HABARI YA MAANDAMANO YA WAMASAI IMEFUNIKWA NA HABARI YA RPC

HABARI YA MAANDAMANO YA WAMASAI IMEFUNIKWA NA HABARI YA RPC

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Jana palikuwa na maandamano ya wamasai ya amani, miongoni katika baadhi ya malalamiko yao mengi walilalamika kwamba wanazuiwa haki ya kupiga kura ilahali wafungwa (prisoners) wanaruhusiwa kupiga kura wakiwa huko magereza.

Pia wamelalamika kukosa haki ya afya bora, elimu bora, makazi pamoja na chakula.

Kwa wale waliofatilia bila shaka waliona hasara na athari kubwa zilizotokea, kwa sababu magari yakiwemo ya utalii yalipata shida ya kuingia na kutoka hifadhini.

Soma: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe

Kwa upande mmoja watalii pamoja na kambi zilizopo hifadhini waliathirika sana, lkn pia WAMASAI walipeleka picha nyingine kabisa/kuufikisha ujumbe huko duniani ambapo kiukweli serikali inapaswa itoke hadharani itoe ufafanuzi na kumaliza swala hili haraka iwezekanavyo bila kuathiri uchumi wa nchi na ustawi wa wananchi hao(jamii ya maasai).

Vyombo vya habari nchini havikueleza kwa kina wala havikuonyesha nini haswa kinaendelea na ikiwa pia kama yale ambayo jamii ya Maasai waliyokuwa wanapazia sauti dhidi ya serikali ni ya kweli ama laa.

Picha iliyoonyeshwa na vyombo vya habari kwa siku ya jana sio nzuri kabisa, na bila kupindisha maneno Ina dalili mbaya na inaondoa uangavu na fikra pevu kwamba kuna uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

Ni matumaini yangu kwamba serikali yetu sikivu itatoka hadharani na kutolea ufafanuzi tukio la jana na ituahidi wananchi kwamba itajitahidi kumaliza jambo hili kwa haki na amani bila malalamiko na maumivu yoyote kwa pande zote. (Serikali na wananchi wamasai)

Kwa upande mwingine swala hili lilikuwa liwe mjadala lakini limefunikwa na mjadala wa RPC wa Dodoma aliyehamishiwa makao makuu.

Huko mitandaoni nimeona kila msanii akilalamika na kutaka haki itendeke. KIUKWELI habari ya WAMASAI imefunikwa kabisa na haiongelewi na vyombo vya habari vimetulia . Hii inaashiria nini?

Hivi ni kwamba hakuna wasanii ambao wanafuatilia maswala mengine ya jamii? Kuna wasanii wengi wamefika maeneo ya wamasai na kufanya filamu, wengine muziki lakini leo hii hatuwasikii wakitumia ushawishi wao kuomba serikali ikae mezani na wamasai

Kiongozi mmoja wa zaman huku Afrika mashariki aliwahi kusema hivi, nanukuu "there is freedom of speech but can not guarantee freedom after speech"

Ngaiwoye nikiwa hapa Endulen.

 
Back
Top Bottom