Hapana, Mkuu. Ninachokupinga ni kuwa unajaribu ku-demonize homosexuality kwa kutumia kisingizio cha kulinda morals za minor wetu! Hiki kitendo kwangu mimi ni insidious. Ingawa unajaribu kukwepa lakini mifano yako ya kuwa homosexuals wana corruptive influence katika jamii (uki-quote wagiriki wa kale) na kuwa ni criminal act inakusuta. Unamorph homosexuality na ushoga, kitu ambacho si sahihi. Homosexuals ni wote wanaotendewa na wanaotenda wakati katika jamii yetu shoga ni yule anayetendewa tu. Huyu ndiye tunaemlaani wakati mtendaji tunamkubali! Unawashutumu mashoga na wasagaji kuwa wana corrupt minors wakati ushahidi wote ni tofauti na hapo. Maishani mwangu ni shoga mmoja tu ambae nimesikia akiwarubuni vijana. Huyu alikuwa mwalimu mmoja wa kihindi katika shule ya Tambaza. Lakini ni mara chungu mzima nimesikia habari za wale ambao wanajihesabu kuwa wanaume rijali wakiwabaka watoto wadogo wa kiume au vijana wa kiume walioonekana kuwa wana mienendo ya kike! Magazeti yetu yamejaa kesi kibao za hao wanaojihesabu kuwa heterosexuals wakiwabaka watoto wadogo lakini wewe una-insinuate kuwa ni hawa homosexuals ndiyo wanao corrupt watoto wetu?
Tofauti na unachotaka kusema, sipingi serikali kuwa na miongozo ya kitu gani kinapaswa kuwa accessible kwa minors (Teens sio lazima awe minor). Napinga aina zote za child pornography ( hetero au homo). Napinga accessibility ya hardcore na hata softcore porn kwa minors. Tofauti yangu na wewe ni kuwa kupinga kwangu hakuna maana kuwa masuala yanayohusu ngono hayana nafasi katika public arena. Naamini ni kwa kuyazungumza wazi wazi ndiyo hao minors watajifunza namna ya kuwa responsible katika behaviour yao. Sasa tuki -criminalize maneno kama kusagana, kubaka, kujichubua, dildos n.k. tunawafundishaje hawa vijana wetu athari za kuendekeza mambo haya?
Maneno aliyoyatoa Waberoya ni offensive lakini hauwezi ukayaita pornographic. Binafsi, sioni tatizo la kuyatumia mbele ya watoto. Kwa mfano kuna ubaya gani mtu kukiri kuwa yeye ni msagaji? Au mtu kulia kwa mahaba? Mbona hatuoni tatizo kuimba kuwa nalia kwa mahaba? Tatizo ni kuwa hiki kitu kiko kwenye print? Vile vile sioni tatizo kuzungumzia hicho kifaa kinachofanana na utupu wa mwanaume kama vile kuzungumzia utupu wa mwanaume au mwanamke. Matatizo ya hizi false morals katika jamii yetu zinatuzuia hata kuzungumzia vitu ambavyo ni basic. Kama tunaona aibu kuzungumzia sanitary pad ( nakumbuka jinsi tangazo la Always lilivyopigwa vita), tutamfahamisha vipi binti yetu kuhusu mabadiliko katika mwili wake? kama tunaona aibu kutaja kondom na utupu wa mwanaume, tutamfundisha vipi kijana wetu namna ya kuepukana na haya magonjwa ya siku hizi?
Hivi kweli, Waberoya unaamini kuwa tusipozungumzia usagaji basi vitendo hivyo havitafanyika? Mbona Zanzibar wana ngoma ya sumsumia hata kabla ya magazeti ya udaku kuanza kutamba hapa kwetu? Mbona kwenye Chakacha ( ambako watoto wadogo hawazuiwi kuhudhuria) mashoga wamekuweko miaka nenda rudi? Tunataka kumdanganya nani kwa hizi false morals zetu?
Inawezekana, Mzee mwanakijiji alikuwa na nia nzuri lakini mfano alioutumia na maelezo yake ya baadae yanachofanya ni kumwaga petroli kwenye homophobia iliyotanda katika jamii yetu. Hiki ndicho ninachokipinga.
Amandla.....