Habari Njema - Je Mnayajua haya?


Mkuu nimekuelewa unayoyasema! Lakini kwa ujumla labda niseme siyo kuwafurahisha wananchi! Iwe sheria kama sehem ya mgodi kufanya hivyo! Kuna kitu kinaitwa community involvement during mine design! Ni kwamba tunazungumza sheria iwabane kuwashirikisha wananchi na hao ndo wawe waamuzi wa rasilimali zao! Waseme tunataka tufanyiwe nini! Pili wapelekwe wataalam kuwaelimisha wananchi na kuwepo utekelezaji wa wakubaliano! Ni mambo ya ndani sana nashindwa hata namna ya kuyaeleza lakini kiufupi ni kuwa issue ya community involvement in mine design ndo inayoleta tija kwa wakazi! Siyo mwanasiasa awaamulie wananchi! Kwa kuangalia mambo yanayotokea Buzwagi kwa mfano inaonesha kabisa kuwa kuna mtu alifanya maamuzi kwa niaba ya wale watu!
Issue ya madini kuwepo mengi sometimes ni ya kisiasa! Unaweza ukawa na madini lakini hayachimbiki! Issue ni kuwa je haya ambayo tayari tunajua yapo na yanachimbwa yanatusaidia vipi? Wanasiasa wakienda migodini gari lake likitengenezwa na kupata kidogokidogo amechanganyikiwa! Nasikitika sana kwani tunaongozwa na mbumbu mno!
 
Madini ya uranium yanapatikana duniani kote na hayako haba kama tunavyodhani. Kutokana na hili ndiyo maana kwa wenzetu suala la radon gas kupenyeza kwenye makazi ya watu linatiliwa umuhimu mkubwa. Tofauti ni richness ya deposits.

Katika dunia ya sasa kumiliki kila kitu kuanzia mining, processing n.k. ni vigumu. Sio sustainable. Kwa mfano, kuwa na maabara ya kushughulikia madini yanayopatikana nchini tu hailipi. Gharama za uendeshaji ni kubwa mno. Na katika vitu kama hivi ni lazima iwe katika kiwango kinachokubaliwa na IAEA. It is simply not worth it.

Naamini tunachotakiwa kufanya ni kuwa makini katika utoaji wetu wa leseni. Bora kuwa na wawekezaji wachache makini kuliko kibao ambao ni speculators. Sisi tunakimbilia wingi badala ya kuangalia ubora. Kama kawaida yetu hatupendi kufanya kazi ya ziada ya kuziangalia credentials ya hao wanaokuja. Tunachojali sisi ni mapato ya haraka haraka. Na speculators ni hodari kwa kuahidi ufalme wa mbinguni wanapotaka kitu. Tatizo mara nyingi uwezo wa kutufikisha huko hawana.

Amandla.......
 
Tatizo ni kushirikiana na wazungu ambao ni wazugaji wakubwa ziko nchi ambazo zinaweza kutusaidia kikweli kweli na kuwapa elimu tosha wanafunzi,kuna chi zimeshirikiana na urusi na leo ni warushaji wa satalaiti,kuna nchi zimeshirikiana na China na leo wana chimbua mafuta.
Mfano Iran ,Pakistan ,India hawa walishirikiana na nchi hizo Urusi China ambazo zilibanwa na Marekani juu ya kueneza teknolojia lakini wanafunzi waliopelekwa kusoma huko walirudi makwao na utaalamu wa hali ya juu ,leo Muirani anatengeneza mitambo inayotumia uranium sisi huku wazungu wametuletea elimu ya kusema mifuko ya rambo ni hatari masikini viongozi wetu wakaipiga marufuku na ikawa ni kosa la jinai ukikutikana unatumia mifuko hiyo polisi wa jiji ikawa wamepata kazi ya kuwasumbua wananchi.

Ndugu amesema kuifunga migodi hii ni kurudi alikotupeleka Nyerere natumai sio kweli Kama alivyomnukuu Mwalimu kuwa hazina hii tutaitumia tutakapokuwa na wataalamu wetu wenyewe au tutakapojua kuitumia ,hapo alikuwa sawa kabisa ,ila walafi wachache wamewekwa kikao na wazungu na kurubuniwa na tulipofikishwa ni pabaya zaidi kwani kujinasua kunahitaji ukakamavu na kujiamini juu ya tulichonacho kuwa ni mali yetu na mshenzi yeyote hana amri juu yake.

Kama taifa halijapata wataalamu wa kuyatumia madini tuliyonayo ilikuwa ni kosa kuwaalika wazungu kuja kutuibia kimachomacho wakitunga mahesabu ya mamilioni ,wakijua fika maziro yakiongezeka Serikali itabwaga manyanga na kushindwa kumudu gharama hivyo ,itakuwa rahisi kwao kuingia na kuhodhi maeneo makubwa.

Wandugu ipo haja ya kushirikiana na nchi kama Urusi na Uchina naamini kabisa hawa watawafundisha wasomi wetu kwa jitihada zao za mwisho kabisa na tutaona mafanikio ndani ya muda mchache ,Nchi hizi zinahitaji urafiki wa kweli na sio urafiki wa kufuatilia interest kama walivyo wazungu wa kimarekani ambao wengi wa kampuni za huko hufuata hazina bila ya kuwajali au kuwafundisha wazalendo.

Kubwa ambalo nalo naliona ni kuwapoteza wasomi na kuwapa kazi zisizo husika tunae mzenji ambae ni msomi wa juu kwenye mambo ya nguvu za Nyuklia lakini sijui amepewa wizara gani na baada ya muda atakuwa hana kazi,aidha huu ni mkakati wa kuwapoteza wasomi ambao kwa taaluma aliyonayo anaweza moja kwa moja kuwa mtaalamu wa Nchi na kuhusishwa na mambo ya nguvu za nyuklia tu.

Tuondokane na wazungu na tuhamie Urusi China ili tusome na tusomeshwe bila ya gharama kubwa ,ioneni Libya ,Sudan hawa wanashirikiana na China na leo Sudan ni mchimbaji mkubwa wa mafuta ,haikuchukua hata miaka kumi Sudan kuchimba mafuta na sasa inapiga hatua kimaendeleo halikadhalika na Libya na tumeiona Columbia ilivyokata urafiki na Marekani na kuhamia Urusi na mwisho kusema ni bora ununue ndege ya kivita kutoka Urusi kuliko Marekani akimaanisha ukinunua kutoka Marekani unaletewa pipa tupu ulisarifu mwenyewe na spea hupewi ila ukinunua Urusi unaletewa ndege ilivyokuwa full equiped. Na free maitenance na fundi na mwalimu unaletewa kwa gharama ileile uliyonunulia ndege.
Umefika wakati wa kuachana na matapeli wa kizungu na makampuni ambayo ni wezi na wadhalilishaji wakubwa hizo kampuni za uchimbaji zote kwao ni Marekani , Canada na Australia ni danganyo tu.
Tusikubali kudhalilishwa kwa kusema au kuambiwa na kutufanya tuamini kuwa gharama za uchimbaji ni kubwa sijui ni hatari ,hakuna kisicho kuwa hatari hata kimoja mambo yote ni hatari ila hatari waliyonayo wazungu ni kubwa maana hatutafaidi chochote.
Marekani anataka kujenga infrastructure ya Tanzania ,jamani hilo si bure tazameni route alizozikusudia ,hizo zitatumika kusafirisha mchanga kutoka machimboni hadi bandari ya DSM na kupakiwa kwenye mijimeli mikubwa na kwenda kusikojulikana wameshaona kuwa kuondoka na hazina kwenye vipolo ,dili hiyo tutaisitukia sasa wanataka kusomba kwa meli.
njia ni kutengeneza barabara na huku wakiimba wimbo wa gharama za kuchimba ni kubwa na uchunguzi unachukua miaka mingi siku wakimaliza kujenga barabara basi mwezi unaofuata wataanza usafirishaji wa nguvu wakisema hapa hakuna mitambo ya kuisafisha Uranium hilo litakuwa goli jengine.

War-ridden Sudan, which only started exporting oil in 1999, during this year has become sub-Saharan Africa's third largest oil producer, only surpassed by Nigeria and Angola.

Sisi tuliokuwa au tunaoishi kwa amani na utulivu tunadanganywa kama hatuna akili uzuri ,tunavaa suti safi ,viatu mchongo tai shingoni tukionekana wasomi wa kweli na gari za kifahari zikiwa na vipeperushi ,bungeni wabunge wanasema mpaka wanatoka povu ,Sudan hao wanapiga hatua mbele leo ni yatatu na wanafaidika na matunda ya Nchi yao sisi ni watatu kwa Dhahabu lakini hakuna faida badu Nchi inaendeshwa na ujinga au tunaonekana tupo kwenye zama za mawe ,ndio maana watu wanashangaa kusikia bado tunauwana kwa mambo ya kishirikina.
 
Mwiba! Kumbe tatizo lako ni wazungu? Wa-Iran wameendeleza yalioachwa na Shah Pahlavi aliyeshirikiana sana na wazungu. Wahindi( na wapakistan), basis ya elimu ilitoka kwa waingereza, wachina nao kabla ya wakina Mao walishirikiana sana na wazungu, wajapan walianza kwa kuwaiga wazungu. Leo, Mkuu, unataka tusishirikiane na wazungu? Hao warusi mbona nao ni wazungu? Wao nao ni ushirikiano na nchi za magharibi ndiyo ziliwainua. Lugha kuu kwenye utawala wa Tsar ilikuwa ni kifaransa. Hao wakomunisti walijenga kwenye misingi iliyotegenezwa na waliowatangulia.

Leo unawatukuza wachina. Kwani hao waoshindana na wamachinga Kariakoo ni wazungu? Kwani aliyepewa TRL ni mzungu? Kwani hata huyo Richmond ni mzungu? Leo tunawapa wachina ATCL na kiwanja cha ndege. Ngoja mtatueleza nini baada ya miaka michache!

Kwa taarifa yako, urusi na uchina ( umeshasahau ya Tazara) si ile unayoijua wewe. Hawa nao hawana msalie mtume. Mbaya zaidi ni kuwa hata watakapoona dhahiri kuwa tunawaharibia vizazi vijavyo, hawatatuonya! Na sisi kwa vile hatupendi kukemewa tunafurahia na kuwaona ni wenzetu. Matunda ya mapenzi yao tutayaona baada ya muda si mrefu. Sijui tutamgeukia nani wakati huo utakapowadia.

Amandla.....
 
Hapana ila wazungu wamekuwa wakituchukulia muda mwingi,na dili ambazo ni faida kwa wananchi huwa wanatuhangaisha,na kushirikiana ni kwenye fani maalum tu ,pale ambapo tunaona ipo haja ya haraka,unaposikia wao wanashirikiana na wazungu basi ujue ni ushirikiano wa kidugu ,tofauti na kwetu ,wazungu wanatazama maslahi yao kwanza,kama ulivyosema kuwa mambo yamebadilika ni kweli ,maana Marekani imetiliwa fedha na Mchinas ili kuinua Uchumi ,kila moja sasa ni mwanamme ,tofauti bado kwetu,wazungu bado wanatuona ni mambumbu hivyo kama walivyowadanganya wazee waliopita ndio nao wanatumia hila hizo hizo.Bora tuwategemee masikini wenzetu ambao walionja umaskini lakini wameamka wamesoma na wamefahamu na sasa wako hatua nyingi mbele,hivyo hawa watakuwa na hisia za umasikini na wanajua kusaidia na wamejenga reli ya Tanzambia ,tulichoshindwa ni kuiendeleza ,na hili ni utawala mbovu tu ambao unajali maslahi binafsi hawajui kama uchumi ukianguka hata maslahi yao yataanguka na ndio tuonavyo reli wameshindwa kuzisimamia ,ndege wameshindwa kuzisimamia leo wao wanapoteza kazi na mshirika kupewa wengine ,hapo ndipo utakapoona tabia ya kushindwa na kujali maslahi inapoishia.

Sudan open to Chinese, Indian and Malaysian investors. China National Petroleum Corporation (CNPC), India's Oil and Natural Gas Corporation (ONGC) and Malaysia's Petronas are now the biggest players in Sudan's oil sector.Leo ni ya tatu kwa Afrika ndani ya miaka miaka 9 sisi tuna madini kabla ya uhuru na yanachunguzwa tokea wakati huo jana juzi ndio tumekuwa ya tatu.
Sisi tunaokumbatia wazungu wacha tusote ,wakituahidi kutufanyia uchunguzi.
 
War-ridden Sudan, which only started exporting oil in 1999, during this year has become sub-Saharan Africa's third largest oil producer, only surpassed by Nigeria and Angola.

Mwanachi wa kawaida wa Sudan anafaidika vipi na mafuta? Tukumbuke hata aliye Darfur nae ni raia.

Equatorial Guinea wana mafuta kibao. Nako niambie wananchi wake wanafaidika vipi?

Angola ni ya pili kwa kutoa mafuta lakini nako niambie wananchi wamefaidika vipi?

Nigeria ndiyo usiseme kabisa. Na Gabon ndiyo balaa!

Kote huku utawalaumu wazungu?

Chad walisaidiwa kujenga njia ya mafuta kwa makubaliano kuwa sehemu kubwa ya mapato yawekezwe kwenye maendeleo ya wananchi. Bomba lilipokamilika tu, waChad wakayatosa makubaliano na kuanza kufanya shopping ya silaha! Nako tumlaumu mzungu?
 

Sudan iliwachagua hawa kwa sababu hawakutaka kuulizwa mapato ya mafuta wanayafanyia nini. Sudan imeweza kuendesha vita kutokana na mapato haya. Hawa uliowataja hawajali kama sudan watatumia mapato hayo kuwauwa watu wa Darfur au kujenga maghorofa yasiyo na maana Khartoum. Hawajali kama sehemu kubwa inalambwa na wajanja. Wao wanachotaka ni hayo mafuta tu.
 
Mwiba. Wakati wa ujenzi wa Tazara palikuwa na shutuma nyingi tu kuwa wachina wanatuibia madini na vitu vingine. Laiti wakati ule ingekuweko JF tungejua mengi zaidi.

Hakuna mjomba huko. Ni sisi wenyewe kuwa makini. Ni sisi kuwabana tuliowachagua watutimizie waliyotuahidi wakati wakiomba kura zetu. Mkombozi wetu ni sisi wenyewe na wala si mchina, mhindi, mrusi au mzungu.
 
Can one of you moderators inform me why you delete most of my contributions on this blog.
 

Sudan wamepiga hatua kubwa hata kwa wananchi wake ,hilo tatizo la Dharfur ni hao hao wazungu wanaolitilia maji ili wapate kuingia kinguvu kama walivyoingia Iraq na Afghanistan,Dhafuri ni eneo ambalo Uranium ipo nyingi na madini mengine na ndilo linalotakiwa na Marekani ila Wasudani wapo macho na tayari Mchina ameshafika huko kuandaa machimbo ,kama hujui Mmarekani ameshindwa kuingia kwa sababu Mchina ameshawahi sasa anatumia kila mbinu ,tuliache hilo la huko tugange ya hapa kwetu.
Kwetu ni amani na utulivundio uliotawala ,hakuna vita wala hatuna vita,muamko uliokuwepo hautasababisha faida kutumiwa na wachache kwani tumeshaona yaliopo na ni fundisho tosha kwa watakaoongoza nchi. Jambo kubwa ni mikakati ya uchunguzi usiokwisha na maleseni kibao na mikataba hewa na makampuni juu ya makampuni hata hajulikani akamatwe yupi ,hapa ndipo tulipo ,na wanaoshikilia mikataba hiyo na leseni hizo ni wazungu wenye private kampuni zenye watoto kibao wakizisajili kama local kumbe wao wapo nyuma,hii ni mipango isiyo na mwisho mzuri,ukiangalia huwa wanapasiana kila baada ya miaka na vilevile kuna machimbo kibao ambayo yapo Tz lakini huwezi kujua yapo sehemu gani wala ukienda kwenye dataz haiainishwi wapi yanaendeleza machimbo yao Tz ni kubwa sana ,hivyo hata maficho ya uchimbaji yapo,utaona njia zinaelekea porini tu kumbe ni sehemu ya kubukua hazina ya Nchi.
Tunaitakia mema Nchi yetu na sio tunasema kwa kuwasakama walioko madarakani lakini wananchi na watawaliwa wanaelekea kuamka na kuchoka na ahadi za serikali . haya hayataendelea hivi hivi kuna siku watavamia na kusema kweli kuwa kama hakuna faida na gharama ni kubwa basi na wao wafunge virago waende kwao.Makampuni kibao yametia nanga Tz halafu mnasema harama ni kubwa ,hivi kama gharama ni kubwa wanafanya nini na kupokezana machimbo kama mbio za vijiti.
 
