Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanajamvi,
Natumaini mmeamka salama na wenye afya tele. Ijumaa hii na iwe mbaraka kwako.
Jumatano mbili zilizopita nilitoka dar-es-salaam kuja Moro. Sasa, siku kabla treni iliniacha. Nilichelewa kwa dakika mbili (treni ilipaswa kuondoka saa 10 kamili. Nlifika 9.57, nkakuta milango ya treni ishafungwa). Nikalazimika kukata treni ya siku inayofuata.
Jumatano nkafika saa moja kabla, nkaketi kwenye siti yangu. Safari.
Tulipofika Ruvu, mtangazaji akatwambia kuwa tungebakia hapo kwa "dakika kadhaa" kwa sababu ya tatizo la ufundi. Nkajua hazitazidi 30, kwa maana nlishampigia mke wangu aniandalie chakula nnachokipenda cha ugali, mboga fulani hivi na kachumbari ilopikwa yenye nyanya nyingi.
Bwana wee. Nusu saa ikageuka kuwa saa zima, masaa 2,3,4... Tulitoka saa nane asubuhi.
Habari Njema
Nilisoma ripoti njema leo kuwa TRC washaagiza injini za diesel. Kwa mujibu wa gazeti la "The Guardian", injini hizi zinatarajiwa kusaidia wakati ambapo kuna changamoto ya umeme, ili wananchi mambo yao yasikwame.
Akizungumza jijini Dar-es-Salaam, meneja mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, alidokeza kuwa kuna mkandarasi kutoka ulaya ambaye tayari anafanyia kazi injini hizo. Hii ni baada ya Bw. Masanja kuwahakikishia wananchi kuwa mfumo wa umeme wa SGR ni tofauti na mkonga wa taifa.
Faraja inayokuja ni kwamba gharama za injini hizo zipo tayari kwenye bajeti ya shirika hilo (kwa hiyo tutegemee kuwa utekelezwaji utakuwa wa haraka).
Ifahamike kuwa mfumo wa treni za SGR inaruhusu utumiaji wa mafuta ya diesel na umeme pia. (Hybrid engine).
isitoshe, shirika hilo lipo mbioni kuwezesha engine ambazo zina battery zinazotunza chaji ili kusaidia endapo umeme utakuwa na hitilafu.
Kuimarisha Usalama
Imebainika kuwa kuna watu fulani ambao wamekwisha kukamatwa kwa wizi wa mali za shirika (pamoja na kwamba hatujui kuwa gharama ya vifaa vilivyoibiwa havijulikani).
TRC wameweka CCTV katika maeneo yenye usalama mdogo, na wanazidi kufanya hivyo hadi watakapofunika njia nzima kutoka Dar hadi Dodoma.
Chanzo: The Guardian, December 12, 2024.