Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Nimecheka leo Dom kwa Tv naona mtu anakimbia kwa speed ya hatari yuko mbele krb na gari lile jeusi na yupo serious. Nikasema kweli tunatofautiana vipaumbele

When emotions (some people term it a weakness) take over your sensibility, the body just reacts! It’s all in order!

Haikwepeki! Ipo kwa viumbe wengi sana (kama sio wote) inapotokea furaha, majonzi, hatari, tukio kubwa na la pamoja lenye kugusa hisia za ndani/maumbile (emotions).
 
Niliona video watu wanesongamana balaa na anayechukua anasema. "Ona watu wanakufa". Vyombo vya ulinzi na usalama haviwezi kukwepa lawama kwenye hili suala.
Halafu kuna lijinga limoja humu likaandika kwa kutumia makalio likasema habari hiyo imetengenezwa sio ya kweli.Limejionea lenyewe jinsi ilivyotengenezwa akili yake sawasawa na ya pimbi.
 
RATIBA YA ZOEZI LA KUAGA MWILI HAYATI DAKTARI JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MKOA WA KWANZA

1. Milango ya Uwanja wa CCM Kirumba itakuwa wazi kuanzia saa 10 Alfajiri.
2. Mwili kuwasili uwanja wa ndege saa 12:00 Asubuhi.
3. Msafara kuelekea uwanja wa CCM Kirumba utakapofika kona ya Bwiru mtaa wa Selemani Nassoro Msafara utasimama jirani na Nyumba yake alipokuwa anaishi akiwa Mkoani Mwanza Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wanachama wa CCM na wananchi tujitokeze kwa wingi mkiwa mmevaa sare.
4. Ibada na shughuli za kuaga Uwanjani.

NB:
Mwili utapitishwa katika barabara zifuatazo kwa ajili ya wananchi kupata fursa zaidi ya kuaga mwili wa mpendwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

ILEMELA.
Barabara ya...
1. Nyamanoro
2. Pasiansi
3. Kiloleli
4. Montessori
5. Maduka 9
6. Nyasaka
7. Buzuruga


NYAMAGANA-NYERERE ROAD.
1. Mabatini
2. Mlango Mmoja
3. Nata
4. Mnara wa Nyerere
5. Mjini Kati

NYAMAGANA-KENYATTA ROAD
1. CCM Mkoa
2. BP
3. Pepsi
4. Voil
5. Mkuyuni
6. Nyegezi
7. Mkolani
8. Buhongwa

NB:
Mwili utaendelea kupitishwa hadi Usagara kuelekea Kigongo Ferry hadi Sengerema kuelekea Geita.

Muhimu kuwaambia wanachama wa CCM na wananchi wote ambao hawatapata nafasi ya kuja uwanja wa CCM Kirumba kujitokeza na kujipanga barabarani wanachama wa CCM tuhakikishe tumevaa sare.


IMETOLEWA NA CHIEF DENNIS KANKONO KATIBU WA SIASA NA UENEZI WA CCM WILAYA YA ILEMELA
 
Mimi nilishangaa familia moja imepoteza watu wanne mke watoto na msaidizi wa nyumbani, inakuaje familia nzima mnaenda kwenye shughuli moja wote ndio kuna baadhi ya maeneo watu wa familia moja ni mwiko kusafiri sehemu moja wote maaana laweza kutokea ajali kizazi chote kikapotea.
 
Mimi nilishangaa familia moja imepoteza watu wanne mke watoto na msaidizi wa nyumbani, inakuaje familia nzima mnaenda kwenye shughuli moja wote ndio kuna baadhi ya maeneo watu wa familia moja ni mwiko kusafiri sehemu moja wote maaana laweza kutokea ajali kizazi chote kikapotea.
Mungu awalaze mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom