Habari na historia nyngine ya vita vya majimaji sehemu ya kwanza

soskeneth

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2016
Posts
583
Reaction score
235
Katika kusimulia historia ya Tanzania huwezi kuacha kusimulia historia ya vita vya Maji Maji ambavyo vilipata kutokea miaka ya 1900-1910. Vita hivi vilikuwa vinahusisha Watanganyika (watanzania) waliokuwa wanatoka kwenye makabila mbalimbali yaliopatikana maeneo ya kusini mwa Tanzania dhidi ya Wajerumani.

Malengo ya vita hivi yalikuwa mengi sana lakini kubwa ni kupinga utawala wa kikoloni ambao ulianza mnamo miaka ya 1890. Na maandiko mengi yanasema kuwa katika vita hivi Watanganyika walishindwa na Wajerumani walishinda na kupata nafasi ya kutawala Tanganyika.

Hakika habari za vita hivi vya Maji Maji zimeandikwa sana na wanahistoria wengi. Na tunafahamu mengi juu ya vita hivi licha ya kwamba kuna mengi yamefichwa na wengi hatuyafahamu. Ukweli ni kwamba Habari na historia ya vita hivi zimeandikwa kwa kuegemea mitazamo mingi sana, kwa mfano kuna mtazamo ya imani ya kikristo,

kuna mtazamo wa kisiasa, kuna mtazamo wa kijamii na pia kuna mtazamo wa imani ya kiislamu. Lakini pia asilimia kubwa ya watu wanaofahamu historia ya vita hivi wanafahamu katika mtazamo wa kijamii na kisiasa ambapo ndio hata shuleni hujifunza hivyo. hivyo kwa leo tutajadili kwa uchache habari na historia ya vita hivi kwa upande wa imani ya dini ya kiislamu.

Yaani tutajadili kuona jinsi vita hivi vya Maji Maji vina dhana gani kwenye imani ya dini ya kiislamu.
Awali ya yote naomba ifahamike kuwa mimi ninaendika habari na historia ya vita vya majimaji sina dhina ya kushadidia imani ya dini yoyote. isipokuwa napenda kuchambua habari na historia ya vita hivi vya Maji Maji kama sehemu ya taaluma mimi kama mwanahistoria. Hivyo naomba nisionekane nipo hapa kidini.

Uchambuzi huu umechukua baadhi ya maandiko ya mwanahistoria mahiri Mwalimu Abdalah H. Bashir na wanahistoria wengine kama wakina I.John na Erick Cline.
Inasimuliwa kuwa licha ya vita hivi vya Maji Maji kuwa moja ya sehemu ya mapambano ya Watanganyika katika kupigania uhuru wao kisiasa, kiuchumi na kijamii bado vita hivi vilikuwa na dhana pana sana kwa waumini wa dini ya kiislamu.

Hivyo kuna mambo tutakayoayachambua ambayo yalitokea kwenye vita hivyo vya Maji Maji ambavyo vinagusa moja kwa moja imani ya dini ya kiislamu.

Kwanza miaka na sehemu zilizopiganiwa vita hivi: inasimuliwa kuwa vita vya Maji Maji vilipata kutokea mnamo miaka ya 1900. Ambapo kutokea kwa vita hivi ni matokeo ya uvamizi wa kikoloni mnamo miaka ya 1890.

Hivyo kipindi wakoloni wanaanzisha ukoloni miaka ya 1890, tayari Uislamu ulishafika Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla tangu miaka ya 600BK/BM. Hivyo wakoloni walipofika walikuta Uislamu upo na idadi kubwa ya watu walikuwa Waislamu. Kama ni hivyo katika kupambana na ukoloni kulikuwa na idadi kubwa sana ya waislamu kwa makabila yote. Kwa mfano kuna kabila kama Wayao,

Wazaramo, Wamakonde na Wandengereko bila kusahau Wamatumbi, makabila haya idadi kuwa ya watu walikuwa ni waislamu kwenye hiyo miaka ya 1900 au hata kabla ya 1900. Hivyo kupinga ukolonio kwao ilikuwa Jihadi ya kupinga Ukristo kwenye ardhi ya Tanganyika.

Lakini pia maeneo ambayo vita hivi vilipiganiwa kulikuwa na idadi kubwa ya Waislamu. Kwa mfano maeneo ya Uzaramoni, Umatumbi, Umakondeni na maeneo mengine yote ambayo yalihusika na mapambano ya vita vya Maji Maji. Hivyo kwa kuwa maeneo hayo yalikuwa yameshafikiwa na Uislamu na kuwa na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu. Basi Kuwepo kwa vita hivi ilihesabika kama sehemu ya kuupigania Uislamu kwenye maeneo hayo.
 
Uko sahihi, Baada ya Kinjikitile kutoka Mecca alirudi na holly water(Zamzam)
Maji haya ndiyo aliyotumaini kuwa yanauwezo wa kufight kinyume na Ukafiri(wakimaanisha ukristo)
Ndipo wakanawishwa na kuingizwa vitani na mwisho wa siku wakala mkenge.
Mimi nilikwenda makumbusho ya Mashujaa Songea nilijipatia historia ya vita hii lakini siri ya udini hawaisemi, yawezekana hawafahamu au wanaficha ukweli kwa maslahi ya taifa.
Kwahakika vita hii ilikuwa kama Jihad na wapiganaji wa Kitanganyika walioingia porini karibia wote walikuwa waislamu.
 
Exactly, Asante sana
 
Shule nilisoma vita vya majimaji vilipiganwa 1905/1907 sasa wewe umesema 1900/1910 hipi ni sahihi hapo.
Soma kwanza title ya hyo thread nn inasema na umalizie kusoma thread yote na uelewe huo mwaka umetajwa kwa misingi ip
 
Uko sahihi, Baada ya Kinjikitile kutoka Mecca alirudi na holly water(Zamzam)
Maji haya ndiyo aliyotumaini kuwa yanauwezo wa kufight kinyume na Ukafiri(wakimaanisha ukristo)
Ndipo wakanawishwa na kuingizwa vitani na mwisho wa siku wakala mkenge.
Mimi nilikwenda makumbusho ya Mashujaa Songea nilijipatia historia ya vita hii lakini siri ya udini hawaisemi, yawezekana hawafahamu au wanaficha ukweli kwa maslahi ya taifa.
Kwahakika vita hii ilikuwa kama Jihad na wapiganaji wa Kitanganyika walioingia porini karibia wote walikuwa waislamu.
Una uhakika!!! imeandikwa wapi kuwa Kinjeketile aliwahi kwenda Mekka??? Hakuwahi kuitwa Alhaji sijawahi kusikia akiitwa jina la Kiislamu!!! Hii dhana naona ni muflisi kabisa. Hii ni ile dhana ya kusema Mwafrika asingeweza kuji organize based on anything African except perhaps on imported beliefs or faith!!! Kinjeketile alikuwa na imani za mizimu kama mababu zetu kabla na hata baada ya kuja kwa hizi dini muflisi za ukristo au uislamu zilizotumika na watawala waliozileta kututawala, kutudhalilisha na kutufunga akili mpaka leo!!! Nani anaeweza kubisha kuwa dini hizi mfano dini ya kiislamu zilitumika kutu pacify na kuingia utumwani au ukristo na ukoloni?!
 
Wewe umetokea mkoa gani na umewahi kuingia google na wikipedia kuangalia kwa urefu kuhusu Kinjikitile?
Kama haitoshi nenda Peramiho Songea utaikuta full history of this man.
Una uhakika!!! imeandikwa wapi kuwa Kinjeketile aliwahi kwenda Mekka??? Hakuwahi kuitwa Alhaji sijawahi kusikia akiitwa jina la Kiislamu!!! Hii dhana naona ni muflisi kabisa. Hii ni ile dhana ya kusema Mwafrika asingeweza kuji organize based on anything African except perhaps on imported beliefs or faith!!! Kinjeketile alikuwa na imani za mizimu kama mababu zetu kabla na hata baada ya kuja kwa hizi dini muflisi za ukristo au uislamu zilizotumika na watawala waliozileta kututawala, kutudhalilisha na kutufunga akili mpaka leo!!! Nani anaeweza kubisha kuwa dini hizi mfano dini ya kiislamu zilitumika kutu pacify na kuingia utumwani au ukristo na ukoloni?!
 
Uko sahihi, Baada ya Kinjikitile kutoka Mecca alirudi na holly water(Zamzam)
Maji haya ndiyo aliyotumaini kuwa yanauwezo wa kufight kinyume na Ukafiri(wakimaanisha ukristo)
Ndipo wakanawishwa na kuingizwa vitani na mwisho wa siku wakala mkenge.
Mimi nilikwenda makumbusho ya Mashujaa Songea nilijipatia historia ya vita hii lakini siri ya udini hawaisemi, yawezekana hawafahamu au wanaficha ukweli kwa maslahi ya taifa.
Kwahakika vita hii ilikuwa kama Jihad na wapiganaji wa Kitanganyika walioingia porini karibia wote walikuwa waislamu.
Nilivyosoma na kufundishwa historia ni kwamba maji yaliyotumika kinga yalikuwa yanachanganywa na unga wa mtama.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya unga wa mtama na uislam?
 
Historia za darasani sometimes zinalengo la kubalance vitu.
Mfano vita ya majuzi na Amini licha ya kutokea miaka michache nyuma lakini mitaala yetu imeshindwa kuichambua vita hii kiundani.
Mfano vita ya Kagera wananchi/wanafunzi hawajapewa exactly reasons za vita, pia idadi ya Watanzania waliokufa.
Watanzania wapatao 10 elfu walikufa kwenye vita na Amini, Amini hajavamia eneo letu bali sisi tulimbambikiza kesi ili kumsapoti Milton Obbote swahiba wa Nyerere.
 
Nilivyosoma na kufundishwa historia ni kwamba maji yaliyotumika kinga yalikuwa yanachanganywa na unga wa mtama.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya unga wa mtama na uislam?
Pole kwa Kusoma tu historia ya darasani
 
Una uhakika!!! imeandikwa wapi kuwa Kinjeketile aliwahi kwenda Mekka??? Hakuwahi kuitwa Alhaji sijawahi kusikia akiitwa jina la Kiislamu!!! Hii dhana naona ni muflisi kabisa. Hii ni ile dhana ya kusema Mwafrika asingeweza kuji organize based on anything African except perhaps on imported beliefs or faith!!! Kinjeketile alikuwa na imani za mizimu kama mababu zetu kabla na hata baada ya kuja kwa hizi dini muflisi za ukristo au uislamu zilizotumika na watawala waliozileta kututawala, kutudhalilisha na kutufunga akili mpaka leo!!! Nani anaeweza kubisha kuwa dini hizi mfano dini ya kiislamu zilitumika kutu pacify na kuingia utumwani au ukristo na ukoloni?!
Jitahid kuwa mpole bila kutumia jazba,umewahi kwenda makumbusho pale ili kujua kuhusu hii maji maji!
 
Back
Top Bottom