Habari njema kwako Bachelor mwenzangu

Habari njema kwako Bachelor mwenzangu

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,646
Habari za siku nyingi waungwana..

Ewe Bachelor mwenzangu unayehangaika kutafuta mke sehemu mbalimbali hadi huku mitandaoni bila mafanikio hii ni habari njema sana kwako......Fuatilia.

Sio jambo la ajabu kwa mtu kukuunganisha na mwanamke ambaye anahisi ni chaguo linaloweza kukufaa kuwa mkeo iwapo utaondokana na ile mentality kuwa siwezi kutafutiwa mke...

Binafsi naomba nikueleze wewe bachelor unayehitaji mke kuwa mm nipo radhi kumuunganisha bachelor mwenzangu mmoja ambaye atakuwa na uhitaji wa dhati na binti mmoja ambaye mm sina uwezo wa kumuoa kutokana na sheria na mila zetu ila ni binti ambaye kiufupi ana sifa zote za kuwa mke ambaye kamwe km mwanaume unayehitaji mke huwezi kujutia kumuoa..Yaani kiugupi hata mm kama ingekuwa sio kikwazo cha mila zetu haki ya nani nisingekuwa bachelor mpaka leo..

Ni binti ambaye hajajichanganya na harakati zozote za mapenzi ambaye 60% kwa imani yangu ninaamini ni BIKRA lakini sio kwamba ni mlugaluga wa kijijini la hasha bali ni binti aliye na akili zake ila akaamua kutulia tu,hizo 40% naziacha kwa ajili ya mashaka ya kutambua akili za wanawake...

Sipo kwa nia ya kumuuza mtu,kumpigia promo wala nia nyingine yoyote bali kumsaidia kijana mwenzangu bachelor anayehangaika kutafuta mke mwema na aliye serious ktk jambo hili.

Utakayehitaji maelezo ya kina unaweza kunifuata Pm maana maelezo mengine siwezi kuyaweka hapa ila huko nitakueleza kwa kina.

Angalizo ni kwa aliye serious tu na uhitaji wa mke playboys wenzangu tuendelee tu na misako yetu ya kawaida.

Sharing is Caring

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mkuu unatuhaminisha wema wa huyo binti hadi binafsi naogopa [emoji23] [emoji23], Anyway elewa tu watu huwa wanabadilika mkuu, leo anaweza kuwa kama malaika ila kesho na keshokutwa mambo yakawa tofauti kabisa.

Jambo la msingi ungekuja kutufundisha namna ya kuvumiliana katika mahusiano ungekuwa umesaidia mabaharia wengi.

Mahusiano mengi yanavunjika kwasababu ya mmoja kukosa uvumilivu, ila mkiweza vumiliana na kukubaliana mapungufu yenu mtafika mbali sana, maana mmoja anaweza kosea leo na mwingine akavumilia vivyohivyo ikitokea kwa mwingine basi na yeye pia atakuwa na uwezo wa kuvumilia.

Mkuu upo sahihi ila kiukweli sina uwezo wa kupredict tabia ya mtu huko mbeleni nachoweza kuzungumzia hapa ni tabia yake ya sasa so ni kweli kabisa kabisa kuwa watu wanabadilika but hii haizuii kumuamini mtu kwa tunavyomuona na kumfahamu kwa sasa so mengine ni kumuomba Mungu asaidie kutuongoza ktk njia iliyo sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom