Habari na historia nyngine ya vita vya majimaji sehemu ya kwanza

Habari na historia nyngine ya vita vya majimaji sehemu ya kwanza

Katika kusimulia historia ya Tanzania huwezi kuacha kusimulia historia ya vita vya Maji Maji ambavyo vilipata kutokea miaka ya 1900-1910. Vita hivi vilikuwa vinahusisha Watanganyika (watanzania) waliokuwa wanatoka kwenye makabila mbalimbali yaliopatikana maeneo ya kusini mwa Tanzania dhidi ya Wajerumani.

Malengo ya vita hivi yalikuwa mengi sana lakini kubwa ni kupinga utawala wa kikoloni ambao ulianza mnamo miaka ya 1890. Na maandiko mengi yanasema kuwa katika vita hivi Watanganyika walishindwa na Wajerumani walishinda na kupata nafasi ya kutawala Tanganyika.

Hakika habari za vita hivi vya Maji Maji zimeandikwa sana na wanahistoria wengi. Na tunafahamu mengi juu ya vita hivi licha ya kwamba kuna mengi yamefichwa na wengi hatuyafahamu. Ukweli ni kwamba Habari na historia ya vita hivi zimeandikwa kwa kuegemea mitazamo mingi sana, kwa mfano kuna mtazamo ya imani ya kikristo,

kuna mtazamo wa kisiasa, kuna mtazamo wa kijamii na pia kuna mtazamo wa imani ya kiislamu. Lakini pia asilimia kubwa ya watu wanaofahamu historia ya vita hivi wanafahamu katika mtazamo wa kijamii na kisiasa ambapo ndio hata shuleni hujifunza hivyo. hivyo kwa leo tutajadili kwa uchache habari na historia ya vita hivi kwa upande wa imani ya dini ya kiislamu.

Yaani tutajadili kuona jinsi vita hivi vya Maji Maji vina dhana gani kwenye imani ya dini ya kiislamu.
Awali ya yote naomba ifahamike kuwa mimi ninaendika habari na historia ya vita vya majimaji sina dhina ya kushadidia imani ya dini yoyote. isipokuwa napenda kuchambua habari na historia ya vita hivi vya Maji Maji kama sehemu ya taaluma mimi kama mwanahistoria. Hivyo naomba nisionekane nipo hapa kidini.

Uchambuzi huu umechukua baadhi ya maandiko ya mwanahistoria mahiri Mwalimu Abdalah H. Bashir na wanahistoria wengine kama wakina I.John na Erick Cline.
Inasimuliwa kuwa licha ya vita hivi vya Maji Maji kuwa moja ya sehemu ya mapambano ya Watanganyika katika kupigania uhuru wao kisiasa, kiuchumi na kijamii bado vita hivi vilikuwa na dhana pana sana kwa waumini wa dini ya kiislamu.

Hivyo kuna mambo tutakayoayachambua ambayo yalitokea kwenye vita hivyo vya Maji Maji ambavyo vinagusa moja kwa moja imani ya dini ya kiislamu.

Kwanza miaka na sehemu zilizopiganiwa vita hivi: inasimuliwa kuwa vita vya Maji Maji vilipata kutokea mnamo miaka ya 1900. Ambapo kutokea kwa vita hivi ni matokeo ya uvamizi wa kikoloni mnamo miaka ya 1890.

Hivyo kipindi wakoloni wanaanzisha ukoloni miaka ya 1890, tayari Uislamu ulishafika Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla tangu miaka ya 600BK/BM. Hivyo wakoloni walipofika walikuta Uislamu upo na idadi kubwa ya watu walikuwa Waislamu. Kama ni hivyo katika kupambana na ukoloni kulikuwa na idadi kubwa sana ya waislamu kwa makabila yote. Kwa mfano kuna kabila kama Wayao,

Wazaramo, Wamakonde na Wandengereko bila kusahau Wamatumbi, makabila haya idadi kuwa ya watu walikuwa ni waislamu kwenye hiyo miaka ya 1900 au hata kabla ya 1900. Hivyo kupinga ukolonio kwao ilikuwa Jihadi ya kupinga Ukristo kwenye ardhi ya Tanganyika.

Lakini pia maeneo ambayo vita hivi vilipiganiwa kulikuwa na idadi kubwa ya Waislamu. Kwa mfano maeneo ya Uzaramoni, Umatumbi, Umakondeni na maeneo mengine yote ambayo yalihusika na mapambano ya vita vya Maji Maji. Hivyo kwa kuwa maeneo hayo yalikuwa yameshafikiwa na Uislamu na kuwa na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu. Basi Kuwepo kwa vita hivi ilihesabika kama sehemu ya kuupigania Uislamu kwenye maeneo hayo.
Usidanganye wa2, vita ya majimaji ni ya mwaka 1905-1907, Maji yaliyotumika ni ya mto rufiji, aliyefanikisha zoezi la kichawi kuzibadili risasi kuwa Maji kupitia dawa iliyochanganywa na Maji ya mto rufiji ni bibi mmoja ambaye alikuwa Mganga wa kienyeji, na ni kweli zilibadilika hadi alipotokea msaliti(miongoni mwa wapiganaji) aliyewafahamisha wajerumani siri hiyo na kwenda kumuua yule bibi, sasa lini kinjikitile alienda makka? Uislamu umeingiaje? Acha blah blah, wanahistoria wanasema IF U DON'T HAVE FACTS DON'T SPEAK!!!
 
Hii makala niliisoma kwenye ukurasa WA Facebook unaitwa historia ya afrika. Ile page iko poa na wanaandika historia adimu sana. Pongezi kwake mwandishi. Maana nimejua mengi sana kupitia kwake.
 
Usidanganye wa2, vita ya majimaji ni ya mwaka 1905-1907, Maji yaliyotumika ni ya mto rufiji, aliyefanikisha zoezi la kichawi kuzibadili risasi kuwa Maji kupitia dawa iliyochanganywa na Maji ya mto rufiji ni bibi mmoja ambaye alikuwa Mganga wa kienyeji, na ni kweli zilibadilika hadi alipotokea msaliti(miongoni mwa wapiganaji) aliyewafahamisha wajerumani siri hiyo na kwenda kumuua yule bibi, sasa lini kinjikitile alienda makka? Uislamu umeingiaje? Acha blah blah, wanahistoria wanasema IF U DON'T HAVE FACTS DON'T SPEAK!!!
Nyie ndo walewale wa historia ya darasani unaelewa mtu akisema n ya miaka 1900-1910?au Unaongea tu ilimrad kuongea? Ulishawah kwenda makumbusho hata moja hapo ulipo? KMA huelew meng u better keep quit, usipende kukalil ww, Mwalimu kakufundisha 1905-1907,ndo umeishia hapohapo??? Halafu angalia kabla ya hzo tarh katikati na baada ya vita nn kilitokea ndo mantiki ya huu uz,, uwefuatiliaj Na makumbusho uwe unaend
 
Historia za darasani sometimes zinalengo la kubalance vitu.
Mfano vita ya majuzi na Amini licha ya kutokea miaka michache nyuma lakini mitaala yetu imeshindwa kuichambua vita hii kiundani.
Mfano vita ya Kagera wananchi/wanafunzi hawajapewa exactly reasons za vita, pia idadi ya Watanzania waliokufa.
Watanzania wapatao 10 elfu walikufa kwenye vita na Amini, Amini hajavamia eneo letu bali sisi tulimbambikiza kesi ili kumsapoti Milton Obbote swahiba wa Nyerere.
Thibitisha.
 
ahsante kwa taarifa,
naomba nielekezwe mambo kadhaa hivi..;
1. kwanini vita hii licha ya ukubwa wake wa kupiganwa eneo kubwa na kwa ushirikiano wenye mfano kabisa hata kwa vizazi vijavyo, bado haionekani kupewa kipaumbele/kupaishwa kama ya mkwawa wa iringa ambaye hadi 'movie' zimeshachezwa katika kumtukuza na kumkumbuka?!!! vipi, inawezekana ikawa udini ulioutaja ni moja ya sababu?

2. kwanini maadhimisho ya vita hivi yanafanyika songea na sio kilwa ambako vita ndo ilianzia?

naomba kueleweshwa tafadhari!!
 
Back
Top Bottom