Nafikiri mnapogoma lazima mjipange vyema. Mimi ninafanya utafiti wa crisis managemnet in higher learning institutions. Kwa miakamitano sasa UDSM hakuna mgomo hata mmoja uliofanikiwa na kila mwaka kuna mmgomo kama siyo mmoja ni miwili. Kisa ni ni ni? Hakuna mipango thabiti ya migomo hiyo. Kwanza lazima ujue unagomea nini? (hapa uwe specific kama ni mikopo kwa waliokosa uwe na data kamili ya ambao hawajaweza kujipia kabisa kati ya hao 14,000/= na pia mnataka wawe means tested kivipi?), Kwa faida ya nani?(ya unao watetea? ya kwako kwa mgongo ya hao mnao watetea? "isije kuwa wale waosema kina fulani walifanya hivi au vile leo ni wabunge" kama mmoja wa viongozi wa kunji la UDSm alivyosema pale rev square, ni kwa faida ya kundi au makundi fulani? ni ya shinikizo jingine zaidi ya lengo linalotamkwa?), Upepo wa kusikiliza ukoje huko kwa tunaowashinikiza? wako tayari kutoa pesa kwa shinikizo la migomo? wanahusisha migomo yoyote na maswala ya kisiasa au kidini au kikabila?), Je kuna mtu au kundi la watu ambalo limeshaanza mchakato wa madai husika(ni kwa staili gani na imefanikiwa au haijafanikiwa kwa kiwangoa gani?), Je mikakati yenu imepangikaje(hakuna double face "wenye nia tofauti na inayokusudiwa", haiingiliani na mipango mingine ambayo imeshaanza? mipango ya wawli haiwezi kuwa kikwazo?). Mwisho lazima ujiulize kama mkakati mliousuka ukishindikana nini kitafuata?
Ushauri wangu ni huu: (siyo lazima ufuatwe ila naangalia uzoefu na utafiti ambao bado naendelea kuufanya.
Ni vyema kushinikiza wabunge kujadili swala husika na kufikia maafikiano ya nini hasa kifanyike ili hata kama ni kuandika barua ifuate utaratibu unaokubaliwa kama taarifa za awali ili baadae isisemwe hawa ni wahuni kwa kuwa hawajaleta taarifa yoyote kuhusu madai yao. Barua itaandikwa na katibu wa bunge na kupata signature za wabunge wote badala ya kusainiwa kwa jina la "MWANAHARAKATI" bila kueleza hata mwanaharakati wa wapi!!! lazima tujue hata wanaopigania haki za mashoga ni wanaharakati za ushoga, wanaharakati za waabudu shetani, wanaharakati za kisiasa n.k. pili lazimabaada ya barua kwenda kwa mamlaka husika na kutopata majibu iandikwe nyingine na mwisho ya tatu huku mkimobilize mabunge ya vyuo vingine kufanya hivyo ili mwisho wa siku isionekane ni chuo fulani tu!! Ikifikia hapo kila mtu atakua anajua nini kinachoendelea na watu wa usalama na wanahabari wengine watapeleka ujumbe sahihi kwa kadiri iwezekanavyo. Mwisho mabunge ya vyuo vyote yatapitisha mgomo wa kutoingia madarasani bila propaganda zinazotumiwa na wanasiasa kwa kusaini petition kubariki mgomo husika. Kwa kutumia rev square hata kwa ugomvi wa kisiasa ndani ya association za wanafunzi hakuna atakaye wasikiliza. Enzi za kina kina samweli sita, kina bashiru ali, kina kitilla mkumbo, kina mkenda ukisikia rev square ni bunge au rais wa DAURSO anaongea kwa jambo lenye mvuto na kama ni mgomo hata Rais wa Nchi anatoa majibu au mkwara muda mfupi baada ya rev. Waongoza migomo na maandamano wa sasa wamepotelea kusikojulikana walikua wanang'ata na kupuliza wakigoma leo chuo kikifungwa ndiyo wakwanza kuandika barua za kuomba kurudi kwa uapa kuwa hawatahusika na migomo tena labda niulize watu wengi wanasififia watu kadhaa waligoma na kufukuzwa miaka kadhaa iliyopita bila kujiuliza kina machibya wako wapi nani aligoma warudishwe? UDOM watu mia kadhaa nani anataarifa zao? ana hata amedhiriki kufungua kesi kushinikiza warudi? Ninachomaanisha hapa ni kwamba ukiendesha migomo kiuanharakati usiojulikana uanaharakati upi mwishowe utabaki na begi lako kama ulivyoingia chuo na hutakua umemsaidia uliyetamani kumsaidia.
Tujipange upya, vyema, kuiokomboa nchi kutoka mikononi mwa walafi wachache au tuanze mpango wa Haraambeee ya kenya ile 7500 tunayopewa ya chakula tuimege kama 2500 tusaidie waliokosa mikopo kabisa ili angalau wapate ada,(2500x100000=250,000,000/=) itawaokoa wengi sana. au tuanzishe scholaship funds kama za baadhi ya wabunge kama godbless lema na wengine wengi kupitia mfuko wa wabunge inayowasomesha wanafunzi wa shule za kata.
Mwisho ushauri kwa serikali. 1. TCU iondolewe mamlaka ya kudahi wanafunzi kama inavyota kwanza shughuli ya kudahili siyo kazi yake ni kazi ya vyuo iache tamaa ya kupata pesa za admission. Kazi hiyo viachiwe vyuo vya elimu ya juu ili mwanafunzi aamue aende wapi vyu vipeleke majina TCU kwaajili ya cceditation tu. 2. Serikali itoe elimu ya umma kuhusu mikopo ya elimu ya juu ili ieleweke kuwa ni mkopo na siyo hisani. 3. Serikali ishinikize vyuo viwe na ushirikiano wa karibu na TCU na Bodi ya mikopo ili wanafunzi wanodahiliwa wapate mikopo stahiki badala ya serikali kuangalia idadi ya wanafunzi kuwa kubwa badala ya kuangalia pia adha wanayoipata wazazi na wanafunzi wanao pata mikopo nusu au waliokosa kabisa ha hapa kigezo kiwe ufaulu mkubwa na siyo uwezo wa mtu kifedha maana ni ngumu kuutambua(hili nasema kwa kuwa kila mtu ni maskini anposikia fedha inatoka serikalini hata mkulima mwenye ng'ombe 100 shamba hekari 50 na zaid atajiita mkulima mchanga) na wale watakaokosa basi waombe vyuo kama private candidates kulingana na uwezo wao.
Naomba kupewa michango ya ziada na kukosolewa ili ninacho kifanya kiwe strong na kwaajili ya kuliendeleza taifa na kuondokana na migogoro isiyo ya msingi vyuoni.