 44 tutaumwa kifafa

Vipi kuhusu yule kitimoto wa polini maana yeye hujitafutia chakula mwenyewe!

nashawishika kuamini kuwa kitimoto ni mti wenye matunda...

Aaah! Jamani eeh! Huyu nguruwe 'swine', si ameharamishwa katika vitabu vya dini. Kwenye biblia hadi kuraan.

Hawajaisha na kitimoto kinaendelea kuliwa, hivyo watu lazima wajue namna ya kujikinga na ugonjwa ikiwa ni pamoja na elimu kwa wafugaji kuacha ufugaji huria.

Nazungumzia ule wa ng'ombe si zoonotic lakini magonjwa ni mengi. Hivyo ushauri huo ni wa jumla zipo njia nyingi za kujikinga na ugonjwa huo

ok

mkuu unasema CB sio zoonotic lakini wakati huohuo unawaasa wawe makini wakati wa kula nyama kama imeiva vizuri hapa unamaanisha kitu gani?. huu ni ukigeugeu na una-jeopardize taaluma ya udaktari kwa kuongea uwongo wa waziwazi.
kimsingi minyoo hii ya tegu ni Zooanthroponosis, kwa maana kuwa inaathiri binadamu kutokea kwa wanyama tofauti na TB ambapo inaathiri wanyama kutokea kwa binadamu. like it or not, that's is the fact.
hydatid cyst ni mnyoo inayosababishwa na mbwa ambayo ni hatari pia kwa binadamu inaweza kuleta kifafa.

na utamu wake wote ule dah ngoja nijisogeze kwa mangi asee

Nikukumbushe tuu hapa kuwa wale wa kwenye ng'ombe si kama wa nguruwe hivyo hawamdhuru binadmu (siyo zoonotic kwa lugha ya kitaalamu). Hpa ni kuwa makini na nyama iwe imeiva vizuri kabla ya kuliwa

Maisha ya sasa,kila kitu ni hatar kwa afya.Mungu aliyetupa kumilik na kutawala atuepushe na haya matatizo.

Tunapoelekea tutaanza kula vyura na nyoka kama nyama maana kila kitu hatar kwa afya

Ajabu ni kwamba huyo mtafiti ni muuzaji na mlaji mzuri wa kitimoto

kimsingi hata ng'ombe wanao minyoo wa aina hii wenye cyst wanaokaa kwenye nyama/misuli na moyo, ambapo kwa ng'ombe wanaitwa cystercercuss bovis (CB)na kwa nguruwe wanaitwa cystercercus cellulosae (CC). hivyo ngoma droo, wote walao nyama kwa ujumla wanakuwa katika hatari hii. pengine kwa nguruwe inaweza kuwa hatari kwakuwa sijajua machinjio ya nguruwe na ukaguzi wake na inaweza kuwa sio hatari kwakuwa maambukizi hayajafika kwenye eneo la mfugaji husika vilevile sio nyama zote za ng'ombe zinazoliwa zinapita kwenye machinjio pia.
stop worrying and start living.

Aisee ushanitamanisha sasa!

Hizi tafiti siku hizi kila kitu hakifai.Jana tu mwingine kanitumia kwamba tusiweke vyakula vya moto kwenye vyombo/vifaa vya plastik tutapata kansa hujakaa vizuri chumvi sukari sio nzuri mwishowe sasa tutaambiwa kulala kwenye nyumba ya bati sio nzuri kwa afya yako.

Inatisha, thanks for posting though!:A S thumbs_up:

Ngombe Hali kinywesi wala mizoga!!kesi yake tofauti na kiti moto!!kuna tinnea sollium hao ndo minyoo tegu!!yaaani haiteguki ni balaaa!!!!

Madhara ya kula nyama ya Nguruwe/Kitimoto kwa afya yako...

Rosemary Alvarez alijikuta akiwa na maumivu ya kichwa na mkono kukosa nguvu. baada ya kufanyiwa scanning ikaoneka kama ni "brain tumor", pindi alipofanyiwa upasuaji alikutwa na "mnyoo (taenia solium)" akiwa hai unakula brain yake. Chanzo hasa cha mnyoo huo ni kula nyama ya nguruwe ambayo kitaalamu anaprotein nyingi kuliko mnyama yoyote na hivyo kuvutia parasite wengi kwa mnyama huyu . Je ni watanzania wangapi wanapata uangalizi wa kugundua afya zao na wanakula nyama hii kila siku tena inayofugwa katika mazingira si salama?. soma zaidi kwenye link hii hapa chini

Source : ABC News: It's Not a Tumor, It's a Brain Worm

Angalia hapa Mchina huyu pia akitolewa minyoo mingi usoni ambayo pia ilisababishwa na utamaduni wa kula nyama ya nguruwe:

Last edited by a moderator:

hata gari zinauwa lakini hatuachi kuzitumia, hata ndege zinauwa lakini hatuachi kuzitumia, nungwi kule zanzibar wanazama kila mara lakini hadi leo hii watu wametumia usafiri wa majini.... Hatuachi, huyo mchina mmoja hawezi kutufanya sisi 44M tuache kitimoto.
 
Last edited by a moderator:
Eti huenda.... Narudia ... Huenda wengi tukapata kifafa.... Haya bana, .... Habari mpya...Huenda watembea kwa miguu wote wakagongwa na magari.... Huenda.... Hili neno hili haliwezi kuniachisha kitimoto.

Nini kifafa banaaaaaa....... Wakati kuna watu wanakunywa sumu kabisaaaaaa itakuwa kitimoto banaaaa...??? Wewe ogopa kifafa cha kwenye kitimoto, uje ukipate kichaa cha bangi, unga etc etc

Kwa hiyo aliharamisha kwa sababu ya HUENDA TUTAPATA KIFAFA...???

1232629.jpg
[I

Katika viumbe vinavoliwa na binadamu ambavyo Mwenyezi Mungu (swt) ameviharamisha ni Nguruwe. Japokuwa nyama ya Nguruwe inaliwa kwa kiwango kikubwa sana katika nchi za Ulaya, Amerika, Asia na baadhi ya nchi za Afrika. Bado Nguruwe ataendelea kuwa ni mnyama aliye najisi kubwa kabisa. Hasa katika jamii za waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) kwenye Qur'an anasema hivi:

Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na Nyama ya Nguruwe,
Na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
Qur'an 5:3

Kwa nini basi Nguruwe awe ni haramu kwa waislamu na kwa baadhi ya watu wengi?
Kwa waislamu jibu lake ni rahisi mno. Kwani hiyo ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Na waislamu hatuna budi kuitekeleza kwa hali na mali.
Lakini je, ukiamua kuila kwa sababu ni nyama inayo onekana kuwa imenona sana, ili uweze kujipatia afya iliyo bora. Je unafikiri takuwa umefaidika? Jibu lake ni kuwa utakuwa ni mwenye kuikharifu amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa kukataa kuitekeleza amri yake, kwa hali iyo atakuadhibu hapa duniani na kesho akhera.
Pili utakuwa ni mwenye kujitia hasara kubwa katika afya yako. Kwani katika uislamu kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu (swt) ametuamrisha tulitekeleze au tusilitekeleze basi linafaida kimwili na kiroho.
Wataalamu wa Lishe baada ya kufanya uchunguzi wa muda mrefu kuhusu nyama za aina mbalimbali, ikiwemo nyama ya Nguruwe, wakaja kugundua kuwa nyama ya nguruwe si nzuri kabisa kuitumia. Kwani imeonyesha kuwa inaongoza kuwa na vijidudu vya maradhi yasiyo tibika. Japokuwa nyama za Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo na nyinginezo zimeonekana kuwa na vijidudu kiasi Lakini vijidudu hivyo vya wanyama wengine wanaoliwa kihalali vinaweza kutibika bila matatizo yoyote, kulinganisha na nguruwe. Kwani nyama ya nguruwe hata ukiichoma na kuwa majivu bado baadhi ya vijidudu havitakufa kabisa. Kwani baadhi ya vijidudu hujitengenezea kinga au Cyst. Cyst ni kinga ambayo baadhi ya vijidudu hujitengenezea ili visidhurike.

MARADHI NA VIJIDUDU KTK NGURUWE:
Nguruwe ni chanzo kikubwa sana cha maradhi ya aina mbalimbali yasiyo tibika, nguruwe ana vijidudu vya maradhi aina zaidi ya 20,000. Hebu na tuangalie baadhi tu ya vijidudu ambavyo vinapatikana kwenye nyama ya nguruwe.

Protozoan Ciliate. (Balantidium Coli):
Hiki ni kijidudu chenye chembe hai moja, na kinaishi katika utumbo mpana wa nguruwe. Kijidudu hiki licha ya kusambazwa kwa kupitia ulaji wa nyama ya nguruwe pia husambazwa kupitia kinyesi chake. Pale kinapotumika kama mbolea. Mdudu huyu anasababisha maradhi ya kuhara damu. Maradhi haya yanapatikana sana katika nchi zile ambazo watu wana mahusiano makubwa na nguruwe.

Trichinella Spiralis (Trichina):
Vijidudu hivi hukaa katika misuli ya nyama ya nguruwe, na pale inapoliwa husababisha udhaifu mkubwa sana kwenye mwili wa binadamu, kwa sababu si mkazi asilia katika mwili wa binadamu. Mdudu huyu anauwezo wa kuishi hadi kufikia miaka arobaini (40) akiwa mwilini mwa binadamu. Hupendelea kukaa kwenye utumbo mdogo wa binadamu, baadae ujipenyeza na kuingia katika mzunguko wa damu na kusambaa mwili mzima na kushambulia maeneo mbalimbali ya mwili wa binadamu. Mfano hushambulia mishipa ya damu na husababisha kuvuja kwa damu, ndani kwa ndani (Internal Bleeding), hushambulia kioo cha jicho (Retina) na kusababisha upofu (Blindness), hushambulia mapafu na mafuta yaliyoko kwenye mifupa, na misuri ya moyo, pia husababisha Baridi yabisi (rheumatism), kupooza kwa misuri (Muscular Paralysis), ugonjwa unao sababisha upungufu wa damu mwilini yaani saratani ya damu (Anaemia).

Taenia solium (Pork tapeworm): Tegu. Tegu ni minyoo anayosababisha mwili kukosa lishe na kupelekea kupata utapia mlo, na pia hushambulia sana ini, husababisha kuhara (Diarrhoea), uleta ugonjwa wa uzuni (Melancholia) na kushindwa kwa usagaji wa chakula (Digestive Disturbances). Na kuharibu uti wa mgongo (Spinal cord).

Roundworms: Kuna aina zipatazo 12,000 za Roundworm, wakiwemo hookworms au Filarial ambao uleta maradhi ya matende. Pia husababisha maradhi ya homa ya Manjano (Jaundice) kutosagwa vizuri kwa chakula (Digestive Disturbances), kuziba kwa kidole tumbo (Appendicitis).

Hookworms:
Zaidi kusababisha maradhi ya saratani ya damu (Anaemia) na magonjwa ya homa ya matumbo yaani kuharisha (Typhoid), pia husababisha utapia mlo, na maradhi ya moyo (Heart Failure), safura, Mtindio wa ubongo au utaahira (Mentally Retarded). Na hali ya kutojali (Apathy). Pamoja na kifua kikuu TB (Tuberculosis)

Faciolopsis Buski: Ni vimelea ambavyo hukaa katika utumbo mdogo wa nguruwe pia husababisha kuharisha damu kutosagwa vizuri kwa chakula (Digestive Disturbances).

Paragonimus: Ni kimelea kinacho ishi kwenye mapafu ya nguruwe na kinasababisha maradhi ya Pneumonia na kuvuja kwa damu katika mapafu.

Clonorchis Sinesis:
Husababisha magonjwa mabaya sana ya kuvimba Ini na kifua kuchoka, ulegevu na kupata ugonjwa wa uzuni (ulio kama aina ya wazimu hivi).

Erysipelothrix: Mdudu huyu husababisha maradhi yanayojulikana kwa jina la Erysipelas, ugonjwa huu husababisha kuharibika kwa ngozi ya mwili, kuwa na mabaka mabaka yakiambatana na homa kali. Vile vile nyama ya nguruwe husababisha ugonjwa wa kutoa mimba unaoitwa Brucellosis (Malta fever).

The pig is full of pus: -
Pus ni majimaji ya njano (yanayo fanana na Usaha) ambao husababishwa na kuharibika kwa tishu na kufa kwa chembe chembe nyeupe za damu (white blood cell), na hii husababishwa na aina ya bacteria, protozoan pamoja na kufu (fungal) na uharibu ngozi, fizi, mifupa, na baadhi ya viungo (Organs) kama vile ini, mapavu, na ubongo. Maeneo yalioathirika uvimba na kuwa mekundu, na husababisha maumivu makali na kusababisha joto la mwili kupanda, na kumsababishia muathirika kupata homa kali. Na hii huweza kumsababisha kifo kwa mgonjwa kama hatawahi kutibiwa.
Vile vile nguruwe husababisha maradhi mengi yanayo ambukiza, yanayotokana na bakteria na virusi (Bacterial and viruses Diseases). Kama vile kifua kikuu (Tuberculosis), kipindupindu (Cholera), pepopunda (Lockjaw), kuoza kwa sehemu za mwili (Gangrene), ukoma (Leplosy), na ugonjwa wa Tauni (Plague). Kaswende (Syphilis), ugonjwa wa donda koo (Diphtheria)
Kwa bahati mbaya sana matibabu ya magonjwa yanayotokana na nguruwe hayajapatiwa dawa ya kuyatibu au kuponyesha kabisa, isipokuwa ni kutuliza tu kwa muda. Dawa hapa ni kuacha kutumia nyama ya nguruwe.

TABIA YA BINADAMU NA ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE

Binadamu ameumbwa katika hali ya kimwili, kiakili na kiroho. Makazi ya akili ni katika ubongo. Ubongo ambao hupata lishe na chembe hai (cell) mpya kutokana na vyakula tunavyokula. Vyakula tunavyo kula husaidia sana kuzalisha chembe

hai mpya katika mwili wa mwanadamu ili kuchukua nafasi ya zile zilizo kufa. Cell ambazo baadhi yake ndizo hizo zinazo tengeneza cell za ubongo. Ambamo humo kwenye ubongo ndimo kunapopatikana Akili. Unapokula nyama ya ngururwe

jua kuwa mafuta yake huwa hayatumiki mwilini, kinachofanywa na mwili wa binadamu ni kuyarundika mafuta hayo chini ya ngozi, na kwenye mishipa ya damu, na kwenye chemba za moyo na kwenye ini. Na hii baadaye husababisha ongezeko

la mwili kupita kiasi, kuwa na wasiwasi, kutojiamini, maradhi ya moyo, na mwili kukosa nguvu. Na kutoweza baadhi ya viungo yaani ogani kutofanya kazi vizuri. Pia protini inayopatikana kutokana na nyama ya nguruwe ndio inayo kwenda

kurutubisha DNA zako na hapo ndipo unapoanza kurithi tabia na mienendo ya nguruwe. Kwani katika DNA ndimo kunapo patikana kila kitu kinacho muhusu binadamu. Kuanzia tabia, umbo lake na kila kitu kuhusu binadamu. Na sasa

hebu fikiria kuwa DNA inakwendwa kubadilishwa kulingana na unachokula na chakula chenyewe ni nguruwe je unafikiria itakuwaje na sisi sote tunakuwa hivi tulivyo, kulingana na tunavyokula.

Tufahamu kuwa chakula kilicho safi na halali, na kilichopatikana kwa kheri na kuliwa kwa mawazo ya amani ujenga athari njema katika mwili na akili ya binadamu. Lakini chakula kichafu au kiliwacho katika machafuko ya kiroho hudhuru mwili na akili.

Nguruwe japokuwa anapendwa kuliwa na watu wengi, bado anakuwa ni alama ya uchafu, ufisadi, uasherati na ulafi wa kupapia visivyo halali. Nguruwe amekuwa ni chanzo cha uharibifu wa tabia za watu walio wengi. Watu wengi huathiriwa

polepole na tabia za nguruwe pale wanapokula nyama hii bila ya wao kujua. Mambo ya uasherati ukosefu wa adabu watu kukosa haya na huruma ni vitu vya kawaida sana katika jamii inayokula nguruwe, na unyoofu wa maadili huwa ni kama

jambo lisilowezekana au lililopitwa na wakati. Watu huwa na tabia mbaya za ubinafsi na ukatili usio na sababu ni jambo la kawaida mno. Hebu leo hii Angalia vichwa vya habari vya magazeti mengi hapa nchini mengi yao habari wanazopenda

kuziandika ni zile za ngono na za waendao uchi. Leo hii zinaa ni jambo la kawaida sana mfano tendo la kubaka linaonekana ni sawa na kumpiga mtu kofi la shavu tu, nao wanadai waonewe huruma kwani jambo walilolifanya ni la kawaida tu halihitaji adhabu kubwa. Huu ni msiba mkubwa katika jamii zetu hizi. Mambo ya kubadilishana wake, watu

kuishi na vimada kuingiliana kimwili kwa makundi (group sex), kutembea uchi (Nudism) na kadhalika haya yote yanapatikana pale tu ulaji huu wa nyama ya nguruwe unaonekana kama ni jambo la kawaida katika jamii. Hebu angalia

nchi za Amerika na Ulaya zilivyo haribika kitabia. Watu wake wengi si wastaarabu hata kidogo, ukilinganisha na nchi ambazo hakuna ulaji wa nyama za nguruwe. Sisemi kuwa katika nchi ambazo ulaji wa nyama za ngurwe ni mdogo au hakuna kabisa kuwa hakuna uasherati la. Sisemi hivyo ila katika nchi ambazo ulaji wa nyama hii ni mdogo au hakuna

kabisa matendo ya uzinzi na ukahaba ni matendo ya aibu sana kwa wana jamii, tofauti na nchi zinazokula nyama ya nguruwe. Kwani katika nchi hizo za ulaji wa nyama hii kwa wingi tendo la kucheza au kutembea uchi ni kitu cha kawaida na huitwa kuwa ni sanaa, na wala si utovu wa maadili. Kwani matendo hayo ya kutembea uchi yanapata baraka za wanajamii na serikali kwa ujumla.

Mambo haya yanapozidi na kuendela na kuonekana ni mambo ya kawaida katika jamii. kidogokidogo jamii huharibika na kurithisha tabia hizi chafu hasa kwa watoto wanaochipukia. Na kwa wale wanaopenda kuiga kila jambo linalopigiwa debe na vyombo vya habari. Kwani wakubwa wao tayari wamekwsha athirika na tabia hizi za uasherati na uzinzi.Ndugu

msomaji kwa ili unaweza kufanya utafiti mdogo tu, kwa kulinganisha maeneo au watu wanaokula nyama ya nguruwe na wale wanao pendelea kutokula nyama ya nguruwe. Hususani watu wanokula samaki au mboga za majani (vegetarian). Au walaji wa nyama za ng'ombe na mbuzi.
 
Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa

kuwa ni haramu: "
Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao" (Walawi 11: 7 – 8).

Agizo hilo limerudiwa katika Kumbukumbu la Shari'ah 14: 7 – 8 na pia Isaya 66: 17.

Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema
kuwa hakuja kutangua shari'ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha (Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.
Mkuu hapa naona ni kama vile unapiga upepo rangi, utapoteza muda wako tu. Piga ua, walaji wa Noah katu hawatoacha kumla huyo mnyama. Labda waambiwe wakila watageuka matoashi may be ndio wataacha kumla Noah.
Ushauri wangu: Wewe waache tu waendelee kumla noah
 
kwenye matumbo yetu kuna mnyoo kamba (tape worm) hafi hadi siku utakayokufa..sembuse k'moto?
 
Kuleni tu Mbuzi wa Kikatoliki mukiumwa Ma-Daktari

wapate kuwatibu na kufaidika bora Wanaokula nyama ya Nguruwe wakiumwa wengi

ndio bora tupate kuwatibu . Waswahili wana sema Vifo vya wengi ni Harusi . Kuna

Ukimwi lakini watu hawachi Mambo ya Zinaa itakuwa kula Nyama ya Nguruwe? Kula

tu kaka kitomoto Faida yake utakuja kuijuwa tu muda sio mrefu.

kwenye matumbo yetu kuna mnyoo kamba (tape worm) hafi hadi siku utakayokufa..sembuse k'moto?

NYAMA YA NGURUWE YAPIGWA MARUFUKU MJINI IRINGA, NI KWASABABU YA HOMA YA NGURUWE

Na Solomon Lekui

Picha hii ya maktaba yetu, inamuonesha Profesa Peter Msolla (Mbunge wa Jimbo la Kilolo) akiangalia jinsi wafanyabishara wa nyama ya nguruwe mjini hapa wanavyofanya biashara yao

WAPENZI wa ile nyama ya nguruwe maarufu kama Kitimoto inayoaminika kuongeza kinga za mwili kwa watu walioshambuliwa na maambukizi ya Ukimwi kama utaila sana, imepigwa marufuku kuuzwa mjini Iringa kuanzia leo.

Hatua hiyo itakayowaacha mamia ya wafanyabiashara wake wakiathirika kiuchumi, imekuja baada ya ugonjwa wa homa ya nguruwe kuripotiwa kuingia mjini hapa.

Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Augustino Nyenza amesema kuanzia leo machinjio zote za nguruwe zinatakiwa kufungwa kwasababu ya tatizo hilo.

Amesema tangu Mei 20 mpaka jana, ugonjwa huo ulikuwa umekwishauwa nguruwe 44 katika kata ya Mkwawa, huku uchunguzi uliofanywa ukioneshawa wengine wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huo.

Alisema wakati halmashauri hiyo ikitangaza kuchinja na kuuza nyama ya nguruwe, wananchi wanatakiwa kusubiri karantini kubwa ya wilaya.

"Tunaendelea kufanya mawasiliano kuhusu hali ya ugonjwa mjini Iringa ili karantini iweze kutangazwa rasmi," alisema.

Alisema karantini hiyo itazuia kuingiza, kutoa au kuuza nyama ya nguruwe mjini hapa mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo baada ya ugonjwa huo kudhibitiwa.

Hii ni mara ya pili kwa ugonjwa huo wa nguruwe kuingia mjini hapa katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi mitatu iliyopita.

Mapema mwezi Machi mwaka jana, ugonjwa huo uliingia mkoani Iringa ukitokea mkoa jirani wa Mbeya ambako pia uliuwa idadi kubwa ya nguruwe.

Ugonjwa huo uliingia mkoani Mbeya ukitokea katika wilaya ya Kalonga nchini Malawi na baadae kuingia mkoani Iringa kwa kuanzia wilaya Ludewa ulikouwa nguruwe 145 kati ya 716 katika kijiji cha Lupingu na Ntumbali.

Baada ya kutangazwa kwa karantini, timu ya madaktari wa mifugo wa ofisi ya kanda na halmashauri ya manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini waliwauwa kwa kuwachoma

moto nguruwe 99 waliokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh Milioni 8.5, waliokamatwa wakisafirishwa kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililokuwa la kusikitisha, nguruwe hao waliosafirishwa kwa kutumia gari la taka la manispaa ya Iringa na kupelekwa katika dampo la manispaa hiyo,

walitumbukizwa wakiwa wazima kwenye shimo dogo lililokuwa na moto mkubwa uliowashwa kwa kutumia miti na matairi chakavu na baadaye kufa. Chanzo.
http://tumainihabari.blogspot.com.tr/2012/06/nyama-ya-nguruwe-yapigwa-marufuku-mjini.html
 
Back
Top Bottom