Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Kwanza makinika nami vizuri kuhusu hizi picture hapa chini:-

View attachment 587398

View attachment 587399

View attachment 587400

View attachment 587401

View attachment 587402



Sasa twende kwenye upotoshaji wa SUA kuhusu huyu mdudu:-

Nchini Tanzania nyama ya nguruwe ni maarufu katika maeneo mbali mbali ya starehe na imepewa majina mengi kama vile mkuu wa meza, kiti moto na mengineyo mengi.

Hata hivyo utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha sokoine( SUA) umebaini kuwa walaji wa nyama ya nguruwe wako katika hatari ya kupata magonjwa kama vile kifafa kutokana na mnyoo Tegu uliopo kwenye nyama ya nguruwe.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezungumza na mtafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama Dkt. Boa Mathias Emanuel kutoka chuo kikuu cha SUA na kwanza amemuuliza ueneaji wa ugonjwa huu.


SUA wanafanya makusudi sana.
Kilichopotoshwa ni nini sasa?Mbona hukueleza ukweli unaoujua kuhusu kitimoto?
 
Mi ningekuwa nishapata zaman maana ni ngumu siku kupita bila kupata walau nusu kilo na ndizi mbili, na sitaacha kama ni kufa acha nife tu, kwan wale waliokutwa wanaelea baharini kwenye viroba nao walikula KITIMOTO??

Sent using Jamii Forums mobile app
KULA TU KWA UKAIDI WAKO LAKINI IMEKATAZWA
 
Mwaka wa ishirini nakula tena sanaaaa, sijaumwa na sitaumwa maana hao minyoo siyo rahisi kuwapata kwanza tegu kwa ng'ombe unapata. Tens usinikumbshe rift valley fever ilivyoua wamaasai ,nguruwe is safe by far
 
matokeo ya utafiti huu ni sawa na mtafiti kufanya utafiti wa kujua kama ndani ya binduki ya mlinzi kuna risa
Mkuu utakapo wewe umwa na maradhi ndio furaha ya Ma-Daktari kupata pesa kwa sababu utakapo shikw ana amradhi utakimbilia Hospitali na huko Hospitali utalipa pesa sasa wewe kula kitomoto faida yake utaiona mwisho mwake.
 

Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa kuwa ni haramu:

"
Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama
yao wala msiguse mizoga yao" (Walawi 11: 7 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 8).
Agizo hilo limerudiwa katika

Kumbukumbu la Shari'ah 14: 7 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 8 na pia Isaya 66: 17. Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema
kuwa

hakuja kutangua shari'ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha
(Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni

kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.
Hata hivyo, Nabii Paulo ndiye aliyekuja akaenda kinyume na

shari'ah hiyo kwa kutoa agizo kwa barua aliyowaandikia Warumi:
"Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa

sababu ya ubishi juu ya chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya

aanguke katika dhambi"
(Waroma 14: 20).
Pia, "Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba

hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake"
(Waroma 14: 14).
Paulo amesema tena kuwa kila kitu

alichoumba Mungu ni chema wala hakuna kinachohitaji kukataliwa
(1 Timetheo 4: 3 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 5). Na Mwenyeezi

Mungu ndie anayejuwa zaidi.@
FALSAFA
Kwa hiyo nguruwe ni kitu chema au haramu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
utafiti huo si wa kweli kwa sababu nguruwe wana vimelea wa magonjwa wengi sana na hasa retroviruses ambao hawadhuriki hata baada ya kuchemsha/kukaanga/kupika nyama yake.Wengi wa hawa viruses wanaadhiri ubongo. kwa maana hiyo akili unayopigia chapuo itatoka wapi?
Mnadanganyana sana mkuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa unalialia nini? Ulitaka huo utafiti ufanywe na Mzumbe ndo uamini? Unamjua huyo tegu anayezungimziwa na jinsi anavyoweza kumwingia binadamu? Hebu wacha porojo zako hapa!
 
Mkuu utakapo wewe umwa na maradhi ndio furaha ya Ma-Daktari kupata pesa kwa sababu utakapo shikw ana amradhi utakimbilia Hospitali na huko Hospitali utalipa pesa sasa wewe kula kitomoto faida yake utaiona mwisho mwake.
nitajie mnyama anayeliwa na binadamu ambaye hawezi kuwa na deadly microbes au parasite wanaosababisha maafa kwa binadamu:
kuku?
bata?
ng'ombe?
ufahamu tu kuwa ni nguruwe tu ambaye yuko under poor managerial practice anayekuwa na hicho (cysts ) kinachoogopwa, vipi CB, TB, RVF, ANTHRAX kwa ng'ombe? vipi Salmonella kwa kuku?
 
Lakini wamesema asipoiva Vizuri ndo unaweza pata madhara hayo hasa wale wanaopendelea kuchoma ila akikaangwa/kupikwa Vizuri hakuna shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena wameponda sana ya kuchoma, wanasema ina minyooo ambayo haipati motomoto wa kutosha bora kuchemsha na kukaaanga! mie hata wakimdisi simuachi bora tegu ziniue potelea mbali!
Ni bora hao tegu kuliko kipindupindu,alafu mbona hawatupi takwimu sahihi zinazoonyesha idadi ya watu waliopata minyoo ya tegu kwa kula nyama ya nguruwe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tegu anaweza kupatikana kwenye wanyama wote hata mbwa! Isitoshe nguruwe hakuanza kuliwa leo bali toka kabla ya Yesu maanake alkwakuta na walikuwa wakiliwa tena kwa kuchomwa!
Niulizieni kwa huyo dr kuwa, ulaya, asia na hata america ni walaji wazuri sana wa kitoweo hiki na hakuna wagojwa wa kifafa walioeipotiwa kule. Ni kwanini walaji wa hapa bongo ndio wawe wahadhirika tu? Dr kasome tena sisi walaji hatudanganyiki na rudisha fedha ulizoomba kufanyia utafiti huu.
 
Nasoma hii taarifa..nikimaliza kusoma comments zote naenda kushushia na mkuu wa meza roast na Coca Cola baridi..[emoji2]
 
kwani ambao wametumia kipindi kirefu cha maisha yao wameathirika?more evidence should be applied
 
Back
Top Bottom