Mzee wa Masaki
Member
- Sep 30, 2012
- 21
- 15
Muda huu hapa Masaki, yule kijana ambaye niliwahi kutoa taarifa kuwa anataka kudhulumiwa haki yake amevamiwa tena na wafanyakazi wa Manispaa ya Kinondoni na wameendelea kubomoa.
Kijana huyu juzi J'pili alikamatwa akawekwa polisi lakini baada ya kujieleza jana akaachiwa bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Inasemekana Mkurugunzi bwana Fwema amepokea shinikizo kwa Janeti Mbene ambaye anasisitiza kumtoa huyo kijana ili yeye na mfadhili wake mkuu wa uchaguzi wa CCM, mmiliki wa Double Tree waweze kukimiliki hicho kiwanja.
Muda huu nimeshuhudia kijana wa watu akihangaika kuwasihi wabomoaji wasiendelee na ubomoaji lakini wamegoma. Mwanasheria wa Manispaa ametoa ushauri wake lakini umegomewa na ubomoaji unaendelea.
Inasemekana wakati Janeti anaenda Dodoma kwenye uchaguzi wa CCM alimhakikishia tajiri wa Double Tree kuwa hilo eneo atalipata tu na asiwe na wasiwasi na akaahidi akirudi toka Dodoma atashughulikia na ujenzi wa parking ya magari utafanyika hivi punde. Tajiri huyo alifurahi sana na akamwagia Janeti Mbene mapesa na ndiyo maana ubomoaji unaendelea mpaka sasa.