Habari Mnayo! Simba SC yaiadhibu kisawasawa KMKM

Habari Mnayo! Simba SC yaiadhibu kisawasawa KMKM

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Leo mabingwa watarajiwa wa VPL msimu wa 2015/2016 wamehitimisha ziara yao kisiwani Unguja kwa kuiadhibu ipasavyo KMKM mbele ya refa wao, uwanja wao pia mashabiki wao goli 3-2.

KMKM ndo walianza Mpira kwa kasi na kujipatia goli 2 za chap chap katika kipindi cha kwanza. Baadae Simba ilitulia, na Hamis Kiiza akatupia goli moja kabla ya half time.

Kama kawaida kipindi cha pili.. lile soka la kasi sana lililojaa pasi fupi fupi lilianza kuoneshwa.. ambalo liliwaduwaza mashabiki na wachezaji wa KMKM.. Ibrahimu Ajibu a.k.a Hatrick Master alitupia kambani goli mbili (brace) za chap chap, na kukamilisha ushindi wa Simba SC.. Shukrani kubwa ziwaendee mabeki na kipa wa KMKM, maana dazani leo ilikua inawahusu.

Baadhi ya matukio ya leo;

View attachment 273829

Kama kawaida, mabeki wa Zenji Rugby ndo mchezo wao.. Hapa Musa Hassan Mgosi alikikusanya hiki kijiji.

View attachment 273830

Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Ajibu baada ya kufunga goli lake la pili.. Mchezaji huyu Deo Corleone na Edo Kumwembe wanamuita mvivu.. Sasa najiuliza hao kina Busungu, Ngoma n.k ambao si wavivu hua wanafunga goli ngapi???!!

NEXT VICTIM: AFC Leopards

STADIUM: Taifa Stadium

DAY: 08/08/2015

More pics to come..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom