Habari ya kusikitisha: Gari la ‘mafao’ lilivyokatisha uhai wa mwalimu mstaafu na mwanawe

Habari ya kusikitisha: Gari la ‘mafao’ lilivyokatisha uhai wa mwalimu mstaafu na mwanawe

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Muktasari:

Alistaafu utumishi wa umma Oktoba 2024, akapata mafao yake na kuamua kwenda jijini Dar es Salaam kununua gari. Hakufika nyumbani akapoteza maisha ajalini akiwa na mwanawe wa mwisho na rafiki yake.
20250204_115430.jpg

Watu watatu wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Rav4 kugongana uso kwa uso na basi la abiria kampuni ya Esther Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Amesema, “ajali imetokea leo asubuhi eneo la Mdawi, watu watatu waliokuwa kwenye gari dogo aina ya Toyota Rav4 wamefariki dunia baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Esther Luxury lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam.”

Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya mashuhuda wamesema Basi jingine lilikuwa likiovateki na liliongozana na gari dogo, kisha wakati yakijaribu kurudi katika upande husika ghafla basi la Esther lilikutana uso kwa uso na Rav 4 na kupelekea tukio hilo.

Hata hivyo, Kamanda Mkomagi amesema hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na mili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.
 
Inasikitisha mno.

Binadamu tunaoamini Mungu kwa imani zetu, tujifunze katika maombi yetu kwa yale tunayoyataka; tumuombe Mungu atukubalie ikiwa tu maombi yetu tunayoomba yana heri na sisi.

Kuna wakati pasi kuelewa kwetu kile kile tunachohisi kitakuwa sababu ya furaha zetu huishia kutuletea huzuni.

Mungu awalaze mahala pepa peponi marehemu na awape moyo wa subira na tumaini waliofiwa.
 
Kwamba Mungu ndio kasabisha?
Mungu ameweka muda wa kila mtu na kuondoa, hakuna kuwah wala kuchelewa. No one will live forever, its a matter of time .
Namna ya kuondoka tu ndio zinatofautiana.
Kuna wanao ondoka wakiwa "juu ya kidonda", wapo wanaofia kwenye ndege, wapo wanaofia ICU , wapo wanaofia vitani huko DRCilimradi kila mtu ana njia yake .
 
Hakuwa dereva huyo mwl akisubili mafao huku akijifunza kusogeza gari then kajua kusogeza kaamua akanunue gari.in short barabara za mikoa ni hatari sana kwa mtu ambae hajaijua gari vizuri plus sheria za barabarani
 
Chuma #......EKU imemuua ”MEKU”

Nime-assume kama anatokea kanda hizo.
 
Hakuwa dereva huyo mwl akisubili mafao huku akijifunza kusogeza gari then kajua kusogeza kaamua akanunue gari.in short barabara za mikoa ni hatari sana kwa mtu ambae hajaijua gari vizuri plus sheria za barabarani
Hapo Tatizo si Barabara Mkuu, Tatizo ni kutokufuata sheria za usalama barabarani.
 
Hakuwa dereva huyo mwl akisubili mafao huku akijifunza kusogeza gari then kajua kusogeza kaamua akanunue gari.in short barabara za mikoa ni hatari sana kwa mtu ambae hajaijua gari vizuri plus sheria za barabarani
Kwa haraka , Mwalimu , mtoto wa mwalimu na rafiki wa mwalimu hapo ilikua kamati ya manunuzi . Mwalimu kama mtoa fedha , mtoto kama mchagua gari na rafiki kama dereva
 
Back
Top Bottom