The following News was released Feb, 2007:
Tanzania: Barrick to Open $400 Million Gold Mine

The world's largest gold producer, Barrick Gold Corporation, is to invest in a new $400 million gold mine at Buzwagi in Tanzania. According to Deo Mwanyika, the executive general manager for corporate and legal affairs at Barrick Tanzania, Buzwagi is expected to generate benefits for at least 10 years as it has probable gold reserves of 2.64 million ounces. The open pit mining operation will produce between 240,000 and 250,000 ounces of gold per year.
 
SPEECH BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE INVESTING IN AFRICAN MINING INDABA XII, CAPE TOWN, SOUTH AFRICA
February 6, 2007
"I will not be bragging in saying that my country, Tanzania, contributes a sizeable share of Africa's mineral wealth. Tanzania is richly endowed with minerals of all kinds. Almost every mineral known to exist in the earth's crust can be found in Tanzania, and some exist in large quantities. Tanzania offers a stable political environment with sound legal and fiscal policies. In terms of potential, the following is what we have to offer: Excess of 45 million ounces of gold, 1.5 million tonnes of nickel and 50 million carats of tanzanite..."

Muungwana anapiga mnada halafu mnasema uchunguzi haujakamilika.
 
STATEMENT BY THE RIGHT HONOURABLE EDWARD LOWASSA (MP), PRIME MINISTER OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE BUSINESS LUNCHEON HELD IN TORONTO, CANADA
December 4, 2006
"In conclusion let me answer the question why I think you should consider seriously investing in Tanzania. First and foremost is the long experience of political and economic stability, as well as peace and security that Tanzania continues to enjoy."
 

No, No, you did not quote him properly.

Lowassa concluded by saying that:

"..... First and foremost the long experience of political and economic instability, that favours the investors, by continuing impoverishing itself, entering in bogus contract all in investors' favour. So come and enrich yourself at Tanzanian’s impoverishing opportunity cost policy”
 
Ona hii kong'oli hapo was 2005 _ UK firm buys Tanzania uranium licences ,miaka miine imemaliza exploration haijulikani wakati tokea 1978 mambo yanachunguzwa na wajeru , feza inagawiwa na kugawanywa ,uku mnatuambia uchunguzi bado unahendelea ,mi naona iyo madini inachimwba kwa nguvu tu ,yuko wapi yule waziri alidai kuwa Wanategemea kutumia au kujenga vinu vya mitambo ya nyuklia hapa Tz kwa ajili ya kupata umeme ,jamani adaiwe tarehe na muda sio kutuburuza tu,hivi alipata wapi nguvu za kusema maneno yale ,nafikiri alidanganywa kuwa na nyinyi tutawagaia na mtaweza kujenga hizo tanuri za nuclear power ,haya tukae na kungojea kugaiwa.

Na hii was 2007- http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/01/19/82626.html wakihongezea kutudanganya kuwa bei sio kubwa , sasa sisi tuone ni hasara wakati wao wanahodhi mapande ya ardhi na kupewa leseni na wao kuwagaia wenzao ,sijui washauri ,wachunguzi yaani wanarudia kinyang'anyiro cha Tanzania badala ya Afrika.
 
Madongo na kudharauliwa.

...but Tanzania, rich in uranium, seriously wants to go atomic ?
...Despite the fact that Tanzania is endowed with over 30 per cent of the total uranium deposits in Africa, the government appears not to know what to do with them.

Msola ambae ni profesa alituliwaza kwa kusema au kujibu ....:-
Along with better availability of electricity, nuclear energy would be used for medical purposes in treating cancer in four major hospitals - Ocean Road Cancer Institute, Muhumbili National Hospital, Bugando Hospital and Kilimanjaro Christian Medical Centre,"

Wananchi tunaposikia maneno hayo kutoka kwa Waziri tunafurahi na kupata matumaini lakini miaka inapita awamu za uongozi zinapishana hatuoni kitu tena ni giza tu,wala hatuna wa kumhoji matamanio yamefikia wapi ? Nani ameachiwa kuyaendeleza ,na zaidi ni hatua gani zimefikiwa na kama haitoshi ni lini tutaweza kuona gulopu ya mwanzo ikimurika kwa kutumia nguvu za Nyuklia hapa TZ.

Naibu waziri nae akazidi kuwakosha wananchi pale aliposema :- A single nuclear plant is capable of producing a minimal of 5,000MW of power, while demand in a country like Tanzania, does not reach even 1,000MW at peak

Ndipo niliposema umeme utakuwepo hadi kwenye wanyama wetu na hizo 4000MW tutaweza kuwauzia majirani kwa bei powa.

Kuna wanaosema :- It is political rather than technological reasons that have held back uranium research in countries like Tanzania.

Leo panapotakiwa kufanya jitihada za kweli na kuamua kulalia madini kuna watu wanatwambia uchumi wetu au madini kwa hapa tulipo yanasaidia uchumi wa nchi kwa asilimia mbili na wanategemea ifikapo 2025 madini yatasaidia uchumi wa Tz kwa asilimia kumi.
Je ikiwa tutaweza kutumia umeme wa nyuklia ndani ya miaka mitano ? Uchumi wetu utakuwa wapi ?
 


Mzalendo akiangalia mauzauza ya uchimbaji visima vya kupata sampuli za Uranium akiwa na meneja machimbo anaewakilisha timu ya nje ughulikia machimbo hapa Nchini.
Ona tofauti ya watu wawili hao ,mmoja amekonda na mwengine amefura na baada ya muda aliekonda ataambiwa ahame sehemu hiyo kwani kuna kazi inataka kufanywa.
 
Investment by Canadian companies in African is huge, there is a good article on this subject at Pambazuka

Looking through this article, there is reason to worry, for example


Which suggest the already signed mining contracts, giving 3% royalties to Tanzania government is still binding



Link PZN - Canada in Africa: The mining superpower

 
Sasa kabla hatujafunga mkataba nao nafikiri wataalamu wetu wangelipitia zile nchi ambazo zimefunga mkataba na hao WaCanada ili kuona mambo ambayo labda waliofunga mkataba imekuwa ni kikwazo kwao kuyatatua na huwa kama yamewafunga kutoa vilio au kujikwamua.
natumai huu mkataba upo mbioni japo hatuoni habari zake ili kama wananchi watapatiwa nakala kuona na kujadili kama kujifunga isiwe ni kwa wachache tu bali hata wananchi iwe wameshirikishwa kwa kiasi fulani,la kama ni kujifungia mahotelini na kuweka mkwaju basi , matokeo ya baadae ni mabaya.

Mikataba na mikakati :-

http://www.international.gc.ca/trad...iaux/agr-acc/fipa-apie/fipa_list.aspx?lang=en
 
Hiyo ya uranium yote wakuu ndio aliyoifwata rais mstaafu mtarajiwa
wa marekani georgr bush!!!subirini amalize muone safari za tanzania
kama kawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…