Habari njema kwa Watanzania wote wenye akili timamu

Habari njema kwa Watanzania wote wenye akili timamu

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Uzinduzi wa makala mapya ya kipindi maarufu cha Big Brother nchini Afrika Kusini umeahirishwa baada ya moto mkubwa kuteketeza studio za kipindi hicho mjini Johannesburg.

Kipindi hicho kilistahili kuanza Jumapili hii lakini waandaaji wa wa kipindi chenyewe wameamua kuahirisha uzinduzi huku wakitafuta sehemu nyingine ya kupeperushia kipindi hicho.

Hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo wa moto na kilichousababisha bado hakijajulikana kwani uchunguzi untarajiwa kufanywa.

Washiriki katika kipindi hicho kutoka nchi 14 Afrika watakuwa wanashiriki katika makala ya 9 ya kipindi hicho.

Kipindi chenyewe kinatarajiwa kupeperushwa kwa siku 99 kabla ya mshindi kutangazwa.

Mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kupokea kitita cha dola 300,000 kima sawa na kile kilichotolewa kwa mshindi mwaka 2013.

Waandalizi wa kipindi hicho Endemol na M-Net walisema kuwa juhudi za kupata sehemu mbadala ya kuendeshea kipindi hicho itakuwa kazi ngumu kutokana na ukosefu wa teknolojia inayohitajika kuendeshea kipindi hicho kwani haipatikani kwa urahisi.

''Kila juhudi italenga kupata ufumbuzi haraka iwezekanavyo kuhakikisha kuwa kipindi hicho ambacho hutazamwa na watu wengi zaidi Afrika kitaendelea.''waliongeza kusema waandalizi.

Waandalizi pia walisema kuwa washiriki kutoka Ghana walipata tatizo la viza na hivyo wakaamua kuchua raia wa Ghana wanaoishi nchini Afrika Kusini kwenyewe.

Pia washiriki wapya walitarajiwa kutoka Rwanda na Sierra Leone kwa mara ya kwanza lakini kutokana na changamoto za hapa na pale hawataweza kushiriki.

Kipindi cha Big Brother ni kipindi maarufu sana Afrika kutokana na kupendwa sana kwake, na kilianza kupeperushwa mwaka 2003. Washiriki kutoka Tanzania, Angola, Nigeria, Namibia, Zimbabwe na Afrika Kusini wamewahi kushinda katika makala ya awali.

Mnamo mwaka 2010, kipindi hicho kiligonga vyombo vya habari baada ya mshiriki mmoja kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo baada ya kumpiga makonde mshindani mwanamke.

Cc: warumi Dinazarde Pdidy Heaven on Earth The Boss faizaFox
 
Last edited by a moderator:
BBA 2010 ndo ilianzisha hii kitu ya kudisqualify baada ya Hannington kumpiga Lerato then 2011 Lotus wa Tz akatolewa. Nando naye wa Tz akatolewa tena mwaka jana.
 
Ila BBA mwaka huu inagundu bora tu isiwepo maana ilianza World cup then mshiriki wa Ghana kukosa visa then Rwanda na Siera Leone nao kushindwa jana Jumba kuungua Moto nadhani hii ni hujuma why few days before the show.. Isidingo nayo imepata pigo maana Show zao hufanyiaga hapo na zote BBA na Isidingo zinaandaliwa na Endemol.
 
Last edited by a moderator:
Tena huo moto uje utokee wakiwemo washirikiii waungue tuu
 
Mbona BBA ipo powa tuu...Soon wata-fix tatizo ns tutaendelea kupata uhondo..
 
na hicho kipya kitakachopatikana tunakioombea kiungue tu na chenyewe pia hakuna la maana kule ni upuuzi mtupu,moto asante.
 
mkuu hizo ni majibu ya sala maombi yanakuja kuwamaliza wahusika wote walio na wanaoendelea kushiriki hayo ndio maombi ....subiri awamjui mungu na ushetani wao

Amina mtumishi wa Mungu.
 
Back
Top Bottom