Habari ya mjini kwasasa ni Msoga marathon, kuunguruma Jumamosi hii Juni 29 ili kwenda kusaidia huduma ya afya ya mama na mtoto

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
HABARI YA MJINI KWASASA NI MSOGA MARATHON, KUUNGURUMA JUMAMOSI HII JUNI 29 ILI KWENDA KUSAIDIA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

šŸ’„Usajili wake unaendelea nchi nzima, Zoezi la Ugawaji Vifaa kwa ajili ya kukimbia na Msoga Marathon linaendelea

šŸ’„Jisajili sasa upate vifaa vyako ili Jumamosi tukate upepo huku tukisaidia kuboresha afya ya Mama na Mtoto. Usafiri utakuwepo wa kwenda na kurudi

Hatimaye ni Jumamosi hii Juni 29, 2024. Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kushirikiana na Viongozi wenzake wa Chalinze wamekuja na MSOGA HALF MARATHON kwa ajili ya kukimbia wakati huo huo kuchangisha fedha ili kwenda kuboresha huduma za Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Wilaya ya Msoga.

Kutakua na Mbili za aina 3 kwa maana Km 5, Km 10 na Km 21 na lengo ni kuchangisha na kukusanya zaidi ya Milioni 330 ili kwenda kununua vifaa na kuboresha huduma za Afya kwa Mama na Mtoto pale Msoga Hospitali ambayo inahudumia wananchi wengi sana wa Wilaya ya Bagamoyo.

Jisajili sasa kwa Tigo kwa kupiga *150*01# kisha nenda namba 5 halafu 6 halafu 1 hatimaye 1 utakuta Msoga Half Marathon utajisajili kwa Tshs 35,000/= ili tukimbie huku tukienda kusaidia kuokoa vifo vya Mama na Mtoto. Kwa LIPA NO: 15840234 (MSOGA HALF MARATHON).
IMG-20240624-WA0007.jpg
IMG-20240623-WA0009.jpg

Kwa Mawasiliano zaidi piga 0782573880 au 0762210253 au 0713258815
 
Riz1 anashindwa vipi kutoa 330M ktk hiyo hospital? Mahela yote aliyokua nayo, hadi achangishe waja? Lol
 
Ni muendelezo tu wa mambo mengi ya kijinga nchini. Hakuna kitu hapo.
 
View attachment 3024252View attachment 3024253
View attachment 3024254
Kwa Mawasiliano zaidi piga 0782573880 au 0762210253 au 0713258815
Andiko kutakuwa na mbio za aina 3 siyo kutakua na mbili za aina 3 pia jaribu kutofautisha maneno haya mawili, kutakuwa na kitakua
 
Karibuni watanzania wote tuwaunge mkono watanzania wenzetu wa Msoga-Chalinze katika jambo hili la kuchangia matibabu ya mama na mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto wakati na baada ya kujifungua.
Afya ya mama na mtoto ni jambo la kupewa kipaumbele kwa ustawi wa jamii, hivyo kwa umoja wetu watanzania tuungane na wana Msoga kuchangia uboreshaji wa huduma za mama na mtoto kwa kushiriki mbio za Msoga Half marathon zitakazofanyika tarehe 29 June 2024 kijijini Msoga kwa mujibu wa Tangazo lililotolewa.
 
MSHNDI ATAPATA NN?
Mshindi atapata medali kwa kuonesha ushirikiano wa Marathon.
Lengo la Marathon ni kuonesha umoja wa ushirikiano katika kutangaza jambo husika katika jamii ili kukuza na kuonesha mshikamano kama Watanzania.
Msoga Half Marathon ni moja ya jambo lakuungwa mkono kwa kuonesha nia ya kuboresha afya ya mama na mtoto.
Karibuni tujumuike pamoja kwa lengo la kuongeza tabasamu kwa mama na mtoto
 
Riz1 anashindwa vipi kutoa 330M ktk hiyo hospital? Mahela yote aliyokua nayo, hadi achangishe waja? Lol
Hilo ni jambo linalohusu matibabu kwa mama na mtoto kwa eneo lote la Msoga, Chalinze na mkoa wote wa Pwani kwa ujumla.
Hivyo tunatakiwa kumuunga mkono Mh Ridhiwan kwa uthubutu wa kuanzisha Msoga Half Marathon kwa lengo la kuboresha huduma ya mama na mtoto.
 
Waturuki hawaangushi ng'ombe tuje kula nyama
Nyama zilishaisha tangu jumatatu baada ya Iddi,
Karibu tuchome mafuta ya mwili na kuongeza connection za ushirikiano huku tukiongeza tabasamu kwa mama na mtoto kwa kushiriki Msoga Half Marathon.
 
Ni muendelezo tu wa mambo mengi ya kijinga nchini. Hakuna kitu hapo.
Sio kweli ulichoandika, Msoga Half Marathon ni jambo la kheri kwa uthubutu wa kuunga mkono juhudi za kuboresha afya ya mama na mtoto hospital ya Msoga Chalinze na Tanzania kwa ujumla.
 
Hiyo afya ya mama na mtoto kwenye mahospitali yote nchini hamuwezi kuiboresha kwa kupunguza matumizi yenu yasiyo ya lazima, na kuzielekeza hela zote huko?
 
Hospital ya Msoga ni hospital mpya iliyokumbana na dharula ya kutokea kwa dharula ya vifo vya mama na mtoto, hivyo kusubiri hadi bajeti ya serikali itakayoboresha mahospital yote nchini itapelekea kuongezeka kwa vifo vya mama na mtoto.
Hivyo katika moja ya jitihada za kupunguza vifo vya mama na mtoto Mh Ridhiwan akaandaa Msoga marathon kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba kwa ajili ya mama na mtoto.
Karibu sana Msoga Marathon tarehe 29 June 2024 kwa ajili ya afya ya mwili, ushirikiano na kuchangia vifaa tiba kwa mama na mtoto
 
Back
Top Bottom