Habib Kyombo amefunga mabao 6 mechi 15, Kambole amefunga mabao 2 mechi 40, nani kalamba dume?

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Simba Leo imeanza kutambulisha wachezaji wake wapya kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, Leo wamemtambulisha mshambuliaji hatari wa mbeya kwanza, Habib Kyombo, anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa baada ya Mosses Phiri.
Usajili wa Kambole umepokewa kwa hisia tofauti, wapo wanaombeza na kudai Simba imefilisika na haina uwezo wa kifedha, wapo wanaosifia kwa kusema kuwa Kyombo ni mzuri na atasaidia sana.
Mimi nakubaliana na wale wanaosifia usajili wa Kyombo, Habib Kyombo ana uzoefu sana kwa wachezaji wa hapa ndani, Leo nchi haina mshambuliaji wa kati ukiondoa Mbwana Samatta, Stars tunaiona ikihangaika na George Mpole na Kibu Dennis kama washambuliaji wazawa wa kutuvusha, hakuna tena mshambuliaji wa kati ambaye tukimtaja watu wanaweza kusema kweli tumepata mtu.
Habib Kyombo ni chaguo sahihi kabisa, Habib Kyombo ambaye aliwahi kuchezea Mamelod Sundowns kabla ya kuumia, atakuja kuwajibu wanaombeza uwanjani, namshauri afanye mazoezi kwa bidii, ajitume, kwa timu kama Simba anaweza kuwaprove wrong critics wote.
Bahati nzuri mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi, ikiwa kama Kyombo kafunga mabao 6 katika mechi 15 watu wanambeza vip huyo Kambole aliyefunga bao 2 tu katika mechi 40, nani zuzu hapo?
 
Wamezingua sana kuweka attention kubwa kwa mashabiki tukidhani mchezaji anayetambulishwa ni wakimataifa kumbe hamna kitu ni level za kina mhilu

Wametukosea sana mashabiki kwa kweli
 
Shida ya makolo wengi hawana akili. Hawajui jema wala baya. Badala ya kusema ukweli timu yenu ifanye vizuri mnakalia majungu. Unamfananisha kambole mchezaji aliyecheza ligi bora yenye ushindani na wachezaji wenye quality na mchezaji habib ambaye timu yake tu yeyote anapata namba.
 
Huyo Kombole alichezaje hizo mechi 49 alizofunga magoli 2 kama alikuwa hapati namba?
 
Kwani huyo Kyombo hajacheza ligi bora?
 
Mashabiki wa mpira wa Tanzania wengi hata hawajui nini ni nini. Habib Kiyombo kwangu ni mchezaji sahihi wa ndani mbadala wa Captain Fantastic John Bocco. Ukiwauliza watu nani walimtaka atoke ndani ya nchi kwenda kuwa striker pale Simba, watabaki wanaumauma midomo. Habib ni mchezaji sahihi toka ndani ya nchi kwa nafasi ya CF pale Simba.
 
Mashabiki wa mpira wa Tanzania wengi hata hawajui nini ni nini. Habib Kiyombo kwangu ni mchezaji sahihi wa ndani mbadala wa Captain Fantastic John Bocco. Ukiwauliza watu nani walimtaka atoke ndani ya nchi kwenda kuwa striker pale Simba, watabaki wanaumauma midomo. Habib ni mchezaji sahihi toka ndani ya nchi kwa nafasi ya CF pale Simba.
 
Nyie endeleeni kuchezea shilingi chooni, Kwa usajili mnao ufanya zipo Dalili za timu kushuka Daraja.
Sasa msitegemee Yanga awe anafanya kazi ya kuwabeba Ili msishuke Daraja kama Walivyo fanya 1989. Acheni siasa fanyeni usajili, msimu ujao ni mgumu kuliko huu ulio Isha.
Mtakuja kumlaumu Karia bila Sababu
 
Kwenye ligi gani?
 
Wamezingua sana kuweka attention kubwa kwa mashabiki tukidhani mchezaji anayetambulishwa ni wakimataifa kumbe hamna kitu ni level za kina mhilu

Wametukosea sana mashabiki kwa kweli
I feel you Brother
 
Amesajilwa kwa maelekezo ya kocha kulingana na uwezo wa klabu, fyateni mkia.mnacha kudai 20bilioni mpate wachezaji mnaowataka.mnatupotezea muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…