Habari ndungu zangu.

Joyeuse

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
275
Reaction score
182
Nina tatizo la kitu kunizurura rohoni. Nikihoa naishia kutoa kohozi tu lakin chenyewe hakitoki, nikimeza hakimezeki na hata kinanikera hata nikijitapisha hakitoki. Msaada wane jaman.. Hali ina mwezi sasa..... Nimetumia dawa za kusafisha koo bila mafanikio.
 
Peleka tatizo lako kwenye jukwaa la waganga wa kienyeji utasaidiwa!
 
Mkuu Belle kaiya Pole sana kwa hicho kitu hebu tupe historia ya hicho kitu kukukwama hapo rohoni mara ya mwisho ulikula au ulikwenda wapi kula chakula?kama umetumia Dawa za kusafisha koo na hukupona basi hicho kitu kitakuwa cha Sayansi ya Ki-Afrika. Jaribu hivi kabla ya kunywa kitu chochote kile asubuhi kunywa maji yaliyotiwa chumvi glasi moja asubuhi kisha uje hapa utupe feedback.

Hilo jukwaa lipo???..Khaaa.. MziziMkavu njoo msaidie kijana...
Mkuu tedo Hujambo lakini? huyu mkuu Belle kaiya kachezewa na mambo aya kiswahili huenda ikawa hivyo .
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru MziziMkavu kwa ushauri kesho nitaa lifanyia kazi
 
Mkuu MziziMkavu.Ilianza kama mafua. Mafua yanayotokea mdomoni mafua. Nikajua mafua tu yanaganda hapo. Sasa mafua yameisha kidude mithili ya kohozi kinaendelea.
 
Flammable ushauri wako si m'baya kwani nimekuwa naota nakula karibu kila siku ila sijawahi kukwamwa na chakula hicho.
 
Flammable ushauri wako si m'baya kwani nimekuwa naota nakula karibu kila siku ila sijawahi kukwamwa na chakula hicho.

samahani lakini......usinielewe vibaya na wala sina nia mbaya.........unasali (dhehebu) wapi....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…