Habari njema kwa Diaspora wa Tanzania, Wale ambao hawajajilipua, kuwekewa utaratibu, kupiga kura-Waziri Mkuu

Habari njema kwa Diaspora wa Tanzania, Wale ambao hawajajilipua, kuwekewa utaratibu, kupiga kura-Waziri Mkuu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kuna habari njema kwa Diaspora wetu, wale Diaspora ambao wako ughaibuni na hawajajilipua, watawekewa utaratibu kuwawezesha kupiga kura.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambao mbunge fulani za Zanzibar aliuliza ni lini wana diaspora wa Tanzania, wataruhusiwa kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.

Waziri Mkuu akajibu kuwa mchakato wa maandalizi ya sera ya diaspora unaendelea, ukikamilika, wana diaspora ambao hawajajilipua, ambao bado wana uraia wao wa Tanzania, watawekewa utaratibu rasmi kuwawezesha kupiga kura kwenye balozi za Tanzania nchini mwao.

Hili pia likifanyika kwa Zanzibar, then for sure, kuna chama fulani kule kitaagwa rasmi.

My Take.
Hili ni zuri, ila wasiwasi wa ushiriki wa diaspora kwenye siasa, isije kuwa ndio sababu ya kukataliwa kwa dual citizenship, turuhusu tuu dual citizenship ila Watanzania wenye dual citizens ndio wasiruhusiwe kupiga kura.
Hili mo moja ya vilio vya muda mrefu vya wana diaspora wa Tanzania.

P
 
Be positive, hizi kura zitapigwa ki electronic, kura za kielektronic, haziibiki!.
P
Mayalla be serious saa zingine. Kura za kielektronic haziibiwi? Tena hizo ndio rahisi kabisa kuibiwa..maana anaweza akakaa kwenye laptop akadukua...haina haja tena kuanza kuhangaika na masunduku na karatasi feki za kupigia kura.
 
Diaspora wangewawekea mazingira mazuri ya kuwekeza kama kuwapunguzia kodi kwa mitambo au vifaa wanavyokuja kuvitumia pindi wanaanza kufanya uwekezaji hilo ni jambo muhimu kuliko mambo ya kura ambazo wakiamua ziibiwe zinaibiwa tuu...
 
Ni jambo jema, ila hakuna maana ya kupiga kura kuichagua serikali ambayo haita waruhusu kuwezeka, kumiliki ardhi, au kuondoa visa. Haya ni masuala ya kujadili kabla ya kuwaruhusu wapige kura.
 
Kuna habari njema kwa Diaspora wetu, wale Diaspora ambao wako ughaibuni na hawajajilipua, watawekewa utaratibu kuwawezesha kupiga kura.
This is rubbish kama hakuna tume huru ya kuratibu hizo kura toka nje. CCM will take this move to their advantage to manipulate votes to their pleasure and at leisure!
 
Wanabodi,
Kuna habari njema kwa Diaspora wetu, wale Diaspora ambao wako ughaibuni na hawajajilipua, watawekewa utaratibu kuwawezesha kupiga kura.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambao mbunge fulani za Zanzibar aliuliza ni lini wana diaspora wa Tanzania, wataruhusiwa kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.

Waziri Mkuu akajibu kuwa mchakato wa maandalizi ya sera ya diaspora unaendelea, ukikamilika, wana diaspora ambao hawajajilipua, ambao bado wana uraia wao wa Tanzania, watawekewa utaratibu rasmi kuwawezesha kupiga kura kwenye balozi za Tanzania nchini mwao.
Samahani, hivi wana Diaspora mlihesabiwa?.
P
 
Be positive, hizi kura zitapigwa ki electronic, kura za kielektronic, haziibiki!.
P
Jaribu kuwa mkweli uwe huru. Unajua wazi kilichotokea 2015, tallying center ya Chadema ilivyovamiwa na polisi, huku kina 'mwezi 1' waki-hack matokeo yaliyokuwa yanatumwa neck, na kuya-modify.
 
Back
Top Bottom