Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Sudan wamepiga hatua kubwa hata kwa wananchi wake ,hilo tatizo la Dharfur ni hao hao wazungu wanaolitilia maji ili wapate kuingia kinguvu kama walivyoingia Iraq na Afghanistan,Dhafuri ni eneo ambalo Uranium ipo nyingi na madini mengine na ndilo linalotakiwa na Marekani ila Wasudani wapo macho na tayari Mchina ameshafika huko kuandaa machimbo ,kama hujui Mmarekani ameshindwa kuingia kwa sababu Mchina ameshawahi sasa anatumia kila mbinu ,tuliache hilo la huko tugange ya hapa kwetu.
Maendeleo gani Mkuu? Kwa hiyo hao Janjaweed na wakimbizi wanaokimbiliana Chad na wenyewe ni fix ya wazungu?
Mmarekani kama nchi nyingine za Ulaya hawawezi kuwekeza Sudan kwa sababu ya mambo yanayoendelea Dharfur. Sudan amemkumbatia mChina, kwa sababu huyu mwenzetu haulizi kitu. Mnataka silaha kuchinjana? Hizi hapa, tena kwa bei poa! Uranium imejaa kibao Canada, Australia na Kazakhstan. Kwa nini hiyo ya Sudan iwasumbue? Uranium sio dili kama unavyodhani!