Simba Leo imeanza kutambulisha wachezaji wake wapya kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi, Leo wamemtambulisha mshambuliaji hatari wa mbeya kwanza, Habib Kyombo, anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa baada ya Mosses Phiri.
Usajili wa Kambole umepokewa kwa hisia tofauti, wapo wanaombeza na kudai Simba imefilisika na haina uwezo wa kifedha, wapo wanaosifia kwa kusema kuwa Kyombo ni mzuri na atasaidia sana.
Mimi nakubaliana na wale wanaosifia usajili wa Kyombo, Habib Kyombo ana uzoefu sana kwa wachezaji wa hapa ndani, Leo nchi haina mshambuliaji wa kati ukiondoa Mbwana Samatta, Stars tunaiona ikihangaika na George Mpole na Kibu Dennis kama washambuliaji wazawa wa kutuvusha, hakuna tena mshambuliaji wa kati ambaye tukimtaja watu wanaweza kusema kweli tumepata mtu.
Habib Kyombo ni chaguo sahihi kabisa, Habib Kyombo ambaye aliwahi kuchezea Mamelod Sundowns kabla ya kuumia, atakuja kuwajibu wanaombeza uwanjani, namshauri afanye mazoezi kwa bidii, ajitume, kwa timu kama Simba anaweza kuwaprove wrong critics wote.
Bahati nzuri mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi, ikiwa kama Kyombo kafunga mabao 6 katika mechi 15 watu wanambeza vip huyo Kambole aliyefunga bao 2 tu katika mechi 40, nani zuzu hapo?